Cerca

Vatican News
Papa Yohane XXIII Papa Yohane XXIII   (Vatican Media)

Papa Yohane XXIII ni urithi wa upendo!

Tarehe 11 Oktoba Mama Kanisa anakumbuka Papa Yohane XXIII. Ni siku ambayo kwa dhati inakwenda sambamba na maadhimisho ya hatua ya kwanza ya Mtaguso wa wa Pili wa Vatican katika usiku wa “hotuba juu ya mwezi” kama ijulikanavyo katika historia ya wengi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 11 Oktoba katika Liturujia, inakumbuka Mtakatifu Yohane XXIII. Ni siku ambayo kwa dhati imekutana na maadhimisho ya hatua ya kwanza ya Mtaguso wa wa Pili wa Vatican katika usiku wa “hotuba juu ya mwezi”. Chini ya Mlima  na vilima vya utakatifu, alizaliwa muda mfupi wa roho ya kuhudumia wote. Alfa na Omega ya Angelo Roncalli mtoto aliye zaliwa katika kijiji, lakini baadaye atachagua jina la Yohane XXIII , ili kufanya mapinduzi ya Kanisa. Na tangu mwaka 2014 baada ya kutangazwa Mtakatifu, kila tarehe 11 Oktoba ni tarehe ambayo inakumbuka Papa Roncali , siku ambayo inakumbuka mwaka 1962 kufunguliwa kwa Mtagysu wa Pili wa Vatican.

Chini ya Mlima

Kati ya mwezi wa tano na wa sita mwaka huu, masalia ya  Papa Mtakatifu Yohane  XXIII yalipelekwa katika maeneo alipozaliwa na ujana wake kwa wiki kadhaa. Kati ya mji wa Bergamo na mji mdogo alikozaliwa, uwepo ambao unakumbusha Yohane XXIII  na kuweza kuwambusha mambo mengi hasa ya mtoto wa mkulima ambaye aliweza kuendesha mtumbwi wa Petro. Kutokana na tukio hilo, Vatican News, ilifungua mfumo wa WebDoc  kwenye mtanado ya kijamii na ambao unafanana na wa siku hizi kwa ajili ya Papa Paulo VI, ambao umeweza kutangaza kila siku tangu tarehe 21 Mei  hadi 10 Juni 2018, pakiwepo Clip ya video juu ya hija ya masalia na mantiki nyingine zinazo husu “Papa Mwema”.

Usiku wa mwezi

Tarehe 11 pia ni siku ambayo katika kelenda haioneshi rasmi, lakini ni siku ambayo ni ya kihistoria na ambayo kwa sasa miaka 56 iliyopita  ya masimulizi halisi ya hotuba kuu ya Papa Yohane XXIII. Usiku ule ndipo ulianzishwa Mtaguso wa Vatican II, wakati huo  Papa Yohane XXIII alifungua dirisha katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, na kutamka maneno ambayo baadaye yamekuwa katika historia na kujulikana,“ hotuba ya mwezi”. Ni siku wa upendo wa kumbembeleza  na maono ya dunia”, kubembeleza ambako Papa alipotazama umati wa watu wakiwa na mshumaa mikononi mwao inawaka utafiriki ni rangi nyeupe na kama ilivyokuwa ikitumika televisheni ya wakati ule, aliwaomba wote waliokuwa wamefika watakaporudi  nyumbani kwao, wawasalimie watoto wao na katika bembelezo.

Ishara ndogo kubwa mno

Bembelezo la usiku wa tarehe 11 ,hakuna mtu yoyote ambaye angeweza kusahau, na  ndiyo ukawa  urithi mkubwa. Hata hivyo baadaye, Papa Yohane XXIII atazungumza juu ya amani ili kusaidia ulimwengu ambao kipindi hicho kulikuwa na vita baridi ili iweze kuwa na matarajio mema ya amani. Kadhalika Papa Yohane XIII ataweka Kanisa mikononi mwake ili kuliondoa dhidi ya mashambulizi ya kujifungia na ili litoke nje na kwa ajili ya ukaribu wa jirani. Upeo wake alio kuwa nao, ndiyo pia mwendelezo wa Papa Francisko, kwani mara nyingi amesisitiza juu ya Kanisa ambalo liwe kama hospitali katika kambi, na kuwa karibu na watu, ambao wametupwa pembezoni mwa jamii.

 

 

11 October 2018, 13:51