Tafuta

Mnye heri Jean Baptiste Fouque huko Marsiglia, Ufaransa Mnye heri Jean Baptiste Fouque huko Marsiglia, Ufaransa 

Kard.Becciu:Mwenyeheri Padre Fouque ni mfano wa ukuhani mtakatifu!

Mwenyeheri Padre Jean-Baptiste Fouque ni mfano wa ukuhani mtakatifu, kwa mujibu wa Kardinali Angelo Bechu,Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu na wenyeheri, wakati wa maadhimisho ya kumtangaza mwenyeheri mpya wa Kanisa huko Marsiglia,Ufaransa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Katika mahubiri yake Kardinali Angelo Beccui Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu na wenyeheri wakati wa mahubiri yake katika Maadhimisho ya kumtangaza Mwenyeheri mpya   Padre Jean-Baptiste Fouque anasema, katika maisha yake alikuwa ni mfano wa kusaidia kuwatia moyo mapadre wote. Na kwa sababu ya dhambi kubwa kutokana na baadhi ya wakuhani wa Kanisa, lazima kuwa mapadre ambao wanafanya upendo wa Mungu anayetafutwa katika sala na katika Ekaristi Takatifu kitovu cha maisha yote kwa ajili ya kutoa huduma kwa ndugu.

Mwenyeheri Jean-Baptiste Fouque ni Nabii kwa maana katika yeye aliunguzwa na moto wa upendo wa Mungu, na upendo wa jirani ambao aliweza kuonesha wazi kwa wote hasa wale ambao wameitwa katika daraja la ukuhani mkuu.

Kardinali Beccicu amethibitisha kuwa, Mwenyeheri mpya anawakumbusha wao kama wenye wakfu na waseminari ambao wako katika kipindi cha mwanzo wa wito wao , ili waweze kuwa watu wa Mungu , kuwakimbilia ndugu kaka na dada kama alivyokuwa akifanya Bwana, kushuhudia ukweli na uwezo wa kuwapokea na kuwasikiliza.

Katika muktadha huo, Kardinali Becciu pia amewaalika kusali kwa Bikira Maria, ili aweze kuwapatia mapadre watakatifu, kutokana na dhambi kubwa kwa baadhi ya wahudumu wake katika Kanisa, na kwa maana hiyo kuna mahitaji ya namna ya kuwa mapadre kwa mfano wa Padre Fouque, mwenye uwezo wa kutengeneza upendo wa Mungu, katika sala, ekarisitia, kiini cha maisha ya kuhudumia watu wake.

Zaidi ya miaka 90 tangu kuzaliwa mbinguni mwenye heri mpya, wanawake na wanaume, wamweza kuendeleza utume katika matendo ya dhati aliyoanzisha kwa kujikita si katika kuwasaidia watoto, lakini hata wale ambao walijitambua ni wadhaifu katika hali halisi ya maisha,hata  kuanzia katika umri wao. Huo ndiyo ushuhuda wa upendo ambao aliutimiza kwa jina la Yesu na kwa njia ya Neno la Yesu.

Lakini pamoja na hayo hata leo hii, Mwenyeheri Fouque, anaendelea kwa kwa njia ya wamisionari wa ukarimu na huruma, Kardinali Becciu amethibitisha. Na hiyo ni huruma kama ya  mtoto  ambayo ni kubwa sana katika matendo ya upendo.  Mwenyeheri mpya alipenda kusali hivi: “Mungu wangu kwa mara nyingine nisamehe, niwekee nafasi, mimi sisitahili, mimi maskini mdogo katika Moyo wako na nibariki”.

03 October 2018, 08:53