Tafuta

Vatican News
Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu juu ya Vijana tarehe 3 Oktoba 2018 Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu juu ya Vijana tarehe 3 Oktoba 2018  (Vatican Media )

Sinodi ni fursa ya kufungua mazungumzo kati ya Kanisa na vijana!

Katibu Msaidizi wa Sinodi, Askofu Fabio Fabene anasema kuwa ufunguzi wa Sinodi unaofunguliwa leo utaruhusu Kanisa kugundua upendo wake mkuu katika mafundisho.Pia ni kutoa fursa mpya ya kufungua mazungumzo kati ya Kanisa na vijana

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Zitakuwa ni siku za shughuli  ya kina, kukabiliana na mazungumzo ili Kanisa liweze kupata kwa mara nyingine tena upendo wake mkuu wa kutangaza Injili kwa vijana , lakini pia hata upendo mkuu katika kuelimisha na kuonesha katika vijana, uzuri wa maisha. Na hiyo ni kwa namna ya kwamba vijana katika hali yao yoyote wanayojikuta nayo wanaweza kwa mara nyingine tena kuishi na kupata ukamilifu wa maisha na upendo. Huo ndio uthibitisho wa Askofu Fabio Fabene, Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu alioutoa katika vyombo vya habari Radio Vatican, Italia wakati ambapo ni siku ya ufunguzi wa Sinodi ya maaskofu kwa ajili ya vijana tarehe 3 Oktoba 2018.

Vijana wako wazi katika tasaufi

Askofu anathibitisha kuwa, hiki ni kipindi ambacho kinajionesha tayari kuwa changamoto kwa Kanisa, kwa sababu, mada inayokabiliwa na kanisa ni vijana. Mada ambayo ilipendekezwa na Papa Fransisko kwa muda mrefu na mpana wa majadiliano, na ambayo yatazama vijana wote duniani, na hakuna anayebaguliwa. Kanisa linataka kutazama vijana wote wa mabara yote, hali zozote ambazo wao wanaishi ikiwa ni katika hali ya kijamii kwa vijana wa leo hii.

Ni chamaoto kwa sababu sisi wote tunaalikwa kutembea pamoja; tumealikwa kugundua mahitaji yao ni nini, sababu na hasa tunapaswa kukabiliana na hali halisi wanayoishi, na ili kutafuta na kupata njia ya kuweza kuwatangazia vijana wa leo Injili. Wakati wa kutathmini shughuli nzima ya maandalizi, wanaonekana kuwa ni vijana ambao wako wazi katika tasaufi na wako tayari kupokea Injili na zaidi ili waweze kupata maana ya maisha.

Umuhimu wa Sinodi

Sonodi inayoanza leo hii, ilitanguliwa na maandalizi marefu tangu Januari 2017, kwa maswali  kupitia njia za mtandao wa moja kwa moja ( ??Online, semina  na hata Sinodi ndogo ambayo iliwaunganisha vijana 300 kutoka duniani kote.  Askofu Fabene amethibitisha kuwa, ilikuwa  ni kipindi cha dhati, na  muhimu kwani kwa mtindo huo watu wa Mungu waliweza kuingia kwa hakika katika Muungano wa Sinodi ya maaskofu na wote waliweza kutoa mchango ambao uliwakilishwa na kitendea kazi kiitwacho  “Instrumentum Laboris” ambacho kilikusanya matokeo yote yaliyotokana na maandalizi ya mwanzo.

Sinodi ya kanisa la Kisinodi

Tarehe 17 Septemba, ulitangazwa waraka wa Episcopalis communio wa  Papa Fransisko na hii ni Sinodi ya kwanza kujikita katika matendo ya dhati kwa Waraka huo.  Mapya muhimu zaidi na msingi wa Sinodi ni kuhusiana na Katiba hiyo ya Kitume ambayo inawekwa moja kwa moja katika Sinodi ya Maaskofu na ambayo  inabaki jinsi ilivyo katika Muungano wa Kanisa. Kwa maana hiyo, inapitia katika mchakato huo wa hija ya Sinodi. Hiyo inajikita katika hatua ya kwanza ya maandalizi; maadhimisho ya Misa; sinodi yenyewe na mwisho matendo ya dhati ambayo yatasaidia Mabaraza ya Maaskofu, maaskofu wenyewe kutimiza kwa dhati maelekezo ambayo Papa Fransisko atatoa mara baada ya hitimisho la Sinodi hii.

Kati ya wanaohudhuria sinodini ni vijana 34

Kati ya wasikilizaji 49 kwenye Sinodi, wapo vijana 34. Na vijana 34  ni wanawake na wanaume. Uwepo wao, Askofu Fabene anathibitisha, ni muhimu kwani wanaweza kusikiliza  hotuba mbalimbali za maaskofu, lakini pia hata wao kuzungumza, iwe kwa mabaraza makuu hata katika mzunguko mdogo.  Na uwepo wao ni wa kuvutia sana na utakuwa kihamasisho kikubwa kwa kazi yote ya Sinodi.

03 October 2018, 12:51