Askofu Mkuu Anthony Muheria  wa Nyeri Kenya, ameshiriki katika briefing juu ya Sinodi ya maaskofu tarehe 26.10.2018. Ni matarajio ya Kanisa kutoa cheche za moto kwa vijana Askofu Mkuu Anthony Muheria wa Nyeri Kenya, ameshiriki katika briefing juu ya Sinodi ya maaskofu tarehe 26.10.2018. Ni matarajio ya Kanisa kutoa cheche za moto kwa vijana 

Briefing:Roho Mtakatifu ataongoza Kanisa katika upyaisho

Sinodi ni ishara kubwa, kipindi cha neema, bendi ya ajabu na Roho wa Mtakatifu kuongoza Kanisa lake, ndiyo tafsiri waliyo itoa badhi ya mababa wa Sinodi wakati wa kufanya briefing, mchana tarehe 26 Oktoba 2018. Askofu Mkuu Anthony Muheria wa Nyeri Kenya, anasema ni matarajio yao kutoka katika Sinodi hii waweze kutoa cheche za moto ya kuwatia shauku vijana

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

 “Ni matumaini yanayothibitishwa na vijana na maaskofu, kwa mtazamo wa hali ya mateso na ukosefu wa haki msingi katika nchi zao na ambayo yanakumbana na mwangwi wa umma kudai haki zao. Kutokana na suala hili ni matarajio yangu kwamba inawezakana kuwapo sauti moja  hata ya nguvu ili kusema katika ulimwengu wa sera za kisiasa na kiuchumi  juu ya suala la ukosefu wa haki uliopo katika dunia hii”. Ndiyo matashi mema ya Kardinali Christoph Schönborn, Askofu Mkuu wa Jimbo la Vienna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Austria wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari, kwa ufupi kile kinachoendelea katika  shughuli ya Sinodi. Briefing hiyo ilifanyika mchana tarehe 26 Oktoba 2018, kama kawaida ikiongozwa na Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican.

Kutoka katika kusikiliza hadi mang’amuzi

Safari ya Sinodi ni ile ya kufanya mang’amuzi, na mwisho wake atazungumza Papa kama alivyokwisha tayari zungumza”, amethibitisha kard. Schönborn.  “Lakini awali ya yote inahitaji kusikiliza. Sinodi ni ishara kubwa ì, na kwa maana hiyo ni matashi mema ya kwamba Sinodi hiyo ionekane, isikilizwe  na kutangazwa. Akikumbusha maneno kwa namna ya pekee kwa kile alichozungumza kijana mmoja kutoka Afrika kwenye nchi ambayo inayumbishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe : “ Kanisa ni letu moja la matumaini, mahali ambapo linakaribisha na kuelewa, mahali ambapo sisi vijana tunaweza kuhisi kama nyumbani”.

Mabalozi wa Sinodi

Kwa upande wa Askofu Mkuu Eamon Martin, wa Jimbo la Armagh na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ireland, amethibitisha kuwa ,“Sinodi imekuwa kipindi cha neema”, mahali ambapo wote wamehisi  “ uwepo na nguvu ya Roho Mtakatifu”.  Na kwa maana hiyo amebainisha, nguvu hiyo na furaha hiyo, vinapaswa sasa kuhamia katika majimbo mbalimbali. Anasema:“Nitakaporudi katika nchi yangu, ninapaswa kuwa balozi wa Sinodi”. “Kanisa linataka kuwaelekeza vijana wote duniani. Linataka kufanya kazi na vijana na siyo kwa ajili ya vijana. Kwa njia hiyo ninarudi nyumbani na wazo la kwamba, vijana watakuwa ni wadau wa uinjilishaji” amethibitisha Askofu Mkuu Martin wa Ireland.

Bendi kubwa ya pamoja

Katika briefing hiyo sauti nyongine kutoka Afrika imesikika katika tafakari la Askofu Mkuu Anthony Muheria wa Nyeri Kenya, kuhusu Sinodi na kusema, “ matarajio yetu kutoka katika Sinodi hii, yanaweza kutoa cheche za moto kwa namna ya kuwatia shauku vijana”. Sisi kama maaskofu, tunayo matajio yetu ya kuweza kuwawasha mioyo ya  vijana na upendo wa Mungu”. Kwa upande wa Askofu Mkuu anakiri kwamba kuudhuria kwake Sinodi hiyo ni kama, “kusikilliza bendi moja kwa mshangao mkubwa”. Hata hivyo amebainisha kuwa, “mwanzo wa Sinodi labda, ilianza kusikika sauti ambazo hazikuwa na ulinganifu sawa. Lakini baadaye, anasisitiza, Roho Mtakatifu ametuongoza kuelekea katika ulinganifu kubwa wa sauti”.

Atakuwa Roho Mtakatifu kuongoza Kanisa

Akienda sambamba na maneno ya mwongozo wa Roho Mtakatifu, naye Padre Enrique Figaredo Alvargonzalez, Msimamizi wa Kitume huko Battambang nchini Cambodia amesema, “ Ni hakika Moyo wa Sinodi ni vijana, wito na mang’amzi, hivyo tutakuwa na nguvu mpya kwa ajili ya vijana”. Ni matarajio yetu kuwa Kanisa litatokeza likiwa limepyaishwa, lakini hiyo itakuwa ni  kazi ya Roho Mtakatifu kutuongoza”.

Vijana siyo watazamaji bali wadau wa wakati ujao

Naye kijana msikilizaji wa Sinodi Erduin Alberto Ortega Leal, mjumbe kutoka Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Cuba, wakati wa Briefing, amesisitiza kuwa “ katika Kanisa vijana hawapaswi kufikiriwa kama watazamaji, bali wao wako kweli mstari wa mbele. Dunia imejaa matatizo mengi, lakini ni dunia ambayo inaangaikia na kufikiria wakati uliopo. Badala yake, vijana wanahitaji kutazama wakati ujao. Kwa maana hiyo,“Sinodi, imetupatia fursa za kusikiliza na kuweza kusikilizwa”. Amehitimisha.

27 October 2018, 09:41