Tafuta

Bado ipo kazi ya kusuluhisha migogoro nchini Siria na Iraq Bado ipo kazi ya kusuluhisha migogoro nchini Siria na Iraq  

Vatican: Mkutano juu ya kipeo cha kibinadamu nchini Siria na Iraq

Kila kitu kiko tayari katika Chuo cha Kipapa Urubaniana, kuukaribisha mkutano muhimu juu ya kipeo cha kibadamu nchini Siria na Iraq. Ni mkutano wa siku mbili ya tarehe 13 -14 Septemba, kwa kuhitimisho na kukutana na Papa Francisko.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mshirika 50 yanayojikita katika huduma ya upendo kikatoliki, wawakilishi kutoka mabaraza ya maaskofu mahalia, taasisi za Kanisa na mashirikia ya kidini , wataudhuria mkutano juu ya Tema: Kipeo cha kibinadamu nchini Siria na Iraq, kuanzia tarehe 13 -14 Septamba katika Ukumbi wa Yohane Paulo II katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniano. MKuano huo umeandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo Endeledu fungamani ya binadamu. Katika mkutano huo kutakuwa na mabozi wa Vatican nchini Siria, Iraq na Uruki wakiwa mstari wa kwanza katika kutafuta namna ya kupeleka mshikamano wa papa kwa watu hawa walioangamia kutokana na dhiki ya migogoro.

Lengo la Mkutano huo:  Lengo la Mkutano huo ni kutaka kuona jinsi gani inawezakana kuwa na tafakari ya pamoja kindugu kati ya taasisi zote za Kanisa ambazo zinajikita kutoa huduma ya upendo  kusaidia watu ambao wapo katikati ya kipeo cha kibinadamu,na ambao Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi amekuwa akitoa umakini kwa miito mbalimbali kwa umma, watu wenye mapenzi mema na  jumuiya ya kimataifa.

Ni katika kutafuta mzani wa pamoja wa kazi ambayo imefanyika hadi sasa ya mashirika ya upendo na majibu ya Kanisa: kujadili mapendekezo yaliyojitokeza binafsi na kutoa kipaumbele juu ya wakati endelevu: kutathimini hali halisi ya jumuiya za kikristo zinazoishi katika maeneo ya vita  na ili kuhamasisha mkakati kati ya mashirika ya Kanisa, vyama vya kidini na majimbo. Pamoja na hayo pia ni kutafakari kwa namna ya pekee kwa mwaka huu kwa  kutazama mantiki ya hali halisi ya kurudi makwao kwa watu wengi wa kujitolea wa na kwa  wakimbizi katika jumuiya zao asili.

Kukutana na  Papa Francisko: Tarehe 14 Septemba 2018, majira ya asubuhi, wajumbe wa Mkutano huo wanataungana katika makundi mbalimbali ya kazi na kujikita kutafakarii dhana ya dhati ya kushirikiana kati ya shughuli mbalimbali ya  kwa wahusika wote ili kutoa jibu la kipeo. Mchana watajikita kutazama mada kuhusu wahamiaji na wakimbizi wanaorudi katika nchi zao mahalia. Watakao toa mada watakuwa ni Kardinali Leonardi Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, Padre Fabio Baggio Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya binadamu kwa upande wa Wahamiaji na Wakimbizi. Atakayehitimisha ni Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la maendeleo fungamani ya binadamu, wakati huohuo saa sita mchana masaa ya Ulaya wanatarajia kukutana na Baba Mtakatifu Francisko katika nyumba ya kitume.

12 September 2018, 10:31