Tafuta

Vatican News
arcivescovo Ivan Jurkovic arcivescovo Ivan Jurkovic 

Ask.Jurkovič:ufumbuzi wa uhamiaji ni kutafuta haki katika nchi mahalia

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, anasema njia kamili ya kufikia ufumbuzi wa muda mrefu na kutambua ndoto ya kila mkimbizi, ni kuhakikisha haki za wote kuishi katika nchi zao za asili, na kustawi kwa heshima, amani, na usalama

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Mwanzoni, niruhusu nitoe sauti ya Papa Francisko katika sala na salam za rambi rambi kwa watu wa Indonesia na kwa wale ambao wanateseka kwa sababu ya majanga ya asili”. Ndiyo mwanzo wa Hotuba ya Askofu Mkuu Ivan Jurkovič mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, wakati wa kuhutubia Kikao cha 69 cha Kamati Kuu ya Kamishna Kuu ya Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi (UNHCR) tarehe 3 Oktoba 2018 mjini Geneva.

Askofu Mkuu Jurkovič hotuba yake amesema Uwakilishi wa Vatican, unataka kuelezea juu ya ongezeko la mgogoro katika sehemu mbalimbali za ulimwengu  ambazo zimeleta changamoto inayowakilishwa na kipeo cha wakimbizi kuondolewa kwa nguvu  katika sehemu nyingi za dunia. Mnamo mwaka 2017, watu milioni 68.5 walilazimika kuondoka  kwa nguvu duniani kote na miongoni mwao, karibu milioni 25.4 ni wakimbizi.

“Takwimu hizo  ni kiashirio cha kutisha, unyanyasaji na migogoro ambayo inakabiliwa katika umri wetu”, anasema Askofu Mkuu. “Na wakati huo huo, ukarimu na mshikamano wa nchi  ambazo hupokea na kuwakaribisha watu waliohamishwa hutoa vifungo vinavyounganisha familia hizo za kibinadamu”. “Ndugu kaka na dada hawa wakimbizi sio tu kwamba  husambazwa na kupewa mahali pa uwepo, lakini hawa ni watu wenye jina, hadithi, na matarajio halali ya maendeleo ya binadamu”.

Hata hivyo, matatizo mengi yanayokabiliwa na wakimbizi yanabaki bila majibu ya kutosha. Hayo ndiyo mambo ambayo yamepunguza na ngumu, na ni vigumu sana kutekeleza,  hivyo husababisha huzuni na kukatisha tamaa kwa  walio wengi. “Kwa watu walioathirika, hasa wadogo wasiokuwa na wasindikizaji, na familia, kufurahia kamili kwa haki zao za msingi, hubakia kwao kuwa ndiyo shauku na lengo lao. Hali kama hizo ni changamoto katika kuchanua kwa hadhi ya kibinadamu, ambayo ni msingi wa maendeleo ya binadamu”.

Mambo makuu matatu msingi

1.     Uwekezaji elimu kwa watoto wakimbizi

Zaidi ya hayo nusu ya wakimbizi wacko chini ya miaka 18. Kama tunataka kuona kuwa hakuna nayebaki nyuma, ni muhimu kwamba rasilimali ziweze kuwekezwa katika elimu ya watoto wakimbizi. Katika suala hili, ukosefu wa fedha ni chanzo cha wasiwasi mkubwa hasa cha kutoa rasilimali na fedha kwa ajili ya elimu ambapo ndiyo maendeleo ya kibinadamu. Ni muhimu kutekeleza sera ambazo zinawawezesha watoto wakimbizi kupata elimu bora kutoka hatua za mwanzo za makazi yao ili kuwalinda kutokana na usafirishaji haramu wa binadamu, kazi ya kulazimishwa na suruba na aina nyingine za unyonyaji au, hata mbaya zaidi, ile ya kuwafanya watumwa. Shule kweli hutoa ulinzi mkubwa ambapo usalama wa watoto unaweza kufuatiliwa na kukuzwa.

Watoto wa Wakimbizi wanastahili haki ya kuwa watoto. Kama Papa Francisko alivyosema: “hii itawawezesha sio tu kukuza na kutambua uwezo wao, bali pia kuwapa uwezo wa kukutana na wengine na kukuza roho ya mazungumzo badala ya kukataliwa au mapambano”. Zaidi ya hayo, ni muhimu kwamba Uamuzi na wenye msumamo  upatikane  kwa ajili ya  wakimbizi wote wa watoto, lakini hasa watoto wasiosindikizwa na mtu ,na kwa pande zote mbiòi  wakati wa mchakato wa uamuzi wa hali na wakati wa kung’amua ufumbuzi sahihi kwa watoto hao.

2.     Majadiliano ya Global Compact

Majadiliano kuhusiana na Global Compact juu ya Wakimbizi (GCR) yalionesha kuwa jumuiya ya kimataifa inafahamu haja ya njia bora na sahihi zaidi na ya usawa, inayotokana na ushirikiano wa kimataifa na mshikamano. Ushiriki na wengi wa wawakilishi wa vyama vya kiraia ni kiashiria wazi cha kutaka, sio tu kuunga mkono mbinu ya kawaida ya jumuiya ya kimataifa kulenga ulinzi, msaada na kutafuta ufumbuzi wa kudumu, lakini pia kutafuta ufumbuzi  kwa  pamoja kama familia ya ulimwengu wote.

Hata hivyo, maendeleo ya kuhamasisha yaliyotolewa na Global Compact (GCR), tunapaswa pia kuwa wa kweli na thabiti kuhusu utekelezaji wake, kukumbuka kwamba haki za wakimbizi, kama ilivyowekwa katika vyombo mbalimbali vya kimataifa, mara nyingi huendelea kukiuka. Katika suala hili, uwakilishi wa Vatican, Askofu Mkuu Jorkovic anathibitisha, “tunataka kuoneesha michango ambayo viongozi wa dini na mashirika mengi ya ya kidini  yanaweza kutoa wakati wa utekelezaji wa Global Compact (GCR).

3. Kilio cha dunia na kilio cha maskini

Baba Mtakatifu anawatakia mafanikio mema wengi walio katika mazingira magumu. Leo tunapaswa kukiri kwamba mbinu ya kweli ya kiekolojia inakuwa daima mbinu ya kijamii; inapaswa kuingizwa katika mjadala juu ya mazingira, pamoja na kilio cha dunia na kilio cha maskini. Hatimaye, Mwakilishi wa Vatican Jurkovic  anatoa wito wa   kukumbuka kuwa, ni lazima kutafuta   mzizi unaosababisha kuhama  kwa kulazimishwa. Hii inahitaji ujasiri na sera za kisiasa, mapambano ya amani, upatanisho na heshima kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi. Uhamisho wa kulazimishwa sio tu suala la “bahati mbaya”; mara nyingi zaidi kuliko, ni matokeo ya maamuzi ya kisiasa. Na hatimaye, njia kamili na ya  kufikia ufumbuzi wa muda mrefu, na kutambua ndoto ya kila mkimbizi, ni kuhakikisha haki za wote kuishi katika nchi zao za asili, na kustawi kwa heshima, amani, na usalama

04 October 2018, 14:29