Tafuta

 Wat Phra Chetuphon, ni hekalu la wabudha, nchini Thailand Wat Phra Chetuphon, ni hekalu la wabudha, nchini Thailand 

Ukristo na Ubudha ni daraja rafiki katika dunia isiyo na amani!

Katika Ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini katika fursa ya maadhimisho ya miaka 230 ya Hekalu la kifalme la Chetupon, nchini Thailand , Askofu Ayuso Guixot amethibitisha juu ya uhusiano mzuri wa kirafiki kati ya wabudha na wakatoliki na kwamba ni daraja la urafiki katika dunia iliyojaa vurugu na malumbano

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufuatia na mwaliko wa Phra Thepweeraporn, abate wa Wat Phra Chetupon, Monsinyo. Miguel Ángel Ayuso Guixot, Katibu wa Baraza la Kipapa la Ushauri na Mazungumzo ya kidini na monsinyo Indunil Janakaratne Kodithuwakku Kankanamalage, katibu msaidizi wa Baraza hilo kwa upande wa wabudha tarehe  9 Novemba, wametembea  mjini Bankok kwa ajili  sherehe za miaka 230 za Hekalu la kifalme la Chetupon (Wat Pho). Wawakilishi hao, wamekuwa na Askofu Mkuu Paul Tschang In-nam, Balozi wa Vatican huko Bankok  na Padre Dario Pavisa, Katibu wa Balozi huyo na wawakilishi wa Kanisa katoliki mahalia.

Ufuatao  ni ujumbe wa  Askofu  Miguel Ángel Ayuso Guixot

Ufuatao  ni ujumbe wa  Askofu  Miguel Ángel Ayuso Guixot, M.C.C.J, Katibu  mkuu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini wakati wa sherehe hizo: Mheshimiwa PhraThepweeraporn, Baba Mtakatifu anafurahi kupokea taarifa za maadhimisho ya miaka 230 ya hekalu la Wat Phra Chetuphon (Wat Pho)  zilizo anza tarehe 1- 11 Novemba 2018. Amenirihusu na kwa niaba yake  kuwakilisha salam zake na matashi mema nikiwa na wawakilishi wote  kwako na Mkutano Mkuu wa Sangha ya Helalu Phra Chetuphon ikiwa pamoja na Wabudha wote wa Thailand katika fursa hii. Ni heshima kupata mwaliko huu katika tukio la kumbukumbu hii, na kwa dhati ninatoa shukrani zetu kupata mwaliko huu. Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini linapongeza urafiki uliopo kati ya Hekalu la Wat Pho na Kanisa Katoliki. Kwani  Mfalme Rama VII wa Thailand alimtembelea Papa Pio XI kunako tarehe 21 Machi 1934 na alimzawadia Papa Nakala ya Phra Malai, ambalo ni andiko Takatifu la Kibudha liloandikwa katika maandishi ya kizamani ya alfabeti ya Khmer”.

Tarehe 16 Mei 2018 kukabidhi Tafsisi za maandiko ya kizamani kwa lugha mbili ya Pali na Thai

Kufuatia na maombi kutoka Jumba la Makumbusho Vatican, kikundi cha wataalam wa kibudha wa Hekalu la Chepton walitafsiri kitabu kwa lugha mbili ya Pali na Thai. Tarehe 16 Mei 2018, wawakilishi karibia 50 mamonaki wakibudha, na wawakilishi wa serikali na wakiongozwa na Mkuu Phra Thepweeraporn, walimzawadia Baba Mtakatifu nakala ya tafsiri wakati wa Mkutano wa faragha. Katika fursa hiyo, kadhalika Papa Francisko alionesha furaha yake juu ya hekalu la Wat Pho na kusema: “ Ni maonesho ya ishara ya ukarimu na urafiki tunaoushirikishana kwa miaka mingi , ni safari inayotengenezwa kwa hatua fupi ( hotuba kwa wawakilishi wa Wabudha kutoka thailan, tarehe 16 May 2018)

Uwakilishi kukuta na Papa Paulo VI, tarehe 5 Juni 1972

Aidha Uhusiano mzuri wa kudumu wa kirafiki na ushirikiano wa pamoja ni wa muda mrefu ambao ulianza na wawakilishi wa kwanza wa Wamonaki wa kibudha kutoka Thailand kuna mwaka  tarehe 5 Juni 1972 na ambapo waliweza kukutana na Baba Mtakatifu Paulo VI. Katika fursa hiyo Papa alisema “Ni matumaini yetu kukuza  urafiki wa mazungumzo na ushirikiano kati ya tamaduni mnazoziwakiisha na Kanisa Katoliki.  Na Mmoja wa wamonaki 3 katika wawakilishi hao ambaye alikuwapo ni  Somdej Phra Wanaratana, abati mstaafu wa Hekalu la  Wat Phra Chetupon (Wat Pho), ambaye alikuwa amechaguliwa katika Mkutano Mkuu wa 17 wa  Upatriaki wa Ufalme wa Thailand.

Ziara yao iwe mchango fungamani katika kujenga madaraja katika dunia iliyojaa vurugu na ukosefu wa amani

Uwepo wetu leo hii ni ishala wazi kwa ajili ushirikiano wa urafiki. Tunachukua nafasi hii kuwshuru Mkutano mkuu wa Sangha wa Wat Pho katika kuendeleza msimamo wao wa mazunguzmo ya kidini. Ziara yetu ya leo inaweza kutoa mchango mkubwa na fungamani katika kujenga madaraja leo hii katika ulimwengu unaosumbuliwa na vurugu, ukosefu wa Amani  na matokeo ya mateso ya mamilioni ya watu. Tunarudia kwa upya kushukuru kukaribishwa na kuwatakia furaha na maana ya utamaduni na roho ya maadhimisho!

 

 

09 November 2018, 15:24