Tafuta

Vatican News
 Picha ya Papa Paulo VI itaoneshwa kuanzia tarehe 4 Oktoba katika majukwaa yote ya kidigital Picha ya Papa Paulo VI itaoneshwa kuanzia tarehe 4 Oktoba katika majukwaa yote ya kidigital  (@L'Osservatore Romano)

Vatican: Paulo VI ni mtu, ni Papa na Mtakatifu!

Picha kuhusu Papa Paulo VI itaoneshwa kuanzia tarehe 4 Oktoba 2018. Ni toleo la ubunifu ambao unaunganisha mahojiano, picha, maandiko, video na sauti iliyosainiwa na vyombo vya habari Vatican na Ofisi ndogo ya Mawasiliano ya Jimbo Kuu la Milano na Jimbo la Brescia nchini Italia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Paulo VI anazungumzwa na Picha moja iliyotengenezwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican. Ni mchakato wa simulizi ya historia yake, ambayo itaanza tarehe 4 Oktoba katika miundo ya majukwaa yote ya kidigital ya Vatican News na ambayo itawezesha kuona historia, ishara, mawazo ya Papa Montini ambaye anatangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 14 Okotoba na wengine wakati Sinodi ya maaskofu ya kuhusu vijana, imani na mang’amuzi ya miito inaendelea.

Mababa wote washiriki wa Sinodi na wasikilizaji watakuwa mstari wambele katika maadhimisho hayo Siku ya Jumapili 14 Okotba 2018 katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Ni toleo la ubunifu ambao unaunganisha mahojiano, picha, maandiko, video na sauti iliyosainiwa na vyombo vya habari Vatican na Ofisi ndogo ya Mawasiliano ya Jimbo Kuu la Milano na Jimbo la Brescia nchini Italia.

Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, limewasilisha utangulizi picha hiyo Jumatatu 1 Oktoba 2018 na iliyopewa  jina: “ Paulo VI ni  Mtu, ni Papa na Mtakatifu”. Ni mfululizo wa vipindi 12 vinavyozingatia masuala maalum ya maisha na Papa Montini, ambavyo vitakuwa hata katika mtandao wa moja kwa moja (online) kila siku kwenye Habari za Vatican na kwenye majukwaa ya kijamii ya  kuanzia tarehe  4 Oktoba 2018.

02 October 2018, 18:11