Tafuta

Askofu Mkuu Paul  Gallagher akiadhimisha Misa wakati wa ziara yake nchini  Georgia Askofu Mkuu Paul Gallagher akiadhimisha Misa wakati wa ziara yake nchini Georgia 

Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Georgia

Katika Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher, kuanzia tarehe 21-24 Oktoba nchini Giorgia kwa mwaliko wa wakuu wa nchi kufuatia na maadhimishi ya miaka 100 tangu kupata uhuru wake. Ameweza kukutana na Rais wa nchini, Waziri Mkuu, wa Mambo ya nchi za Nje, viongozi wa kidipolomasia,na kutembelea vyuo vikuu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican amefanya ziara yake rasmi katika nchi ya Giorgia kuazia tarehe 21 hadi 24 Oktoba kufuatia mwaliko wa viongozi wakuu wa nchi katika kuadhimisha miaka 100 tangu kutangazwa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Georgia. Katika ziara yake hiyo Askofu Mkuu Gallagher amesindikizwa na Balozi wa Vatican nchini Giorgia, Askofu Mkuu José Avelino Bettencourt. Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Vatican, Tymon Tytus Chmielecki na Mihăiţă Blaj, katibu wa balozi. Wakati wa mikutano na viongozi wa kisiasa na kidini katika nchi na wawakilishi wa Vatican, walikuwa pia na Balozi wa Giorgia aliyeko Vatican, Bi Tamara Grdzelidze.

Askofu Mkuu Gallagher alifika katika uwanja wa ndege wa Tbilis mchana tarehe 21 Oktoba na siku iliyofuta, alipokelewa na Waziri wa Mambo ya nchi za Nje  Bwana David Zalkaliani. Wakati wa mazungumzo yao marefu ambayo yaliendelea hadi wakati wa chakula cha jioni kilichotolewa na waziri kwa heshima yake, wameonesha ufanisi wa mahusiano mema yaliyopo kati ya Vatican na nchi ya Jamhuri ya watu wa Giorgia, ambayo yanasimikwa mzizi wake tangu kuanza kwao na kuimarisha nguvu wakati wa ziara ya kitume nchini humo na Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka wa 90 na Papa Francisko kunako 2016, hata kunzisha kwa shughuli za kiutamaduni zinazo waunganisha kwa pamoja. Kadhalika, hawakukosa kuonesha kuwa, nchi ya Gorgia ni  nchi yenye utamaduni wa kizamani wa kiristo ambao umetanda mzizi wake katika bara la Ulaya ya kusini Mashariki,na kuwa  na nafasi maalumu ya kujikita katika kuhamasisha thamani na kutoa kwa namna ya pekee mchango maalum wa utamaduni, tasaufi katika bara na katika taasisi zake.

Aidha Askofu Mkuu Gallagher aliwaweza kutembelea Chuo Kikuu katoliki cha Sulkhan-Saba Orbeliani kwa ajili ya mkutano mfupi na jumuiya ya Chuo. Na mchana aliwezakuweka shada ya maua katika makumbusho ya mashujaa wa nchi, na mara baada alikwenda kutembelea Ikulu na kukutana  na Waziri Mkuu Mamuka Bakhtadze. Katika mazungumzo yao, kiongozi wa nchi alionesha changamoto zinazokabiliwa na nchi, kwa namna ya pekee juu ya mtazamo wa matokeo ya migogoro iliyokumba kanda mbili, hivyo akishukuru Vatican kwa ajili ya msaada wa kibinadamu. Katika kubadilisha hali halisi ya kihusiana na kanda na kimataifa, wamesisitiza juu ya shauku ya nchi katika kudumisha kwa dhati mahusiano na Umoja wa nchi za Ulaya.

Tarehe 23 Oktoba Askofu Mkuu Gallgaer, alikutana  na Rais wa Bunge la Giorgia, Irakli Kobakhidze. Wakati wa mazungumzo pamoja pia wameonesha nafasi msingi ya thamani za kikristo kwa ajili  ya kudumisha jamii ya nchi ya Giorgia pia wamezungumzia juu ya ushirikiano wa bunge na chi nyingine ikiwa pia  ulazima wa mazungumzo ya pamoja kwa ajili ya kuishi kwa amani katika kanda. Baada ya kutoka katika Jumba la Bunge, Askofu Mkuu Gallagher alikwenda katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Ivane Javakhishvili huko Tbilisi, ambacho ni Chuo Kikuu cha Kwanza cha Taifa cha Caucaso, kilichoanzishwa miaka 100 iliyopita, ili kukutana na Jumuiya ya  wanachuo, viongozi wa kidiplomasia nchini Giorgia na wawakilishi wa madhehebu mengine ya kidini.

