Tafuta

Vatican News
VAskofu mkuu Dagoberto Campos Salas ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sierra Leone na ataendelea pia kuwa Balozi nchini Gambia VAskofu mkuu Dagoberto Campos Salas ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sierra Leone na ataendelea pia kuwa Balozi nchini Gambia 

Askofu mkuu Dagoberto Salas ateuliwa kuwa Balozi nchini Sierra Leone

Askofu mkuu Campos Salas alizaliwa tarehe 14 Machi 1966 huko Tilaràn, nchini Costa Rica. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 22 Mei 1994.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Dagoberto Campos Salas kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sierra Leone na ataendelea kuwa pia Balozi wa Vatican nchini Liberia na Gambia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Campos Salas alizaliwa tarehe 14 Machi 1966 huko Tilaràn, nchini Costa Rica. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 22 Mei 1994.

Askofu mkuu Campos Salas Alianza utume wake kuliwakilisha Kanisa katika masuala ya kidiplomasia tarehe 1 Julai 1999 na kubahatika kutumwa sehemu mbali mbali za dunia, lakini hasa nchini Sudan, Chile, Sweden, Uturuki na Mexico. Tarehe 28 Julai 2018 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Gambia na kuwekwa wakfu tarehe 29 Septemba 2018, wakati Mama Kanisa alipokua anaadhimisha Siku kuu ya Malaika Wakuu: Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Ibada ambayo iliongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Tarehe 17 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amemteua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sierra Leone.

Sierra Leone
20 November 2018, 10:35