Mkutano kuhusu uandishi wa amani Mkutano kuhusu uandishi wa amani 

Ruffini:Huwezi kusimamisha muda,bali kukaa na kuutafakari!

Katika Mkutano kuhusu uandishi wa amani, uliofanyika tarehe 13 Oktoba, Bwana Ruffini amekazia juu ya kutafuta muda wa kusimama na kutafakari juu yetu. Ametumia mwandishi Rodari asemaye:"tuna maneno kwa kila kitu, tutafute maneno pamoja ili kuzungumza. Tunayo maneno ya kuuza, kununua, kuumiza,Hebu twende kutafuta pamoja, Maneno ya kupenda”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 13 Oktoba 2018, umefanyika Mkutano wa kimataifa na jukwaa juu ya uandishi wa amani. Katika mkutano huo, naye Paulo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ametoa hotuba yake, kwanza kwa kuwashukuru uwepo wao. Na kuendelea kusema kuwa; Katika kipindi kinacho kimbia haraka zaidi ni muhimu kutafuta muda wa kusimama kidogo na kutafakari juu yetu sisi ni wapi tunakwenda, na hatuwezi kusimamisha muda huo, lakini tunaweza kuwa na muda wa kusimama na kutafakari. Amemshukuru hata Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani, aliye ruhusu kuanzisha suala hili na kuwa mwenyewe binafsi katikati yao.

Salam kwa washiriki wa mkutano huo: Amemshukuru Rais wa Signis, Bi Helen Osman, na  watoa mada wote ambao wameweza kufika pale ili kutoa wazo kuhusu mawasiliano ya  amani, uandishi wa habari ya amani, katika kipindi ambacho kuna habari nyingi lakini hazihabarishi, zinazungumza, lakini hazisikilizi, zinaona lakini hazitambui. Ni katika kipindi ambacho kimezaa upweke na ukosefu wa kuwasiliano katika jamii ya mawasiliano! Ni kipindi cha hatari kinacho shawishi kuondoka katika mizizi kutokana na haraka, au kutka kukimbia kwa  haraka ili kufika mwisho, lakini bila kuwa na uvumilivu na uelewa. Ni kipindi ambacho kinatafuta kujenga daima  mbuzi wa upelelezi ili kupunguza chochote kile na hata kwa nguvu zote, ili rafiki awe adui , au  ninakupokea au ninakufuta, hadi kufikia kunyoeshe mwingine kidole!  Ni wakati ambao hujenga utambulisho uliosimikwa juu ya kukataa mwingine. Ni kipindi kina chojaribu kutushawishi kwa udanganyifu kwamba,  njia pekee mbadala tuliyo nayo ni ile ya ya kujikataa sisi wenyewe na kukataa wengine.

Sisi tumo ndani ya utandawazi uliogawanyika: Bwana Ruffini akiendelea na hotuba yake ameomba samahani mapema , kwa maana alipendelea kuwa nao hadi mwisho wa mkutano, lakini hasingeweza kutokana na majukumu ya sinodi. Pamoja na hayo ameendelea na hotuba yake kwa kusema:  “Lakini ninataka kushirikishana na  baadhi ya tafakari juu ya jukumu ambalo uandishi wa habari hufanya katika kufafanua wakati wetu, ambao unafikiria kuishia  katika kujelezea tu.Jambo ambalo kwa dhati lipo katika utandawazi uliogawanyika na ambao sisi tumo ndani yake pia ni njia za wingi wa mawasiliano na ni mitandao ya kijamii, ambayo inajumuisha mtindo wa utambulisho wetu kuwa utambulisho wa wakati endelevu. “Fursa kama hizi  za mikutano zinaweza kusaidia kuamsha maana ya sisi tulivyo na kile tunachofanya. Kadhalika amesema:“ninafikiria kwa mfano wa maneno" . Je ni mara ngapi tunayapunguza. Tunaondoa maana yake. Tunayaharibu. Huu ni mtazamo wa kwanza ambao ningependa kushirikishana nanyi”.

