Tafuta

Kitabu kipya  cha Papa Francisko "Ni mimi , usiogope" Kitabu kipya cha Papa Francisko "Ni mimi , usiogope" 

Vatican imeamua kuendelea katika Maonyesho ya Vitabu Frankfurt

Baraza la Mawasiliano Vatican linataka kuunga mkono huchapishaji Katoliki kimataifa na kuthibitisha juu ya uteuzi wa matukio wawili huko Roma kunako mwaka 2019 uliotangazwa mwaka jana. Katikati ya mkakati huo ni Duka la Vitabu Vatican, ambalo katika mji wa Frankfurt limekusanya ufanisi wa washiriki wengi kwa kazi ya kuandika mfululizo wa hotuba za Papa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni mzani chanya katika ishara ya kuendelea kwa Vatican katika Maonesho ya Vitabu mjini Frankfurt unaofunga milango yake tarehe 14 Oktoba 2018. “Uteuzi  wa kufanya matukio mawili, amesema Padre Giulio Cesareo, mhariri wa Maktaba ya Uchapishaji wa Vitabu Vatican  kwamba, umethibitishwa na ufanisi wa waandishi katoliki  kimataifa na  sio tu kuhusiana na Magisterium ya Papa Francisko, lakini pia kwa kukusanya mantiki ya hotuba zake katika mfululizo wa uchapishaji wa vitabu vingi Vatican kadhalika kuhusina na kitabu kipya: amesema, Ni kitabu kipya kiitwacho “ Ni mimi , msiogope: Maneno ya Papa Francisko juu ya wakimbizi na wahamiaji,

 Nembo mpya

Hata hivyo kutokana na mambo mapya, kwa mara ya kwanza kwa ngazi ya kimataifa, Duka la Vitabu Vatican , limewakilisha nembo mpya. Ni tunda la mageuzi ya vyombo vya habari Vatican na nembo mpya  hiyo, ina rangi ya  njano ikiwa inafuata falsafa ya nembo ya Vatican News , Vatican Media na Radio Vaticana Italia. Aliyepeleka habari mpya huko Frankfurt ni Kamishna wa Baraza la Mawasiliano, Monsinyo Dario Edoardo Viganò, ambaye alitangaza mipango miwili itakayofanyika mjini Roma mwaka 2019 ambayo inayozungukia  juu la Duka la vitabu Vatican .

Mtazamo huu ya uhariri katoliki

Mpango wote huo ameeleza Monsinyo Vigano kuwa, ni lengo la kuunga mkono ulimwengu wa huchapishaji vitabu Katoliki na kuimarisha uwezo wake”. Hata hivyo mikutano hiyo haitakuwa na sifa kama ile ya maonesho ya kimataifa, bali watakuwa na mikutano  ya kawaida ambayo itaundwa kwa njia ya kukuza hasa  kukabiliana na kushirikiana uzoefu tofauti. Hatua ya kwanza iliyopoendekezwa inaelekezwa kwa sekta ya Italia, itakayo fanyika mwezi Januari 2019.  Na ya pili, ambayo ni ya kimataifa, labda katika nusu ya pili ya mwezi Juni 2019. Taratibu hizo tayari zimekwisha kukubaliwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, Bwana Paulo Ruffini kwa mujibu wa kamishna wa mawasiliano Monsinyo Vigano.

 

13 October 2018, 15:49