Tafuta

Ajali ya Treni nchini TAIWAN Ajali ya Treni nchini TAIWAN  

Telegram ya Papa kwa waathirika wa ajali ya treni Taiwan

Baba Mtakatifu Francisko anasikitika sana kwa taarifa ya ajali ya treni iliyotokea mji wa Yilan nchini Taiwan na kusababisha vifo vya watu na majeruhi wengi. Anawaombea marehemu wote pia kuwatakia uponywaji wa kiroho na kimwili majeruhi wote na wote ambao wanaomboleza kwa ajili ya wapendwa wao

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kufutia na vyombo mahalia nchini Taiwani vinasema kuwa takriban watu 18 wapoteza maisha kwenye ajali ya Treni Taiwan. Kwa njia hiyo, anatuma salam za rambirambi kwa njia ya Telegram iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwamba: Baba Mtakatifu anasikitika sana kutokana na ajali ya treni iliyotokea mji wa Yilan nchini Taiwan, anawahakikishia mshikamano wake kwa wote ambao wameathirika katika janga hili.

Baba Mtakatifu Francisko anawakumbuka katika sala zake kwa Mungu kwa watu wote waliopoteza maisha yao na wote waliojeruhiwa na wengine  wanao omboleza kwa kupoteza wapendwa wao. Anawatumia Baraka ya Mungu ili wapone haraka majeruhi wote, ikiwa ni pamoja na viongozi wote serikali na wale ambao wanatoa huduma hiyo ya uokoaji.

Taarifa mahali zainasema kuwa takriban watu 18 wamepoteza maisha na 170 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria kutoka nje ya njia yake Kaskazini mashariki mwa Taiwan. Mamlaka ya reli imesema inafanyia uchunguzi ajali hiyo, iliyotokea katika mji wa Yilan siku ya Jumapili 21 Okotba 2018. Watu 366 walikuwa kwenye treni hiyo wakisafiri kati ya Taipei naTaitung wakati mabehewa yote nane yalipotoka nje ya njia.

Mamlaka zinasema zimewatoa kila mtu kutoka kwenye treni hiyo. Treni iitwayo Puyuma Express 6432 iliripotiwa kupata ajali hiyo ilipokuwa ikikaribia stesheni ya Xinma, karibu na mji wa Su'ao. Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya reli ya Taiwan, Lu Chieh-shen, ameviambia vyombo vya habari kuwa treni hiyo ilikuwa na miaka sita na ilikuwa na hali nzuri kabla ya ajali kutokea. Haijajulikana mara moja sababu ya treni kutoka nje ya reli yake, lakini mashahidi walisema walisikia kelele kubwa, cheche na moshi.

Vikosi vya zima moto wanasaidia majeruhi na wizara ya ulinzi imesema inapeleka wanajeshi 120 kusaidia jitihada za uokoaji. Mashuhuda walilazimika kuvuja vioo ili kutoka nje ya mabehewa, na baadhi ya waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini. Kiongozi wa Taiwan,Tsai Ing-wen, amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ni tukio baya sana.Taiwan ina mtandao mkubwa sana wa usafirishaji wa treni, na zaidi ya nusu milioni ya abiria husafiri kwa treni kila siku.

 

 

23 October 2018, 15:37