Tafuta

Vatican News
2018-02-06 donne africane 2018-02-06 donne africane 

Ask.Mkuu Auza:Jamii zilinde wanawake dhidi ya vurugu na vitisho!

Askofu Mkuu Auza anasema inatia moyo kuona kuwa mamilioni ya wanawake sasa wanahusika kikamilifu katika maisha ya umma na kisiasa kama wanachama wa vyama vya siasa, viongozi waliochaguliwa au watumishi wa umma na karibu wanawake zaidi ya 10,000 leo hutumikia umma kama wabunge wa kitaifa, licha ya vurugu na vitisho dhidi yao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Uwakilishi wangu unamshukuru Katibu Mkuu kwa namna ya pekee, Ripoti inayotoa umakini kwa ujumla juu ya suala halisi la vurugu dhidi ya wanawake na wasichana hasa wanawake  katika  sera za kisiasa na wale ambao wanaingizwa katika biashara haram ya binadamu na aina mbalimbali za utumwa. Papa Francisko ametaja  suala  la biashara ya binadamu kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, na lazima kuushutumia na kupigwa marufuku. Leo hii suala la utumwa linafikiriwa kuwa ndiyo kumbukumbu  kuu zaidi  ya ilivyowahi kutokea nyakati za nyuma za kihistoria. Huo ni mwanzo wa hotuba ya Askofu Mkuu Bernardito Auza Mwalikishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani  akiwa katika Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa kwenye   Kamati ya tatu kuhusu “uhamasishaji wa wanawake”,  kunzia tarehe 5-8 Oktoba 2018.

Pongezi kwa mashirika ya kitawa kama vile la Talihtha Kum

Askofu Mkuu Auza akiendelea na hotuba yake amesemaMheshimiwa aliyetoa Ripoti  maalum, ameshukuru kuongezeka kwa harakati za kupambana na utumwa wa wanawake zinazoongozwa na wanawake : "kuandaa ulinzi bora wa haki za wafanyakazi wa ndani, wa kilimo na wahamiaji”. Lakini kati ya wengine, anabainisha, wapo hata dada Wakatoliki  ulimwenguni kote ambao huchangia katika jitihada hizi muhimu kupitia mitandao ya kimataifa ya mashirika ya kitawa dhidi ya biashara ya usafirishaji wa watu, kama vile chama cha  Talitha Kum, au kupitia uwekezaji katika elimu na ajira kwa vijana, hivyo kushughulikia kwa kiasi kikubwa, sababu kubwa sana zinazofanya wanawake na wasichana wawe katika mazingira magumu na kufanyiwa biashara haramu.

Katika suala hili, Papa Francisko alionesha wasiwasi mkubwa hasa alipoona sema kwamba: “ikiwa kuna wanawake wengi vijana waathirika wa biashara ambao wameishia mitaani katika miji yetu, ni kwa sababu watu wengi hapa, yaani vijana, wenye umri wa kati, wazee,  wanataka huduma hizi”. "Tuna wajibu wa haki ya kukamata na kuwashtaki wafanyabiashara, lakini pia tunapaswa kukumbuka kuwa, ikiwa tunapaswa kuondokana na uovu huo: “kubadili mioyo, kuimarisha mahitaji na kukausha soko ni mambo muhimu ya yanayohitajika”. Amesisitiza Askofu Mkuu Auza!  Hata hivyo ameseme , inatia moyo kuona kuwa “mamilioni ya wanawake sasa wanahusika kikamilifu katika maisha ya umma na kisiasa kama wanachama wa vyama vya siasa, viongozi waliochaguliwa au watumishi wa umma” na kwamba, “wanawake zaidi ya 10,000 leo hutumikia  umma kama wabunge wa kitaifa”.”Wanawake hawa hufanya, “mchango muhimu” katika serikali katika kuanzishwa kwa miundo ya kiuchumi na ya kisiasa ambayo inastahiki zaidi ubinadamu”.