Katika ukumbi wa jumba la maonesho la Chuo Kikuu, Askofu Mkuu Gallagher alitoa hotuba yake juu ya Diplomasia ya Vatican na kuhusu jitihada zake kwa ajili ya amani, hadhi ya kibinadamu, kwa namna ya pekee, umakini wa kanda ya Caucaso. Baada ya hotuba yake, aliweza kujibu baadhi ya maswali kutoka kwa wanafunzi, na kushiriki chakula kilichoandaliwa na Ubalozi wa Vatican nchini humo. Baada ya mlo wawakilishi wa Vatican walipokelewa na Patriaki Elia II Catholicos, wa upatriaki mzima wa nchi ya Giorgia, akiwa amesindikizwa na baadhi ya viongozi wakuu wa wajumbe wa Sinodi ya Kanisa la Kiordhodox nchini Giorgia, na mapadre wa upatriaki huo. Mkutano huo ulidumu karibu saa moja na kuhitimishwa kwa kusikiliza wimbo wa Salam Maria uliotungwa katika lugha ya kilatino na Patriaki mwenyewe.

Wakati wa mazungumzo yao, Askofu Mkuu Gallagher alifikisha salam za kidugu kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko na zaidi ameonesha ulazima wa kuongea juhudi katika shughuli zote za Makanisa katika kueneza imani katika dunia ambayo kwa sasa inateseka kwa namna ya pekee dhidi ya migogoro na katika hali mbaya ya hatari ya kuweza kupata amani. Kwa mujibu wa Patriaki Elia II, ameweza kuweka bayana juu kupendezwa na  maneno ya Papa Francisko na kwamba yeye anashukuru sana ili waendelee katika mchakato wa mahusiano hayo ya kudumu. Haya hivyo amesisitizia juu ya kuendelea kutetea thamani za kikristo kati ya jamii ambayo iko hatarini kurudia nyumba katika nyakati zilizopita zenye kuwa na giza nene. Na baadaye walibadilishana tafakari juu ya mantiki ya hali halisi ya kisiasa na kijamii nchini Georgia ikiwa pia na mada nyingine zinazohusu sasa.

Siku hiyo mchana Askofu Mkuu alikwenda Ikulu  ili kukutana na Mkuu wa nchi hiyo Bwan Rais Giorgi Margvelashvili, ambapo Rais aliweza kutoa shukrani kubwa kwa ziara ya Papa Francisko ambayo kwa kina imeweza kukaribiana sana kati ya nchi ya Georgia na Vatican; na kushukuru kwa yote ambayo Kanisa Katoliki linafanya katika ngazi ya kibinadamu, na elimu ili kusaidia raia wa Georgia. Pamoja na mengine mengi waliyozungumza na Rais ni juu ya kuonesha ushirikiano wa pamoja kwa ngazi ya kiutamaduni.

Jioni ya tarehe 23 Oktoba, Askofu Mkuu Gallagher alikwenda kukutana na Jumuiya katoliki iliyoko katika nchi ya Giorgia kati ya aina tatu za kiliturujia ambazo ni  ( Kilatino, kiarmeni na Kikaldayo). Aliadhimisha Misa katika Kanisa la Bikira Maria mpalizwa mbinguni mjini Tbilisi kwa ushiriki wa waamini wengi. Walioshiriki naye katika  misa pia  ni Msimamamzi wa kitume wa Caucaso kwa upande wa kilatino, Raphael François Minassian, Msimamizi kwa ajili ya Wakatoliki wa Kiarmeni wa Ulaya Mashariki Padre Benny Beth Yadegar na parko wa jumuiya liturujia ya wakaldayo na idadi kubwa ya mapadre. Mara baada ya misa walikaa kwa pamoja kushirikishana uzoefu wao katika makao ya Monsinyo Pasotto na kesho yake 24 Oktoba, Askofu Mkuu Gallagher  alirudi mjini Vatican.

30 October 2018, 10:04