Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Montenegro Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Montenegro 

Papa amekutana na Rais wa nchi ya Montenegro Bw.Djukanović

Mara baada ya Mkutano wa Papa Francisko na Rais wa Montenegro, mada muhimu zinazohusu kanda kama vile wajibu wa kuhamasisha kuishi pamoja kindugu, dini mbalimbali, kutunza urithi wa mazingira ndiyo mazungumzo yaliyofuata kati ya Rais Djukanović na Kardinali Parolin Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Gallagher

Asubuhi ya tarehe 8 Oktoba, Papa Francisko amekutana katika nyumba ya Kitume na Rais wa Jamhuri ya Montenegro,Bwana, Milo Djukanović, na kufuatia mkutano na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambaztana  na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican anayeshughulikia masuala ya  mahusiano na ushirikiano wa nchi za nje.

Katika mazungumzo yao, wote pamoja wameonesha pongezi kubwa  ya uwepo wa mahusiano mema kati ya Vatican na Jamhuri ya nchi ya Montenegro, uliosimikwa na mkataba wa Makubaliano tangu mwaka 2011. Pia wameweka bayana juu ya  mchango chanya unaotolewa na jumuiya katoliki katika jamii ya Montenegro.

Pamoja na hayo pia wamejikita kutazama hali halisi ya nchi na mchakato wa ushirikishwaji wa Ulaya, pamoja na mada muhimu zinazohusu kanda. Kati ya  mada  hizo ni wajibu wa kuhamasisha kuishi kwa pamoja kindugu, dini mbalimbali,na  utunzaji bora wa urithi wa mazingira. Na hatimaye wamebadilishana mawazo tofauti yanayohusu masuala ya kimataifa na kwa namna ya pekee juu ya suluhisho la migogoro.

 

08 October 2018, 16:22