Tafuta

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Paulo Ruffini Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Paulo Ruffini 

Ruffini:Vyombo vya habari Katoliki katika maendeleo ya binadamu!

Katika Ujumbe wake Bwana Rufini kwa Mkutano wa Umoja Waandishi Katoliki Afrika uliofunguliwa tarehe 9- 13 Septemba katika mji wa Cape, nchini Afrika ya Kusini anasema, Mkutano huo unaweza kuwatia moyo na kutoa chachu juu ya msingi ya utamaduni na kama ilivyo hekima ya kizamani ya Afrika, kwa kukabiliana na kushinda changamoto zake

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Utajiri wa Afrika na changamoto zake zinzoikabili  ndiyo imekuwa kitovu cha ujumbe  wa Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Bwana Paulo Ruffini aliotuma katika Mkutano wa Umoja Waandishi Katoliki Afrika uliofunguliwa tarehe 9- 13 Septemba katika mji wa Cape , nchini Afrika ya Kusini. Ni siku tano za Mkutano huo ili kujikita katika kutafakari mada ya matumizi ya vyombo vya habari na kuhamaisha maendeleo fungamani ya binadamu barani Afrika. Katika Ujumbe wake Bwana Rufini anasema: Mkutano huo unaweza kuwatia moyo na kutoa chachu juu ya msingi ya utamaduni na kama ilivyo hekima ya kizamani ya Afrika, kwa kukabiliana na kushinda mfumo usio sawa unaozidi kuuunda na kuongeza umasikini katika bara hilo angavu na siyo tu kwa ngazi ya mali, lakini pia hata katika maadili na kiroho.

Ukuaji wa binadamu kamili:  Bwana Ruffini anasema, kwa miaka mingi sasa , mawazo ya maendeleo yamegeuka kwa urahisi katika masualia ya  kukua kwa uchumi. Kwa bahati nzuri, leo hii jambo msingi linachukuliwa katika ukuu wote wa makuzi katika  binadamu, katika kutambua jambo ambalo wakati mwingine huwezi kulelezea na ambalo ni gumu lenye tabia ya mafundisho ya binadamu, kihisotria, kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa, kiekolojia , kidini na kitasaufi. Jambo la kawaida la ukuaji wa uchumi na maendeleo sasa halikupotea, hata  baada ya jaribio la kushindwa  kupendekeza idhini ya itikadi ya maendeleo katika nchi masikini.  Kwa mtazamo huo, Bwana Paulo Rifini anasisitiza kwamba, njia bora ya kuhamasisha uhuru na kufikia hali bora ya maisha ya kawaida  ni kuunda mfano wake mwenyewe.

Ukuu wa maendeleo na utajiri wa Afrika : Katika dhana nyingi za kiuchumi jamii, zinaonesha jinsi gani uchumi unashindwa kuunda nafasi za ajira na wala kupunguza ukosefu wa uswa, lakini ni kuzidi kuongezea matatizo tu ya binadamu na mazingira. Muunganiko na mambo mengi hayo, kati ya ukuu huo umewekwa hata na Baba Mtakatifu katika Waraka wa Laudato Si, yaani sifa kwa Bwana; na kama Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI katika mahubiri yake ya Misa ya Sinodi Maalum ya Afrika  kwa maaskofu , alikuwa amnezungymza kuwa Afrika ina mapafu mawili tasaufi ya binadamu. Urithi ambao sasa huko hatari ya kuambukizwa na virus vya aina mbili, kwanza ya mali na pili ni dini zinazoibuka”.

Bara la Afrika kwa hakika liko katika mapambano ya kutaka kuwa na  uamuzi wa kuhifadhi urithi wake wa kiroho dhidi ya mashambulizi mbalimbali na uchafuzi wa kuambukizwa. Na kwa njia hiyo Bwana Riffini anatoa wito katika ujumbe wake  akiwaalika wajumbe wote wa Ucap kusoma kwa makini Azimio la pamoja la maaskofu wa Shirikisho la Maaskofu wa Afrika na Madagascar,  azimio ambalo anasema kwa bahati mbaya halikuenea kiasi cha kutosha!

Ushirikiani kama mabalozi wa matumaini: Hatimaye, Bwana Paolo Ruffini anatumaini kuwa ushirikiano utazidi kuongezeka kati ya mambo mbalimbali ambayo yanaelezea upeo huo, kati ya hao ikiwa ni pamoja na, Shirik Katoliki la Kimataifa la Mawasiliano (Signis), Baraza Katoliki la Vyombo vya Habari (Cameco), na vyombo vya habari vya Shirikikisho la Mabaraza Ya maaskofu Katoliki wa Afrika na Madagascar. Akihitimisha amesema "Hatuwezi kamwe kusisitiza vya  kutosha, kwani “ninawakihakikishia ushirikiano wa dhati wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano "juu ya haja ya ushirikiano kati ya wataalamu wa mawasiliano  Katoliki" ili "kutoa sauti kwa wale ambao hawana sauti, kuwaweka wasi wafisadi na wala rushwa na kukataa miundo mibaya ".

10 September 2018, 11:02