Tafuta

Vatican News
Papa  amemteua monsinyo Mellino kuwa katibu msaidizi wa 'C9' Papa amemteua monsinyo Mellino kuwa katibu msaidizi wa 'C9'   (ANSA)

Monsinyo Mellino ni Katibu Msaidizi mpya wa Baraza la Makardinali 'C9'

Hivi karibuni Papa Francisko amefanya uteuzi wa Monsinyo Marco Maellino kuwa katibu msaidizi wa Baraza la Makardinali kwa jina jingine C9. Ni Baraza lililoundwa kwa utashi wa Baba Mtakatifu, ili wapate kumsaidia katika majukumu yake ya utume wa Kanisa la Ulimwengu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hivi karibuni, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Marco Mellino kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Makardinali (C9),  ambaye pia mjumbe wa Baraza la Kipapa la Nyaraka za kisheria. Hadi kufikia kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu Mkuu wa Jimbo katoliki la Alba nchini Italia.

Baraza la makardinali C9

Baraza hili, ni Baraza la Makardinali tisa kwa jina jingine linaitwa (C9 ) kwa utashi wa Papa Francisko ambapo liliundwa kwa lengo la kumsaidia Papa Francisko katika majukumu yake ya utume  wa Kanisa la Ulimwengu na ili kufanya utafiti wa mpango wa kupyaisha katiba  ya Kichungaji ( Pastor Bunus) mjini Vatican.

Katibu mpya msaidizi Monsinyo Marco Mellino

Monsinyo Marco Mellino alizaliwa huko Canale kunako tarehe 3Agosti 1966 na kujiunga na Seminari ndogo ya jimbo huko Alba kunako 1973, mahali alipopata diploma na kuendelea na mafunzo ya Taalimungu katika Chuo cha Mafunzo cha Taalimungu huko Fossano Italia.  Kunako mwaka 1991 alipata daraja Takatifu la upadre huko Alba Italia. Baada ya miaka katika huduma ya kichungaji, kunako 1997 alihamia Roma ili kuendelea ma mafunzo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano.

Katika chuo hicho kati ya 1999-2000 alipata shahada ya uzamivu wa Sheria.  Mara baada ya kurudi katika jimbo lake, alichaguliwa kuwa hakimu katika Mahakama ya Kanda ya Piemonte, yenye makao makuu mjini Torino na Paroko wa Parokia ya mji wa Piana Biglini. Hatha hivyo tangu 2009 amekuwa akishiriki kama hakimu wa nji katika mahakama ya Kanisa la Roma. Na wakati huohuo mwaka huo alichaguliwa kuwa Padre mhudumu  wa Kanisa dogo la Baba Mtakatifu mjini Vatican.  Kadhalika ameshika pia nafasi nyingine ya kutoa huduma katika kitengo cha  Ofisi ya Katibu Mkuu  Vatican kuanza Septemba 2006 hadi  tarehe 30 Juni 2018, ambapo alirudi katika jimbo lake na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa jimbo lake.

31 October 2018, 10:19