Padre Tullio Maruzzo na Luis Obdulio wafiadini nchini Guatemala watangazwa kuwa wenyeheri Padre Tullio Maruzzo na Luis Obdulio wafiadini nchini Guatemala watangazwa kuwa wenyeheri 

P.Tullio Maruzzo na Luis Obdulio wafiadini dhidi ya ufisadi

Kardinali Angelo Becciu Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu, amwewatangaz wenyeheri, Padre Tullio Maruzzo na Luis Obdulio, tarehe 27 Oktoba 2018, huko Morales nchini Guatemala. "Mashahidi wa Guatemala", ndivyo walivyokuwa wanaitwa katika nchi ile nzuri ambayo walimwaga damu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mahubiri yake Kardinali Angelo Becciu Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu ameongoza Misa Takatifu  tarehe 27 Oktoba 2018, huko Morales nchini Guatemala ambapo amejikitia kukumbusha sura ya hawa wenye heri wapya, Padre Tullio, ambaye alikuwa Mchungaji Mwema, aliyetambua na kupenda zizi alilokabidhiwa, aliwafundisha  watu wake na kuwaimarisha imani, ambayo ilijimwilisha kwa upendo hasa kuwalinda dhidi ya mabaya: alikuwa akitangaza haki na kutetea ukweli. Aliwaangazia dhamiri kwa zawadi ya maisha yao ili waweze kutoa matunda kwa amani.

Padre Tullio Maruzzo, alikuwa mfranciskani kutoka Italia, aliyekwenda katika nchi ya Kimisionari, kwenye Bara la  Amerika ya Kusini na Luis Obdulio Arroyo Navarro, aliyekuwa ni dreva na msekulari wa daraja la tatu la shirika la wafransikani, na ambao kwa pamoja wameinuliwa katika altare ya Bwana kama wenyeheri wafiadini. Kardinali Becciu akiendelea kufafanua wasifu wa kila mmoja amesema watu wa Guatemala, wamekuwa wakisali kwa ajili ya wafia duni ha ambao waliuwawa pamoja kunako tarehe1 Julai 1981 wakati wakirudia parokiani kwako wakitokea kufanya katekesi katika vigango!.

Padre Tullio, na kaka yake pacha katika imani moja

Padre Tulio alizaliwa huko Lapio, Vincenza nchini Italia na familia ya watoto 8, alibatizwa kwa jina la Marcello na akiwa ni pacha na Daniele , ambao walishikirishana masomo yao  na baada wakafanya mang’amuzi ya miito. Wakiwa na mika 10 waliingia katika chuo cha kifransiskani huko Chiampo Italia; kunako 1946 walifunga nadhiri za kimaskini, utii na ufukara, ambapo walibadili majina na kuitwa Tulio na Lucio. Kunako mwaka 1953 walipewa daraja la upadre na aliyekuwa Patriaki wa Venezia Angelo Roncalli, leo hii ni Mtakatifu Yohane XXIII. Mfano wa utakatifu ambao ulijionesha  mapema katika safari ya Padre Tullio ni kutumwa kwenda kufanya shughuli katika kituo cha watoto yatima, Italia, wakati huo pacha wake akatumwa kwenda katika nchi za kimisionari kwa miaka minne kabla yake.

Unjilishaji wa eneo hilo…. mara mbili

Hatimaye kunako mwaka 1960 Padre Tullio naye alitimiza ndoto yake ya kwenda katika nchi ya kimisonari huko Guatemala. Katika bara la Amerika ya Kusini, ndugu wadogo wa kifransiskani walikuwa wawewasili tangu karne ya XVIII, lakini kutokana na kuzuka kwa chama cha watu wakiwa wanadai  kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uhispania , walisababisha vurugu kubwa ambayo ilisababisha kufukuzwa kwa mashirika yote ya dini yaliyokuwa yameingia nchini humo. Ni katika nusu ya karne ya ishirini kwa njia ya utume wa Vatican katika eneo hilo, wamisionari, waliweza kuingia kwa mara nyingine  tena nchini Guatemalam wakifuata mfano wa Mtakatifu Francisko wa Asisi aliyesikia sauti ile ya Msalaba wa Mtakatifu Damiani,  na walikubali majukumu hayo magumu na kwenda katika maparokia ya vijiji vya mbali kwa watu wake wa asili. Hakuwa na mshangao  zaidi kwa upande wa Padre Tullio ambaye kwanza alitumwa huko Puerto Barrios, baadaye  Entre Rios na mwisho, Morales, lakini daima akitokea kituo kikuu cha Izabal.

