Vatican News
Papa Francisko na   Paolo Ruffini,rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Papa Francisko na Paolo Ruffini,rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano  (Vatican Media)

Riffini:Wito wa Papa kuwasiliana ni kuunganisha na si kutenganisha!

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, Bwana Paolo Ruffini, amesisitizia juu ya kauli mbiu ya Siku ya Mawasiliano Duniani ijayo iliyochaguliwa na Papa, “kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine. Kutoka katika jamii hadi Jumuiya”, iliyotangazwa rasmi tarehe 29 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Kuzungumza na mtu mzima ili kuishi ule ukuu wa jumuiya, hata katika kipindi cha Mtandao wa Kijamii”. Ndiyo ujumbe anao usisitiza Bwana Paolo Ruffini Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican akitoa maoni yake na Vatican News na Radio Vatican juu ya kauli mbiu iliyochaguliwa na Papa Francisko kuhisiana na Siku ya Mawasililiano duniani ijayo, ambayo inaongozwa na “kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine (Ef 4,25). Kutoka katika jamii hadi Jumuiya”, iliyotangazwa tarehe 29 Septemba 2018. Katika maoni yake, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anaonesha  umuhimu wa mazungumzo na kukutana kwa ajili ya kushinda vile virus vya mawasiliano ambayo hayaleti tija na kujifungia binafsi, au ambayo huleta mgawanyo badala ya kupatanisha.

Bwana Paolo anathibitisha kuwa, katika kauli mbiu ya Ujumbe Papa kwa Mwaka 2019, ni wazi   kuwa mara nyingi wengi tunapokuwa tunazungumza, na mtu, hatujali kama ni kuzungumza na mtu kamili, bali kwa upende, kutokana na hofu au kulingana na mtazamo wake mwenyewe, wakati huo huo tunasahau kile kinacho tuunganisha na kutushirikisha. Mara nyingi tunatengenisha akili ya moyo na roho, na ndiyo virus hivyo ambavyo Papa Francisko anauita ugonjwa wa moyo, kwa maana moyo unakuwa mgumu. Na hatutambui tena kwa kufikiria kuwalinda wengine, kwa hofu ya kuwa tumeambukizwa, vinagawanya sisi wenyewe na kupoteza au kuwa na hatari ya kupoteza sehemu nzuri zaidi ya uasili wetu, ambao unamwilishwa na uzuri wa kukutana, kujadiliana ,kutengeneza mahusiano, kushirikishana , kuwa na muungano kati yetu na pia Mungu.

Akifafanua juu ya hatari za kujufungia binafsi

Bwana Paulo anasema hatari ya wakati wetu ni ile ya kujenga ukabilia badala ya jumuiya. Na hilo ni kabila lenye msingi wa kubagua mwingine, kwa maana hiyo inahitaji kuingilia kwa haraka, juu ya tabia hiyo katika tazamo wetu, upendo wetu  binafsi, na ule unaoigawa dunia sehemu mbili.  Hiyo inazuia kutazama ndugu mwingine kwamba ni mwana wa Mungu na Mungu mwenyewe. Inahitaji kuondoa tabia hiyo na kurudia kuhisi jambo moja, kama asemavyo Mtakatifu Paulo, “watu wa jumuiya moja"  na jamii.

Kadhalika Bwana Paulo anasema kuwa, katika mitando ya kijamii imebadilisha jamii katika mawasiliano kwenye jamii ya mjadala. Ni sehemu ambamo wanaunda utambulisho wetu hasa kwa upande wa vijana. Mazungumzo yanaweza kutengeneza uhusiano wa kweli, uzuri na udhati. Lakini pia unaweza kueneza hata chuki na mifumo ya uadui , hasa inapotokea kwamba hakuna mahusiano ya kweli; kadhalika hatari ni ile ya kuangukia nyuma kwa kufikiri ni kwenda mbele. Uwepo wa Papa Francisko katika mitandao ya kijamii unatoa mtazamo chanya , kwa namna ya kutazama upeo. Kwa namna nyingine, unaweza kusema ni kama vile kuunganisha mzizi wa kifransiskani na Utume wa Papa. Kuwapo katika mtandao ni kutoa maana iliyo bora zaidi.

Sio kitu ambacho kinakufanya  kama  kuingia kwenye mitego, lakini ni  kitu kinacho kuachilia, na kinatufanya tuwe chombo uhuru! Muungano ni dawa bora dhidi ya mambo yaliyo ya uongo. Hata hivyo Bwana Paulo amekumbuka Sala ya rahisi ya Mtakatifu Francisko wa Assisi isema : “Bwana, nifanye chombo  cha amani yako; mahali palipo na chuki ni nilete upendo; mahali palipo na makosa, ninaleta msamaha”.

Na mwisho amegusia juu ya vijana mbao Sinodi ya Maaskofu inakaribia kuanza na ambayo ni muhumu katika jumuiya, hata katika mitandao ya kijamii, Bwana Ruffini  amethibitisha kuwa: Vijana wanatafuta jamuiya kwa sababu bado hawajapoteza ile haja ya mahusiano; ya mikutano na mazungumzo. Mioyo yao bado siyo migumu. Mtandao unaotafuta ni wa watu, si wa waya tu, kama Papa Francisko alivyosema. Lakini kama mtandao wanaoupata una upendeleo wa mitando ambayo ni huru, na ikiwa vijana wanajikuta katika jamii inayosimamia misingi ya wivu, hasira, basi sisi tuko tunawaharibi vijan na wakati wetu endelevu. Kwa maana hiyo: Jumuiya kwenye mitandao ya kijamii inapaswa kuingiliana na uhusiano wa dhati, na wa kweli, kati ya watu ambao wote hata kama wameishi katika hali isiyo ya kawaida ya kidigital, ambayo lakini  kwa hali yoyote ni ya kweli na si ile ya kimitandao.

Kwa njia hiyo Bwana Ruffini  anathibitisha kuwa, ndiyo maana ni muhimu kuhama  kutoka katika jamii iliyoundwa juu mahusiano  bandia, juu ya uongo unaowakilishwa na hali halisi, kwa urafiki bandia ambao unaweza kufutwa kwa kubonyeza (Clic), ili kuingia katika uzuri hata pia ugumu wa ukweli na kukutana. Umoja ni mlinzi bora wa ukweki. Vijana wanatafuta uhuru. Lakini ni ukweli tu hutufanya huru.

 

 

29 September 2018, 15:23