Cerca

Vatican News
Sinodi ya Maaskofu inaendele mjini Vatican Sinodi ya Maaskofu inaendele mjini Vatican 

Sinodi:Kanisa liwe nyumba ya vijana!

Tarehe 4 Oktoba shughuli ya Mkutano wa XV wa Sinodi ya Maaskofu, juu ya Vijana, imani na Mang’amuzi ya miito umeendelea kwa kujikita katika mada ya usikivu, hasa kusikiliza kitendea kazi. Mama na nyumba kwa maana ya Kanisa ni mwema na anasikiliza sauti ya yule hasiye kuwa na sauti

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wakati sehemu ya kwanza imejikita katika kitendea kazi, yaani Instrumentum Laboris ambapo  sehemu hiyo ya kwanza mada yake  ni kusikiliza. Hotuba 20 zilitolewa katika ukumbi na kufuatia mjadali huru. Vijana wasiwe ni kitu bali watu wa kutangaza Injili. Ndiyo umekuwa ni matashi mema yaliyotolewa katika ukumbi kwa siku ya tarehe 4 Oktoba alasiri. Wazo ni lile la kupyaisha walio mstari wa mbele katika umisionari wa Kanisa, kijamii na kisiasa,  kwa sababu kizazi kipya kiwe ndiyo chachu na mwanga wa dunia, mafundi wa amani na ustaarabu wa upendo.

Kanisa, nyumba na Mama wa vijana

Mama na nyumba ni mwema na anasikiliza sauti ya yule hasiye kuwa na sauti. Kanisa linaalikwa kuwa hivyo, hasa kwa wale ambao wanatoka katika hali ngumu, jiwe lililo kataliwa na ambalo kwa neema ya Habari Njema wanaweza kuwa jiwe msingi la pembeni ,“ katika ujenzi wa dunia iliyo bora. Huo ni ujumbe uliowaendea watoto wote waliokolewa chini ya mzigo mzito wa kuwa maaskali wakiwa watoto, na kwa wote ambao wanatoka katika familia zilizogawanyika au kukumbwa na madawa ya kulevya, wasio kuwa na ajira, rushwa, utumwa ; lakini pia hata wahamiaji wengi , kama vile ambao mara baada ya masomo yao ya  juu, wanaacha nchi yao  ya asili ili kutafuta maisha bora, na kuishia kupoteza mizizi, kuacha imani yake na hasiweze kuzalisha tunda la talanta yake aliyo pewa.

Kuokoa shauku ya vijana

Kadhalika katika kutzama jinsi ya kutumia  hovyo kwa nchi ya Mashariki, Mababa wa Sinodi wameonesha juu ya hatari ya kuzima kwa shauku ya vijana. Hawa daima mara nyingi wanaonekana kutokuwa na mwelekeo, bila kuwa na ndoto, bila imani hata kutokana na asababu za itikadi mpya kama ile ya gender ( jinsia au huria wenye mahangaiko. Kwa maana hiyo wanasisitiza kuwa, “ kuna haja ya kuzungumza kwa ujasiri uzuri wa pendekezo la kikristo juu ya ngono, bila kufunika: Kuwa makini kwa wengi ambao hawawezi kuishi useja wakati wa kipindi cha uchumba”.

Baadhi ya mbaba wanakubali kuwa, sehemu nyingi za  jumuiya za kiparokia hawajitoshelezi kwa matarajio ya vijana ambao mara nyingi,  mara baada ya kipaimara wanakwenda mbali na Kanisa. Kwa sababu hiyo, ni dharura ya kupyaisha huduma ya kichungaji yenye uwezo wa kusikiliza na kuwa na mtazamo wa upendo wa Kristo , lakini pia kuzungumza lugha ya vijana, kuanzia na ile ya digital.

Vijana wanapata imani katika Kanisa

Maaskofu pia wanaona kuwa Vijana wanawasaidia watu wazima kuwa makini katika wakati uliopo na wanasubiri Kanisa ambalo ni ishara ya kinabii ya muungano katika dunia iliyo chanika vipande. Wao ni moyo wa kimisionari wa Kanisa. Kutokana na hiyo, ndiyo kuna pendekezo la kuunda Baraza la Kipapa la ushauri kuhusu wao. Pamoja na hayo washiriki wa mkutano wameka katika mwanga maombi ya upyaisho wa kitasaufi ambao umejitokeza hawali  katika maswali ya maandalizi ya Sinodi. Inahitaji kuwasaidia watu wazima endelevu ili kupata imani kutoka kwa makuhani hasa katika kipindi ambacho uaminifu huo umekumbwa na majaribu ya kashfa ya manyanyaso. Na ndiyo matashi mema ya Sinodi kuwa, wanaweza kutoa mtazamo wa mapendekezo ya dhati ya kichungaji.

Kufufua liturujia na sala katika nyayo za watakatifu

Hata hivyo mababa pia wamesisitiza juu ya kufufua kwa upya katekesi na liturujia ambayo kwa pamoja inajumuishwa na ibada za watu  ambapo wamesisitza kutakana na muktadha hasa wa kuteswa kwa wakristo wengi. Na ili itawezekana iwao haitajikita kuangukia katika vishawishi wa haraka  na hivyo ni muhimu kusisitiza na kuwaonyesha vijana umuhimu wa sala, lakini pia ni muhimu Kanisa liwaombee vijana na wito wao.

Mara nyingi kwa dhati mwelekeo wa ukuu  wa kimya na kutafakari hupotea hasa wakati unapotafutwa katika Kanisa husipatikane, wao hutafuta mahali pengine. Kwa mujibu wa Sinodi ni lazima kuwepo na usindikizwaji kitasaufi na ambao unaonesha thamani za ndani ambazo zinaleta furaha ya kweli katika pendekezo la Kiinjili  na ambalo linaheshimu muda wa ukomavu wa kila mmoja. Katika suala hilo, maaskofu,  wameonesha watakatifu wengi ambao leo hii wanabaki nautajiri wa historia na kuwa  mifano halisi ya sasa.

 

 

 

05 October 2018, 11:44