Matatizo yalikuwa daima ni yake ye hasa ya kuratibu

Matatizo yalikuwa dauma hasa ya Jumuiya za kikanisa kwa mtazamo wa kibinadamu na wakati mwingine hata kiafya  na pia kwa kwanza kujenga majengo ya makanisa. Padre Tulllio alianza kuwafundisha makatekista wapya, ili waweze kumsaidia katika kazi ngumu ya kutembea kutoka kijiji hadi kingine ambavyo daima vilikuwa ndani ya misitu ya kitropiki, ili aweze kupelekea kila kona ya nchi Neno la Bwana. Hata hivyo ili mbisi atumie njia mbalimbali ili watu waweza kupokea Neno la Mungu ambapo ilibidi atembeea akiwa  na mambo mbalimbali ya upendo na kutoa huduma mahalia kuwasaidia, lakini hiyo iliongozana na tabasamu yake iliyokuwa ni tabia yake, na  mfano wake mzuri wa kuigwa  uliweza kuwavuta wengi na haraka akapendwa na wote.

Luis Obdulio, kijana katika kutafuta utakatifu

Kijana Pbdulio aliwakuwa anatokea Quiriguá, katika eneo  hilo mahalia  na ambapo baadaye akawa msaidizi wa karibu wa Padre Tullio. Pamoja na hayo yeye alikuwa karibu na Bwana, akiudhuria mara nyingi Parokiani na kutoa kila huduma ambayo padre Tullio alihitaji. Alihudumia misa, kuandaa sikukuu za Kuzaliwa kwa Bwana, aliandaa Juma Takatifu Kuu na kuwahamasisha familia nyingi na ya kwake katika sala. Yote hayo yakikuwa akichangia kumsaidia awe  mbali na ulievi. Janga ambalo liliwakumba vijana wengine rika lake katika maeneo hayo mahalia. Alikuwa amejikita katika kutoa huduma kwa ajili ya jirani, hata jitihada kama dreva wa Tarafa ya Los Amates, lakini ilionekana mara nyingi akimsindikiza kwa hatua nyingi Padre Tullio ambaye alikuwa akitembelea kwenda katika vijiji.

Kutokana na kufahamiana naye Padre Tulio na makutanao hayo mazuri, ndipo ilimsaidia kujiunga na daraja la Tatu la Mtakatifu Francisko wa Asisi, japokuwa hali ilianza mapema  kuwa ngumu kwasababu, Padre Tulio alipewa tahadhari ya kifo,  na hivyo familia ya Dreva Luis ilimwomba asimsindikize tena, lakini yeye alijibu “ mimi siogopi,  kwanini nirudi nyuma  na kuacha kutoa huduma ya parokia? Na kama nitakufa karibu na padre, ninafikiri ni neema. Kwa dhati Kardinali Becciu amesema hilo ni jibu la Mtakatifu!

Kifo chao wafiadini hao

Ilikuwa siku moja wakati wa kiangazi, kikundi cha wanajeshi, kililazimisha mtoto wa miaka 11 aombe msaada barabarani ambapo ilikuwa ni eneo  katikati  ya msitu na la hatari sana. Gari likiwa linaendeshwa na Luis Obdulio akimrudisha Padre Tullio katika Parokia, lilisimama mara ili kumsaidia mtoto huyo kama kawaida ya walivyokuwa wamezoea. Na kumbe ndiyo ulikuwa mtego wa siku yao ya mwisho ya watumishi hawa wakapigwa risasi na kuachwa katikati ya barabara wamekufa. Licha ya hofu uliyokuwapo katika eneo hilo, mwangwi wa kifo chao ulikuwa na nguvu zaidi katika nmaziko yao yaliyoadhimishwa na maaskofu 4 na mapadre karibia hamsini na kuudhuriwa na mamia ya wanaparokia waliotelemka kutoka katika milima yao ili waweze kuudhuria siku hiyo ya mazishi yao!

Sadaka yao hadi sasa bado inaendelea. Kwa ,aana imetia chachu Kanisa mahalia na kuwafanya wawe na ufahami zaidi wa nini maana ya utume wao, na hata kuzaliwa kwa miito mingi. Baada ya siku 27 ya kifo chao, nchini Guatemala aliuwawa mmisionari mwingine Padre Rother aliyekuwa mfiadini wa kwanza kutoka Marekani na ambaye alitambuliwa na Kanisa na kuinuliwa  katika Altare ya Bwana mwaka mmoja uliopita.

 

29 October 2018, 14:20