Kardinali Sako na Kardinali Baldisseri wamemshukuru sana Papa Francisko wakati wa kuhitimisha Sinodi ya Maaskofu Kardinali Sako na Kardinali Baldisseri wamemshukuru sana Papa Francisko wakati wa kuhitimisha Sinodi ya Maaskofu 

Kardinali Sako:msisahau wakristo wa Mashariki!

Kardinali Louis Raphael Sako, Rais wa Sinodi ya Maaskofu ya Vijana na Kardinali Baladisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi walimshukuru Baba Mtakatifu wakati wa kufunga Sinodi kwa namna ya pekee Kardinali Sako amekumbusha kuwa "milioni ya waamini wa chi za mashariki wanasali kila siku kwa ajili ya Papa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa kufunga Sinodi ya Maaskofu tarehe 27 Oktoba 2018, zilitolewa hotuba kidogo japokuwa zilikuwa fupi na bila kusomwa kwa maana hiyo, kabla ya Papa Francisko kuzungumza waliotangulia kwanza ni Kardinali Louis Raphael Sako, Rais mwakilishi wa Sinodi ya Maaskofu ya Vijana na Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu.Katika hotuba hizo walitoa shukrani kubwa kwa ajili ya Sinodi hiyo na Kardinali Sako akikumbusha kuwa, milioni ya waamini wanasali kila siku kwa ajili ya Papa na kutoa methali moja kwa lugha kiarabu isemayo  kwamba:“ mti mwema mara nyingi ugongwa na mawe” kwa maana hiyo alimwomba Papa aendelee mbele kwa ujasiri na matumaini. Akisisitiza Kardinali Sako amesema, “Mtumbwi wa Petro licha ya mawimbi makali, bado unabaki imara kwa sababu Yesu hatauacha kamwe! Kutokana na hili, ametoa wito wa kuweza kujenga jamii zaidi ya kidugu na wasisahau wakristo wa Mashariki kwani anathibitisha, “iwapo nchi za mashariki zitabaki bila wakristo, ukristo utabaki bila mizizi. Kwa namna hiyo anakazia kusema, " kuna haja ya msaada kuwa na ukaribu hadi dhoruba kali itakapopita, amethibitisha!

Kardinali Baldisseri:vijana wamonesha sura ya mwanga wa Kanisa

Katika hotuba yake ya mwisho Kardinali Lorenzo Baldisseri, Karibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, naye amemshukuru sana Papa kwa ukaribu wake, vijana ambao katika uwepo wake na shauku yao kwa siku hizi wameweza kuonesha kweli uso mwanga na umoja wa kweli wa Kanisa uliopo katika mabara yote. Hata hivyo shukrani hizo ziliambata na makofi yasiyo na mwisho, hata kwa  Mababa wa Sinodi, Marais wanne wawakilishi, watoa mada kuu na Makatibu wakuu wawili maalum, Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi, wasikilizaji na wawakilishi wote kindugu, wataalam na wote ambao wameweza kushiriki katika kufanikisha Mkutano huo!

Kardinali  Coutts wa Pakistan anasema amejifunza mengi na sasa ni kwenda kuzungumza na vijana

Na mahojiano ya Kardinali Joseph Coutts, Askofu Mkuu nchini Pakistan baada ya kuhitimisha Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana mjini Vatican , anasema kwamba amejifunza mengi na sasa wanapaswa kupeleka kwa dhati ujumbe uliotolewa katika chi zao. Kardinali Joseph Coutts, ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Karachi, aliyechaguliwa kuwa Kardinali na Papa Francisko mwezi Juni mwaka huu na ambaye anaitwa na waamini wake kuwa, Askofu Mkuu wa ndevu nyeupe. Ni Baba mwenye umri wa miaka 72 ambaye hachoki kuhamasisha mazungumzo ya kidini lakini pia ni makini katika masuala msingi ya haki za binadamu kama pia ilivyo juu ya manyanyaso ya kukufuru.

Kueneza ujumbe wa mwisho wa  Sinodi sasa

Akizungumzia juu sinodi hasa kuhusu suala la jinsi gani ya kuweza kujibu maswali ya vijana wa Pakistan na changamoto ya kuwasindikiza na kuwasikiliza, amesema kuwamba maaskofu wote, kwa namna ya pekee yeye binafsi, wamejifunza mengi kutoka Sinodi na hivyo ni lazima warudi makwao, mahali walipotokea duniani ili kutoa, wazungumze wazi matatizo kwa namna ya kawaida. Ni wajibu wao kama maaskofu kujikita kwa dhati katika ujumbe huo na kuueneza ipasavyo. Lakini kwa jinsi gani ya kuzungumza na vijana, ni shughuli ambayo bado wanapaswa kuitimiza, amesema.

Wazo la mafundisho kwa walei na makuhani

Askofu Mkuu akijibu swali juu ya wazo jinsi gani ya kufanya mafundisho ya walei na makuhani, amesema wao tayari wamekwisha fanya mambo mengi, ambayo wametoa nafasi kwa vijana, lakini jinsi gani ya  kuwasindikiza kwa dhati, katika nchi yake anadai ni nchi maskini na hawana  wakristo walei na mapadre walio tayari au kufundwa vema kwa ajili ya kuwasindikiza vijana. Ameongeza kusema, kwa sasa, wanatakiwa kutafakari ni jnsi gani:  Kwanza ni jinsi gani ya kupeleka ujumbe huo kwa Baraza la Maaskofu na baadaye kupanda ujumeb huo wa Sinodi kwa wote katika nchi yao.

Vijana katika Sinodi wamekomaa na wenye hekima

Hata hivyo Kardinali Coutts  ameweza kusimulia kwa furaha kubwa kuona wale wasikilizaji vijana katika Sindo jinsi walivyokuwa wamekomaa na kuwa na hekima, mfani anasema kijana kutoka Pakistan Daniel Bashir, wa Jimbo Kuu la Karachi, na mjumbe wa Chama cha Vijana wa Yesu kimataifa alivyoshiriki kwa namna ya ukomavu na hata hekima kubwa, na ambaye amweza kushiriki hata katika mchakato wa uamuzi wa Sinodi.

31 October 2018, 10:07