Cerca

Vatican News
Maandalizi ya Sinodi ya juu ya vijana kuiva Maandalizi ya Sinodi ya juu ya vijana kuiva 

#Synod2018:Bard.Baldisseri:Mada ya vijana ni changamoto ya Kanisa!

Imekilishwa katika Vyombo vya habari Mkutano XV wa Sinodi ya Maaskofu yenye kuongozwa na mada: vijana, imani na mang’amuzi ya miito. Kati ya waliokuwapo ni Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu,Kardinali Sergio da Rocca Msemaji Mkuu wa Sinodi ya Maakofu na Askofu Fabio Fabene, Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

 “Kanisa liko tayari kujiweka katika kusikiliza sauti, hisia, imani na hata wasiwasi na hoja ya vijana, wanaowakilisha changamoto moja kwa ajili ya wakati endelevu”. Ndiyo maneno ya utangulizi wa Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, wakati wa kuwakilisha katika vyombo vya habari juu ya Sinodi ya XV ya Maaskofu inayoanza tarehe 3 -28 Oktoba 2018, ikiongozwa na mada ya: Vijana, imani na Mang’amuzi ya miito.

Kwa mujibu wa Kardinali amethibitisha kuwa, wataudhuria mababa wa Sinodi 267, na kati yao wasikilizaji 34 vijana, wenye umri kuanzia 18-29. Ni vijana ambao watatoa mchango wao ili waweze kuwakilisha sauti ya wenzao duniani kote. Hata hivyo zaidi   na kwa mara ya kwanza, baada ya mkataba wa muda kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa China, watakuwapo kwenye Ukumbi wa Sinodi mjini Vatican hata maaskofu wawili wa China  amethibitisha.

Ni mtazamo wa Kanisa mchumba wa Kristo zaidi ya kashfa.

Sinodi ya maaskofu itaruhusu kuweka moto juu ya utume wa Kanisa na kuwasindikiza katika hija yao ya maisha katika ufunguzi wa kukutana na Mungu, amethibitisha na wakati huohuo, Kardinali  Baldisseri ameweka bayana kila swali ambalo limetokana na waandishi wa habari,  kwamba sinodi hiyo itaruhusu vijana kutazama Mchumba  ambaye ni Kristo zaidi ya kashfa ambazo zimekumba mchumba huyo.

“Vijana wako wazi kutambua udhaifu wa kibinadamu na Kanisa haliwezi kuwakilishwa tu na wale ambao wamekosea, bali watu wambao wanajikitia katika mchakato wa kutembe katika njia ya wokovu na upatanishao”. Zaidi ameelezea juu ya mfumo wa kazi ulivyoandaliwa ya kwamba Sinodi ambayo imetengwa katika sehemu tatu, kwa mujibu wa mhutasari wa kazi, ikiwa ni, “kutambua, Kanisa katika kusikiliza hali halisi; Kutafsiri, imani na mang’amuzi ya miito; kuchagua, safari zipi za uongofu wa kitume na kimisionari”.

Hati ya kazi kama kitovu cha kuanzia

Akiwakilishwa kwa ujumla itakavyokuwa Sinodi, naye Kardinali Sergio da Rocha, Msemaji mkuu wa Sinodi ya Maaskofu amesisitizia juu ya “nafasi ya Kitendea Kazi  yaani Instrumentum laboris, kama kielelezo cha kufuata wakati ya  shughuli nzima ya Sinodi ya maaskofu. Kwa dhati, Hati hiyo, inawakilisha mfumo wa kumbukumbu ya mahusiano yote ya awali ya maelfu ya kurasa za ushuhuda, tafakari na maombi kutoka duniani kote ya vojana, lakini pia siyo kusema ni orodha iliyo tayari na majibu  kwa ajili ya kuwasindikiza  vijana, imani na mang’amuzi ya miito, hata  kama  pia  kupata “suluhisho la awali la maswali mengi ambayo yalisikilizwa na Sinodi zilizotangulia na maswali yaliyojitokeza.

Sinodi Mpya

Na mwishokatika vyombo vya habari wamewakikilisha hatamaelekezo ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu na shughuli za Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu.  Kwa sasa katika Ibara ya 26 ya Katiba ya Kitume ya Papa Francisko ya Episcopalis Communio iliyotolewa tarehe 15 Septemba 2018. Katiba ya Kitume   mpya anachukua nafasi “ile ya hawali ya Motu Propprio Sollicitudo ya Mwenyeheri Papa Paulo VI.

Kutokana na hiyo, Kardinali Fabio Fabene, Katibu Mkuu msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu amesema, hayo ni maelekezo mapya yanaongia katika mpangilio wa Sinodi ya Maaskofu (Ordo Synodi Episcoporum), ambayo kwa karibia ya miaka 50 imeona toleo tofauti, hadi ile ya mwisho iliyokuwa imetolewa na Papa Mstaafu Benedikto XVI kunako mwaka 2006.  Amehitimisha kwa kusema: na hivyo kazi zote na taratibu zote zinazotajwa ili kuwezesha kila iwezekanavyo mjadala zaidi na na maoni kati ya Mababa wa Sinodi, na ili kuleta utajiri wa sauti za Makanisa yaliyoenea duniani kote.

02 October 2018, 10:01