Cerca

Vatican News
Kujadili juu ya Kipindi cha Salam Maria cha Padre Marco Pozza na Papa Francisko Kujadili juu ya Kipindi cha Salam Maria cha Padre Marco Pozza na Papa Francisko  

Papa Francisko:ukawaida wa Maria ni utakatifu wa kila siku!

Ukawaida wa Mama Maria na utakatifu wake ni moja ya mada alizogusa Papa Francisko wakati wa mahojiano katika maandalizi ya kipindi cha “Salam Maria " kilichotayarishwa na TV2000 kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Hivyo ni vipindi vitakavyo anza tarehe 16 Oktoba 2018.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mahojiano ya Papa ambayo yatakwenda katika kipindi cha “Salam Maria” kitakacho onekana katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia(TV2000). Ni vipindi kumi na moja kwa ajili ya kuelezea sala ya inayopendwa ya Mama Maria. oPapa Francisko anasema kiwa: "Mama Maria ni msichana wa kawaida, ni msichana wa leo, msichana ambaye hawezi kusema “ni wa mjini kwa sababu yeye hakuwa wa mjini, lakini wa kijijini,  na wa kawaida, aliye elimishwa kwa kawaida, aliye wazi katika kuolewa na kutengeneza familia”.

Historia kumi na moja

Kipindi kinacho tayarishwa na kuendeshwa na Padre Marko Pozza, wa Kanisa dogo la wafungwa huko Padova Italia, ikiwa ni katika mwendelezo wa kipindi kilichokuwa cha “Baba Yetu”, ambacho kilifanyika mwaka jana. Kipindi hiki kinapendekeza kuelezea juu ya “sala ya Maria” ambayo imeenea duniani kote kwa njia ya mahojiano ya wanawake wa utamaduni wa na tamasha katika televisheni, kuanzia kwa Michelle Hunziker hadi mwandishi Federica Angeli, zaidi ya histaria ya wazazi wanawake na watoto ambao watasimulia jinsi gani sura ya Maria imejikita katika maisha yao. Kipindi cha kwanza kitaonesha kuanzia  tarehe 16 Oktoba 2018 na Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia (TV2000)

Tarehe 23 Desemba itakuwa ni mahojiano ya Papa

Mojawapo ya vipindi 11, vimewekwa kwa ajili ya “Salam Maria” na viwili kwa ajili ya “Utenzi wa Bikira Maria” (Magnificat) , vitakavyokuwa na utangulizi kwanza wa mahojiano ya Papa Francisko, na baadaye kuendelea na mtu mgeni atakaye kuwa amekaribishwa wa utamaduni, sanaa au kawaida na ambapo mahojiano kamili ya Baba Mtakatifu yataonesha tarehe 23 Desemba 2018. Hata hivyo katika matayarisho, ya vipindi hivi tayari yanaonesha kuwa:  “Kila mwanamke katika dunia hii, anasema Papa, anaweza kusema kwamba, mimi ninaweza kumuiga Maria kwa sababu ni mtu wa kawaida”. Hata ndoa yao ya kibikira, ya  utakaso ilikuwa ni ndoa ya kawaida: kazi , kununua vitu, kutayarisha nyumba, kuelimisha mtoto, na kumsaidia mume”.

09 October 2018, 11:06