Maneno mazuri ya wimbo wa watoto wa mtunzi Rodari: Tunayafanyia nini maneno tunayotumia katika hadithi ya kile tu sisi tulivyo, nini tunachofanya, na jinsi gani tunavyoishi? Katika ujenzi wa historia yetu, ambayo hutumia matumizi mabaya ya maneno, hasa yanayo tutoka ghafla, na kugeuka mabaya na yenye ukatili, yanajiandika yenyewe wakati sisi tunayapitia. Katika sauti nzuri ya shahiri kwa watoto wadogo kutoka kwa mtunzi,  Gianni Rodari aliandika: “tuna maneno kwa kila kitu, tutafute maneno pamoja ili kuzungumza. Tuna maneno ya kuuza, maneno ya kununua, maneno ya kufanya maneno. Tuna maneno ya kujifanya, Maneno ya kuumiza, Hebu twende pamoja ili kutafuta maneno ya kufikiri. Hebu tuende kutafuta pamoja, Maneno ya kupenda”. Kwa njia hiyo Bwana Rufffini ameendelea kubainisha kuwa: “Maneno ni msingi wa mawasiliano yetu. Kwa hilo ni vema yakawa yale yanayofaa. Na yale ya haki, kwa hakika ni maneno ambayo yanasaidia kuelewa”.

Tafakari yake ya pili ambayo amependa kushirikisha Bwana Paolo Ruffini ilikuwa”: inatazama uhusiano kati ya amani na usalama. Hapa ametumia maneno ya mwana falsafa, Dietrich Bonhoeffer ili kujaribu kupindua hoja yenye sehemu tatu rahisi sana, kulingana na amani ambayo inategemea usalama. Hivi ni kweli?  Sio kweli. Sio kila wakati. Amani inaambatanishwa na  haki bora ambayo pamoja na usalama, ambayo sio daima sio sawa wakati wote. Na hakika sio inapompunguza mwingine kuanzia wa adui ambaye kwanza ni kujilinda naye hujitetea.

Lakini anaandika Bonhoeffer: "Amani inatengenezwaje? Kwa mfumo wa mikataba ya kisiasa? ... Kwa njia ya pesa? Au hata kwa njia ya kujihami kwa amani kwa ujumla kwa lengo la kupata amani? Hapana, si kwa njia yoyote katika mambo haya. Na hiyo ni sababu moja tu: kwa sababu hapa amani na usalama daima huchangamana. Lakini amani lazima iwe nawasiwasi, kwa maana kamwe huiwezi kuwa na uhakika. Amani ni kinyume cha usalama, kuhitaji usalama ina maana ya kuwa na mashaka, na kwa maana hiyo ukosefu wa uaminifu unazaa vita”. Na hapa Bwana Ruffini anasema ndiyo kipengele kingine cha kutafakari kuhusu njia tunayoelewa ya mawasiliano.  Hiyo inashughulika na wajibu, kwa kila mwandishi mzuriwa habari yeyote, sio kuona mambo kwa mtazamo mmoja tu. Ni uwajibu wa kuuliza maswali. Na katika suala hilo la kutofautisha kati ya usalama wa haki haki na ule usio wa haki.

Tafakari la tatu linatazama ukuu wa kazi ya kung’amua kitu gani cha kusimulia: Katika hilo, Bwana Ruffini amependelea kutumia maneno ya Italo Calvino ambaye ni mwandishi wa vitabu wa kiitaliano ambaye, ambapo anasema, ili kuzungumza hata katika shughuli hiyo  inaweza kukuingiza jehanamu au kujenga amani. Nukuu hiyo imechukuliwa kutoka katika kitabu cha Miji isiyoonekana chenye kichwa cha: “Jahannamu ya walio hai ni ile tunayoishi kila siku. Kuna njia mbili za kutoteseka. Ya kwanza ni rahisi kwa walio wengi: kukubali kuzimu na kuwa sehemu yake hadi mwisho wa kutoiona tena. Ya pili ni hatari na inahitaji tahadhari na mafunzo ya kuendelea: kutafuta na kujua jinsi ya kutambua nani na nini, katikati ya kuzimu, sio kuzimu, na kuifanya idumu, na kuipa nafasi”.  Kwa maana hiyo akifafanua juu ya maandishi hayo, Bwana Ruffini anasema: “hebu tazama katika kuipa nafasi, ipo nafasi ya uandishi wa amani”

