Tafuta

Rais  Filipe Jacitno Nyusi, wa  Msumbiji akiwa Studi za Vatican News Rais Filipe Jacitno Nyusi, wa Msumbiji akiwa Studi za Vatican News 

Rais Nyusi wa Msumbiji:Upo uhusiano mwema kati nchi na Vatican!

Rais wa Jamhuri ya nchi ya Msumbiji Bwana Filipe Jacitno Nyusi katika mahojiano na Vatican News, ameelezea juu ya uhusiano mwema uliopo baina ya nchi yake na Vatican, mkutano na Baba Mtakatifu Francisko, masuala ya uchumi, siasa, kilimo ya nchi yake, na pia tathmini ya utawala wake kwa kipindi cha miaka 3 sasa ya utawala

“Imekuwa muhimu sana kuwapo hapa na kuzungumza na Papa juu ya masuala ya mapatano na maelewano kati ya makanisa na baina ya kanda. Kwa upande wetu imekuwa muhimu kuongelea juu ya nchi yetu katika mambo ya kisiasa, kijami, kichumi, hata kusikiliza ushauri kwa maana mbali na hapo, ushauri wa Baba Mtakatifu daima unaongeza zaidi, kwa maana Yeye  anasikiliza maoni ya mamilioni ya akili za watu na mamilioni ya wazalendo wa dunia hii. Haya ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya nchi ya Msumbiji Bwana Filipe Jacinto Nyusi katika mahojiano na Padre Bernardo Suate  wa Vatican News, tarehe 14 Septemba 2018 katika lugha ya kireno.

Wakati wa mahojiano na Padre Berdardo Suate, Rais wa Msumbiji ameanza kwa kushukuru kwa ajili ya fursa aliopewa kuzungumza, kwa njia ya  Vatican News  katika dunia na kwa namna ya pekee kwa wazalendo wa Musumbiji. Baadaye amesema kuwa mkutano wake na Baba Mtakatifu , umewakilisha  zawadi kubwa ambayo hata yeye alikuwa amewaalika daima  “kuacha kile kinachotengenisha na kubaki na kile kinachounganisha.”

Mchakato wa amani Msumbiji: Kile ambacho kinapeleka kwa namna ya pekee ya mabadiliko ya Katiba ya nchi, na hasa kwa upande unaotazama amani ya dhati, na ya kudumu kwa nchi ya Msumbiji, Rais, amesema hiyo inategemea na maoni ya sehemu ya mwingine. Akifafanua juu ya kuheshimiana, serikali na Renamo (chama cha upinzani cha Kitaifa Msumbiji),  na kwamba, wamefika katika pakiti mpya ya ugawaji wa madaraka ambayo imeunganishwa katika sheria mpya ya uchaguzi.

Na katika swali kuhusu maendeleo ya mchakato wa amani, Rais wa Msumbiji alijibu kuwa "sasa tuko katika awamu ya kusitisha  silaha, kuhamasisha na kufungamanisha tena kwa watu wenye silaha wa Renamo. Na hiyo itatupeleka  na kutuongoza kwenye amani yenye ufanisi na ya kudumu mahali ambapo sisi sote tutakuwa sawa" amethibitisha Rais wa  Msumbiji.

Mchango wa kanisa Katoliki: Akizungumza juu ya mkataba wa nchi mbili kati ya Vatican na Msumbiji, makubaliano juu ya kanuni na masharti ya kisheria ya mahusiano kati ya Jamhuri ya Msumbiji na Vatican wakati yalitiwa saini kunako 2011, Rais Nyusi amesema kuwa hapakuwa na matatizo.

Kuna njia ya moja kwa moja inayo ongozwa na Balozi mwakilishi wa Papa. "Ushiriki wa mwakilishi wa Papa katika mchakato wa mazungumzo katika mzunguko wangu wa kwanza ulikuwa wazi kwamba Kanisa Katoliki linataka kuwa sehemu ya suluhisho la tatizo hilo" na kuhimtimsha  kwamba,  mahusiano kati ya Vatican na Msumbiji yalikuwa mazuri, na pia ziara yake  ya Vatican.

Migogoro ya ya ardhi: Wasiwasi uliojieleza  wa migogoro ya ardhi ambao ulikuwa katika Barua ya  kichungaji ya Maaskofu wa Msumbiji ya mwezi Aprili mwaka huu , Rais wa Msumbiji anathibitisha kuwa, serikali haijawahi kamwe kuuza ardhi . Na ili kuweza kuridhika na haki za wazalendo,  Mtendaji amezindua mpango  wa "ardhi salama" ambayo inasema  kuna usambazaji wa haki” (DUAT) utumiaji wa ardhi na utumiaji wa eneo). Lakini hata hivyo amesema,  maendeleo ya nchi hayapaswi kuachwa kando. Na mwisho wa  mahojiano hayo katika lugha ya kireno amesema alikuwa anatarajia kumwalika Baba Mtakatifu Francisko kutembelea Msubiji mwaka kesho.

 

Rais Nyusi wa Msumbiji katika Lugha ya Kiswahili aeleza mafanikio ya hawamu yake: Mara baada ya kusungumza lugha ya kireno, Rais Nyusi kwa dakika chache ameweze kuzungumza katika lugha ya kiswahili kwa kujibu  Sr. Angela Rwezaula kuhusu ni tathimini ipi anayo itoa mara baada ya miaka mitatu tangu achaguliwe kutokana na kwamba, mwaka 2015 wakati wa kampeni ya uchaguzi alihaidi wazalendo, kuinua uchumi ili wapate kuwa na maisha bora. Yeye anathibitisha hadi sasa tayari wameanza kusambaza umeme karibu kila vijiji, na masuala mengi ya kijamii. Lakini yote hayo ni kwa taratibu, kutokana na nchi alivyo ikuta, lakini maendeleo yapo na wanajitahidi kadiri wawezavyo. 

sikiliza sauti 

Ikumbukwe alipochaguliwa mwaka 2015, Nyusi alipata asilimia 57 ya kura zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake wa karibu Afonso Dhlakama, kiongozi wa chama cha upinzani cha National Resistance (Renamo). Na Dhlakama alipata 37% ya kura zilizopigwa. Renamo  ni chama  ambacho walipigana vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Frelimo ambavyo vilifikia kikomo 1992 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja walikuwa  wamepinga matokeo hayo. Hata hivyo kama Rais alivyosema, nchi inajitahidi kadiri ya uwezo wake kuinuka taratibu lakini yote hayo yanahitaji umoja na ushirikiano, mazungumzo na makubaliano kwa pande zote mbili ili kweli kufikia mchakato wa amani ya kudumu

17 September 2018, 09:37