Tafuta

Vatican News
06.10.2018  briefing juu ya kazi ya sinodi 06.10.2018 briefing juu ya kazi ya sinodi 

Briefing Sinodi Kard. Nzapalainga: wahamiaji wasisukumwe kama wanyama!

Muungano wa Kanisa, mkutano wa vijana na Papa Francisko na mababa wa Sinodi , tukio la wahamiaji, ndiyo baadhi ya mada za briefing ambazo zimetolewa siku ya Jumamosi 6 Oktoba 2018 mjii Vatican kwa ushiriki wa Kardinali Giuseppe Versaldi, Rais wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki na Kardinali D. Nzapalainga wa Jimbo Kuu la Bangui, Afrika ya Kati

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Umoja katika utofauti. Ndiyo unafunguliwa katika utamaduni ambao ni mada iliyojitokeza katika Sinodi. Uzoefu wa ulimwengu wa Kanisa ambao unajikusanya pamoja katika utofauti. Hayo yamethibitishwa na Kardinali Giuseppe Versaldi, Rais wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki wakati wa kushiriki katika vyombo vya habari Vatican kwa waandishi ili kujuza kwa ufupi kazi inayoendelea ya Sinodi, Jumamosi mchana tarehe 6 Oktoba 2018.

Utajiri wa utofauti: Sinodi katika wingi wa sauti, ni uzoefu wa utajiri kwa kila baba wa sinodi. Lakini hatari ya kujiweka katika kitovu, inaweza kupunguza Kanisa na kulifanya liangukie nyuma  ya mitindo ya kimashariki. Lakini wakati huo huo, Sinodi inapaswa kwa namna hiyo kuwa tofauti, na kuiwezesha kutoa pendekezo la mtindo ambayo siyo mmoja tu, bali wenye utajiri wa utofauti na ambao unazingatia hata hatari za kuwa na unafananisho.

 

Kujiweka katika usikivu: Ushuhuda kwa wale wanaoishi nje ya Ulaya amethibitisha Kardinali Vesaldi, unafanya kutambua uzoefu huo ya kuwa ni wenye utajiri. Unatambua kwamba, kubobea katika malimwengu na tukio ambalo lipo katika nchi za Mashariki, lakini siyo katika nchi ambazo wakristo wake ni wachache. Na katika ardhi hizo kwa namna ya pekee kuna uhai na uwepo wa hari ya ukatoliki, ambao unawasaidia vijana kutaka kujikwamua na kuondokana na umaskini. Na unawasaidia hata wasiwe waathirika wa kila ambacho Papa anakiita utamaduni wa ubaguzi.

Mkutano wa vijana na Papa na mababa wa Sinodi: Kardinali Versaldi pia amewakilisha juu ya mkutano wa Papa, Vijana na Mababa wa Sinodi jioni ya siku ya Jumamosi kwamba , hao wanaungana na maelfu ya wanafunzi wengi kutoka vyuo vya kipapa vyote vilivyopo mjini Roma na mkutano amao ulikuwa unajikitia katika kushuhudia, na muziki na kuburudisha safari ya Sinodi.

Wahamiaji, Kanisa lifungue milango: Kati ya mada nyingine iliyoko katika mchakato wa Sinodi, Kardinali Versaldi pia alisema, kuna suala ambalo kweli ni gumu linalohusu wahamiaji. Hii ni lazima kuchanganua kati ya nafasi ya Kanisa ambalo lina wajibu wa kutangaza Injili na nafasi ya mataifa. Katika  Kanisa tendo la kukaribisha ni thamani kubwa ambayo haliwezi kuacha milango imefungwa, wanaofunga milango siyo watu wa  Kanisa, kwa maana Kanisa limefungua milango yake hata kwa wale waliokuwa wamefungiwa milango.

Afrika isinyonywe: Kardinali Versaldi akipanua mada ya uhamiaji ameonesha kuwa Italia inayopokea wahamiaji wasishangae ya kuwa imegutuka kwa maana hata nchi za Afrika wajaribu kuwasaidia vijana na hiyo ni sehemu ya utume wa Kanisa.  Hata hivyo Kardinali ametangaza kwa waandishi wa habari kuwa, mwezi Desemba mwaka huu, maaskofu wa Afrika na Italia watakutana kwa lengo la kuhamasisha matendo ya kujikita kwa  pamoja ili kuwepo na uhuru na siyo kulazimishwa kuacha nchi asili. La sivyo Bara la Afrika litarudia katika hali ya kunyonywa.

Wahamiaji wasioneakane kama wanyama: Katika mada ya wahamiaji wakati wa briefing, ya Jumamosi 6 Oktoba, naye , Kardinali D. Nzapalainga, Askofu Mkuu wa Jimbo la Bangui, nchini Afrika ya Kati, amesema kuwa, vijana, “ wawe wanaobaki au wale wanaoondoka, wanasababu zao, lakini hawawezi kuzuiwa, utafikiri ni wanyama. Wao ni binadamu wanaotaka kutafuta namna ya kuishi. Akifafanua juu ya Sinodi hiyo  anasema ni uzoefu wa aina yake, wa neema, na sinodi hiyo,vijana mbalimbali wameweze kujieleza juu ya mada ya kueneza imani na Papa amependelea kusikiliza sauti yao. Kadhalika Kardinali Nzapalainga, amekumbusha kuwa katika chi yake ya Jamhuri ya watu wa Afrika ya kati, vijana wanapenda Kanisa na wanasubiri kwa hamu ujumbe wa Sinodi.  Ujumbe ambao unapaswa kuwalekeza njia ya kupendekeza kwa vijana.

Papa anayo imani kwa vijana: Katika Briefing pia wameundhuria hata Mariano German Garcia, msikilizaji katika Sinodi na mhudumu wa kichungaji wa vijana wa Baraza la Maaskofu nchini Argentina. Yeye anasema kuwa wapo “wanaishi kipindi cha kihistoria cha Kanisa. Kanisa kwa njia ya Sinodi inaendelea kujikita kwa vijana na iko tayari kuwatambua. “Sisi vijana ni vichupukizi vya Kanisa. Sinodi hii ni mwanzo mzuri na mti ambao unakaribia kutoa maua, hata hivyo ni shukrani kwa ajili ya Vijana.  Papa pia  anayo imani kwa vijana” amehitimisha Germàn Garcia.

 

08 October 2018, 16:11