Orodha ya watakao shiriki Sinodi XV ya maaskofu kutolewa!
Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Tarehe 15 Septemba 2018, Shirika la Habari Vatican limetoa orodha ya watakao shiriki Sinodi XV ya maaskofu ambayo itaanza mjini Vatican tarehe 3 Oktoba 2018 juu ya mada “ Vijana , imani na maang’amuzi ya miito.
Orodha hiyo inaanza na Papa Francisko, Mwenyekiti wa Sinodi ya Maaskofu, Katibu Mkuu, Kardinali Lorenzo Baldisseri, na wenyeviti wanne wawakilishi: Kardinali, Louis Raphaël I Sako, Patriaki wa Babilonia wa Wakaldayo na Mkuu wa Sinodi ya Kanisa la Wakaldayo (Iraq); Kardinali Desiré Tsarahazana, Askofu Mkuu wa Toamasina (Madagascar); Kardinali Charles Maung Bo, Askofu Mkuu wa Yangon (Myanmar); Kardinali John Ribat, Askofu Mkuu wa Port Moresby (Papua Nuova Guinea).
Orodha inafuata watoa mada wakuu Kardinali Sérgio da Rocha, Askofu Mkuu wa Brasilia na rais wa Baraza la maaskofu wa Brazil, pia Makatibu wawili maalumu: Padre Giacomo Costa, Mkurugenzi wa Gazeti (Aggiornamenti Sociali")Sasisho Kijamii, Rais wa Chama cha Utamaduni cha Matakatifu Fedele na Makamu rais wa Chama cha Carlo Maria Martin, na Padre msalesiani, Rossano Sala, Profesa wa Masuala ya kichungaji ya vijana katika Chuo Kikuu cha Wasalesiani na Mkurugenzi wa Gazeti la "Note di Pastorale Giovanile". Yaani masuala ya kichungaji kwa vijana.
Pia kuna Tume kwa ajili ya mawasiliano akiwa ni Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasialiano, na Katibu wake Padre Antonio Spadaro Mkurugenzi wa Gazeti la Civilta Cattolica. Rais wa Tume kwa ajili ya mijadala Kardinali Giuseppe Versaldi, Rais wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki.
Orodha inaendelea kuonesha, Wajumbe wawili kutoka katika tume hiyo, Askofu Mkuu Charles Jude Scicluna, wa Malta, na Askofu Godfrey Igwebuike Onah, wa jimbo la Nsukka nchini Nigeria.
Baadaye inafuata orodha kamili ya Mapadri wa Sinodi kutoka dunia nzima, walio changuliwa na ofisi, wahudumu, wasikilizaji, wakiwa ni wake kwa waume, washauri, wasaidizi na wajumbe wengine ndugu kutoka Makanisa mbalimbali ya kikristo. Katibu msaidizi wa Sinodi ya maaskofu ni Askofu Fabio Fabene, wajimbo la Montefiascone.