Tafakari  ya nne na ya mwisho ambayo ametaka  kushirikisha  inatazama uhusiano ambao  katika mkutano huo pia ni pamoja na  mada ya ijayo ya Ujumbe wa Siku ya Mawasiliano Duniani. Bwana Ruffini amesema: “Katika Mkutano huu pia unawakilisha, kwa namna fulani, kifungu cha ushuhuda kati ya tafakari ambayo Papa Francisko ametualika kufanya kwa mwaka jana na ile analiyopendekeza kwa mwaka ujao 2019, na akituonya juu ya kutopunguze dhana ya jumuiya katika mantiki za kijujuu tu na rahisi.

Hakuna jamii  ikiwa hakuna jumuiya: Wakati wa kuunganishwa, wa mitandao ya kijamii, ya mabadiliko kutoka katika jamii ya mawasiliano hadi jamii ya mazungumzo, lazima tuwe makini ili tusije kubadilika katika  mtandao kwa kile ambacho kwa asili yake sio (na siyo lazima): mahali ambapo kadili tunavyoingia zaidi ndivyo tunavopoteza muungano wa kipekee, utambulisho wa mtu binafsi. Na hata mwelekeo. Uwezo wa kutofautisha kati ya kweli na uongo. Kilicho cha dhati na ambacho hakifai. Kwa kubaki umenaswa katika mchezo ambao unaishia kufuta kila uhusiano wa kweli, kila mazungumzo ya dhati, na kila uwezo wa kuelewa.

Kufuatana na hilo, Bwana Ruffini anathibitisha:“Tunapaswa kurudisha katika mtandao maana yake nzuri zaidi, na zaidi inayohusishwa na hali halisi ya mwanadamu: uzuri wa kukutana, wa mazungumzo, ya ujuzi, wa uhusiano”.  Ukuu wa mwelekeo wa digital ni wa kweli hata kama haujakamilika, lakini isiwe wa kimtandao tu. Na ndiyo sababu tunahitaji kuanzia kutoka katika uhalisia wa watu wote na kutoka katika ukweli wa mahusiano ya kweli, ili kuweza kugundua kwa upya uzuri wa amani, na kuufungamanisha katika upya wa kwanza. Lakini hiyo lazima kuanzia katika kanuni ya kwanza. “Usiwafanyie wengine kile ambacho hutaki kufanyiwa wewe”.

Wafanyie wengine kile ambacho ungependa wakufanyie wewe: Bwana Ruffini akiendelea amesema, Papa Paulo VI  alikuwa sahihi kusema kuwa: wengine wanafikiri ni ndoto, hadithi, kipeo cha hali nzuri. Lakini Sisi badala yake tunasema kuwa amani ni jambo gumu, ngumu sana na zaidi; lakini ni jambo linalowezekana, na ni jambo ambalo ni muhimu”. Kadhalika alikuwa sahihi hata Oscar Romero: “Huu ni ugonjwa mkubwa wa dunia ya leo: bila kujua jinsi ya kupenda. Utafikiri ninamwona Kristo, mwenye huzuni, wakati anasema: Nilikuwa nimewambia mpendane ninyi kama nilivyo wapenda”,  (03/23/78).

Kuwakumbuka watakatifu wapya: Kwa kuhitimisha amesema, tarehe 14 Oktoba Papa Paulo VI na Oscar Romero watatangazwa watakatifu, na kuna mwendelezo ambao unatuunganisha sisi wote kwa Papa ambaye ametuomba kama wahudumu wa tasnia ya mawasiliano ya jamii kufanya juhudi ili kutangazia juu ya paa, Ujumbe wa Kristo (njia, ukweli na maisha) katika ulimwengu ambao nuru yake inatafuta karibu kuzimwa. Kadhalika unatuunganisha na Askofu mfiadini ambaye alijikita kufanya hivyo bila kujisalimisha kwa waongo wa nyakati. Kuunganishwa katika uzi huo kwa upya  ni njia ya kuchangia katika ujenzi wa uandishi wa habari wa amani. Amehitimisha Bwana Paulo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

13 October 2018, 15:58