Tafuta

Vatican News
 Kardinali Peter Erdo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Budapest nchini Hungary Kardinali Peter Erdo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Budapest nchini Hungary  (Vatican Media)

Kard.Erdö: Ekaristi ni kisima cha imani yetu na mlango wa maisha

Katika mahubiri ya Kardinali Erdo Askofu Mkuu wa Budapest, kwa kuongozwa Injili ya siku, wakati Mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Papa Leone Mkuu,ametazama kwa karibu sura ya Mtakatifu huyo kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kongamano la Ekaristi Kimataifa,Roma

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 10 Novemba 2018, Kardinali Péter Erdő Askofu Mkuu wa Budapest ameadhimisha misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa washiriki wa Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa, kufuatia na maandalizi ya Kongamano lijalo la  Ekaristi Takatifu Kimataifa  linalotarajiwa kufanyika kunako mwaka 2020 huko mjini Budapest nchini Hungary.

Karidinali Erdö  amasema:Ni furaha kubwa kuweza kuadhimisha Ekarisiti katika Sikukuu ya Mtakatifu Leone Mkuu,  hapa katika Kanisa Kuu la Matakatifu Petro. Papa Leone alikuwa wa kwanza katika historia na ambaye alistahili wakati huo kuitwa “mkuu”. Baada ya kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II, tumesikia hapa Roma watu wanasema kifo cha Yohane Paulo Mkuu. Haya ni matokeo ya kina ambayp alikuwa nayo hata Mtakatifu Leone Mkuu wakati wa  maisha ya Kanisa na kwa maana hiyo yanafananishwa na yale ya Mtakatifu Yohane Paulo.

Maandalizi ya Kongamano la 52 la Ekaristi Takatifu Kimataifa

Akiendelea na mahubiri hayo amesema, wamekusanyika Roma kwa ajili ya kuandaa Kongamo la 52 la Ekaristi Takatifu kimataifa. Ni kumshukuru Bwana kwa uwezakano mkubwa huo wa ushuhuda na kujipyaisha kiroho. Wanapoadhimisha Ekaristi, wanaadhimisha Yesu Kristo mwenyewe. Hiyo ni dharura muhimu katika nyakati za sasa za kutangaza wazi Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwalimu wetu ambaye hata  sisi wakristo wa Karne ya XXI ni mitume wake. Utu wake, mafundisho yake ni kiini cha imani yetu. Ni yeye anayetupatia maji ya uzima, neema tele na Roho Mtakatifu. Ekaristi ni kisima cha imani yetu na yeye ni mlango wa maisha na amani katika mioyo yetu na katika dunia nzima.

Mtakatifu Leo alitoa mchango mkubwa kwa namna ya pekee uwazi wa mafundisho

Mtakatifu Leo alitoa mchango mkubwa kwa namna ya pekee ya uwazi wa mafundisho ya kikristo kuhusu utu wa Yesu Kristo. Kardinali Erdo anasema: Katika Dogma maarufu, yeye anasema kwamba:  katika  Yesu Kristo hakuna aina mbili za utu. Neno kufanyika Mungu na Yesu Kristo ni kitu kimoja, ni mtu mmoja ambaye kweli ni Mwana wa Mungu na Mwana wa Binadamu  ni Mungu Mtu kwa hakika (Ep.28,4) Katika mtu, kuna asili mbili, ya umungu na binadamu, lakini bila kuchanganyikana. Kwa msingi huo ni wazi kutambua juu ya Yesu Kristo na wakati huo huo, Mtakatifu Leone Mkuu ni shuhuda wa kuthibitisha uwepo halisi wa Kristo katika Ekaristi. Yeye kwa dhati anasema:” Mnapaswa kula mwili wake bila kuwa na wasiwasi au bila kuwa na hofu juu ya ukweli wa mwili na damu ya Kristo (Serm, 91,3) Papa Mtakatifu Leone anafundi kuwa, kushiriki mwili na damu ya Kristo inambadili mkristo kwa kile anachokila ( Srm 64,1). Kutokana na  Mtakatifu Leone Mkuu pia anaonesha wazi kwamba Ekaristi inafikiriwa kuwa ni sadaka(Serm 91,3).

Kardinali Erdo akiendelea kuelezea wasifu wa Mtakatifu Leone Mkuu kuhusiana na matatizo aliyo yapata wakati wa uongozi wake, amethibitisha kwamba hata leo hii  wao wamzungukwa na jumuiya za waamini katika mazingira ambayo ni tofauti na wakati huo huo wengine wanapata vizingiti vingi. Hata leo hii wanaongoza jumuiya za mapadre, wanaoshikirikiana karibu sana na waamini ambao wanahusika katika mwili mtakatifu wa Kristo.

Kanisa lipo kwa sababu ya Uinjilishaji na jumbe wa Injili ni wa lazima  

Katika kujitoa ni kujikita kwa upendo na waajibu katika fumbo la imani ambayo waliipokea kutoka kwa Yesu Kristo Bwana na Mwalimu anathibitisha na kuelendela kusema: Leo hii waamini wanajifunza wazi ukarimu kwa wote waliombali na ambao wanapaswa kwenda katika utume wa kutangaza Injili kama vile Mtakatifu Paulo VI alivyo andika kwamba: Kanisa lipo kwa sababu ya Uinjilishaji; na jumbe wa Injili ni wa lazima. Ndiyo njia, ambayo haiwezi kubadilishwa. Haijali mambo ya  utofauti na wala mahali pazuri, kwa sababu ya wokovu wa watu. Hiyo inawakilisha uzuri wa maonesho na ambao huchukuliwa kwa hekima ambayo haiwezi kupatikana katika  dunia hii!

Amehitimisha mahubiri yake Kardinali Erdo akisema: “Na ili kuweza kutimiza utume huo leo hii katika ulimwengu, inabidi kuandaa Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa na kuomba kwa njia ya maombezi ya Watakatifu Mapapa  kwa namna ya pekee leo hii Mtakatifu Leone Mkuu Amen”.

 

 

10 November 2018, 14:34