Jumuiya zilinde wanawake dhidi ya vurugu na vitisho

Wanapojenga jumuiya zetu, zaidi lazima ifanyike juhudi ili kuwalinda kutokana na vurugu na vitisho. Vatican inashutumu vikali, kila aina yoyote za unyanyasaji dhidi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na madhara mabaya yanayothibitishwa na vurugu na kukuza ubaguzi dhidi yao. Askofu Mkuu Auza ameongeza kutoa mfano kuwa:“ Wakati wa ziara yake Papa Francisko nchini Peru, mapema mwaka huu, alithibitisha kwamba “unyanyasaji dhidi ya wanawake hauwezi kutibiwa tu kama jambo la kawaida “wakati kuna ishara za kudumisha utamaduni kipofu wa mabavu ya kiume” na  wakati huo ho nafasi ya wanawake waliyo nayo katika jamii zetu, ndiyo inayoongoza” . Kadhalika Papa aliongeza kusema “ hatuwezi kuangalia kwa njia nyingine na kuruhusu heshima ya wanawake, hasa wanawake vijana ikanyagwe, juu yao”.

Hata hivyo Ripoti ya Katibu Mkuu aliyoitoa inaonesha kuenea kwa ukatili wa unyanyasaji wa kimwili,  kwa maneno, hata kwa wanawake na wasichana na kuonesha haja ya hatua za kisheria katika kulinda ushiriki wa wanawake katika jamii, bila hofu ya unyanyasaji. Askofu Mkuu Auza anathibitisha kuwa, ingawa ni jambo la kuhimiza na kutia moyo katika kuona  kampeni za kuhamasisha ufahamu na kuongezeka kwa ushiriki wa wanaume, wavulana na viongozi wa jamii, lakini ni suala la wasiwasi mkubwa ambalo  bado lipo katika nchi nyingi, kwa maana wadau wa unyanyasaji wa nyumbani hubakia bado wasioadhibiwa!

Familia ni gundi ya jamii

Kadhalika Askofu Mkuu amesema: “Familia ni gundi ya jamii, na hivyo wakati familia inapokuwa mahali penye vurugu, madhara ni mabaya kwa wote. Kwa njia hiyo tunapaswa kutenda kwa dhati hasa kutafuta juu chini chanzo hiki cha mateso kwa kila uwezekano wa chombo chochote cha kisheria na ili kukuza utamaduni unaokataa kila aina ya vurugu. Aina nyingine ya unyanyasaji na kutengwa inakuja kama matokeo ya kile ambacho Papa Francisko anachoita “utamaduni wa kutupa nje au kibaguzi”.  Katika Mkutano wa Familia Dunia wa hivi karibuni huko Dunblin nchini Ireland, alisema kuwa, “utamaduni ambao tunaishi hupoteza kila kitu ... ambacho hakitumiki tena”. “Huwafukuza watoto kwa sababu wana shida; na huwatupa wazee kwa sababu hawana faida”.

Jamii  linatesekana wakati isopojumuisha wazee, na wanawake wazee hasa  kwa namna ya pekee  mara nyingi wanafikiriwa kuwa hawana thamani tena. Hata hivyo, bibi zetu, ndio wanaweza kuwafundisha utamaduni, maadili na hekima kwa vizazi endelevu, kwa kuwakikikishia kwa njia hizo  endelevu za wakati bota wa siku zilizopita na zile endelevu. Akofu Mkuu Auza amesemaWakati wa kujenga wakati endelevu wa jamii zetu, tunapaswa kutafuta njia za kutambua na kuunga mkono wanawake wengi wasiokuwa na furaha na ambao kila mmoja kwa njia yake mwenyewe huendeleza na kubadilisha familia na jamii. Wanastahili shukrani na upendo wetu, kwani ndio ambao hutuokoa ili tusiondolewa katika utamaduni wa leo na hata kuupoteza.

09 October 2018, 14:28