Vatican News
Monsinyo Christophe Zakhia El-Kassis ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pakistan. Monsinyo Christophe Zakhia El-Kassis ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pakistan.  (Vatican Media)

Mons. Christophe Zakhia El-Kassis ateuliwa kuwa Balozi nchini Pakistan

Askofu mkuu mteule Christopher Zakhia El Kassis alizaliwa tarehe 24 Agosti 1968 huko Beirut, nchini Lebanon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 21 Mei 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuwa ni sehemu ya Kanisa la Wamoriniti wa Beirut.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Christopher Zakhia El Kassis kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pakistan pamoja na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Christopher Zakhia El Kassis alizaliwa tarehe 24 Agosti 1968 huko Beirut, nchini Lebanon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 21 Mei 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuwa ni sehemu ya Kanisa la Wamoriniti wa Beirut. Alijiendeleza na hatimaye, kufaulu kutunukiwa shahada ya uzamivu katika Sheria na Taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani!

Wakati wa maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo, tarehe 19 Juni, akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa. Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza dhamana na utume wake kwenye Balozi za Vatican nchini Indonesia, Sudan, Uturuki na baadaye katika kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Ni bingwa aliyebobea katika lugha ya: Kiarabu, Kifaransa, Kiitalia, kiindonesia, Kihispania na Kijerumani, matendo makuu ya Mungu, zawadi ya Roho Mtakatifu kwa waja wake!

24 November 2018, 15:34