Wanafamilia katika hija ya kitaifa huko Pompei katika Madhabahu ya Mama Maria wa Rosari Wanafamilia katika hija ya kitaifa huko Pompei katika Madhabahu ya Mama Maria wa Rosari 

Papa: Kila nyumba igeuke kuwa shule ya Injili!

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa washiriki wa Hija ya Familia Kitaifa huko Pompei, anasisitiza kuwa “ushuhuda ambao dunia leo hii ina haja kubwa, ni kuona familia hai, familia inayoishi,na ndiyo maombi yake ili awasikie wakitamka katika muungano huo wa maombi kati ya wazazi na watoto , babu na bibi na washiriki wote wa tukio muhimu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Kufuata wazo la utakatifu wa familia”, ndiyo ujumbe msingi  wa Papa Francisko iliotiwa saini na Kardinali Pietro  ambao kwa Washiriki wa Hija ya XI ya familia kwa ajili ya Familia , ambao wamefanya hija hiyo tarehe 15 Septamba 2018, kati ya Scafati na Pompei  huko Napoli Italia. Ni hija   kwa mwaliko wa Chama cha Uuisho wa Roho Mtakatifu, kwa ushirikiano wa Madhabahu ya mama Maria ya Pompei, Ofisi ya Kichungaji kwa ajili ya Familia ya Baraza la Maaskofu wa Italia, Jukwaa la Vyama vya Familia kitaifa, ikiwa pia ni pamoja na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Hija hii ya familia imefanyika chini ya mtazamo wa Bikira Maria wa Rosari, ambapo wote wamejikita kusal Rosari ya Familia ambayo na kutafakari mafumbo saba ya mateso ya Mama Maria.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, anasisitiza kuwa “ushuhuda ambao dunia leo hii ina haja kubwa, ni  kuona familia hai, familia inayoishi,na ndiyo kilio ch Papa Francisko akiomba asikie wakitamka katika muungano huo wa maombi kati ya wazazi na watoto , babu  na bibi na washiriki wote wa tukio hilo ambalo, ni kama mwendelezo wa mawazo ya Mkutano wa IX wa Familia duniani ambao umemalizika hivi karibuni mjini Dublin Ireland.

Kuwa makini juu ya mstari wa mbele wa familia: Kila kitu kinageuka kuwa Injili ya familia, shule ya uaminifu, na uwazi, ya amani na msamaha, ya kusikiliza na mapatano, ya umoja na mshikimano. Hata hivyp Papa Francisko ameatakia hija hiyo iweza kuwa na umakini juu ya kuwa msatari wa mbele katika Kanisa, jaminii ya familia kwa namna ya kuhamasisha zaidi katika ulimwengu, ule utamaduni wa maisha  wa mtu katika hadhi yake yote fungamani na ukuu wake.

Umakini wa familia dhaifu:  Kutokana na hili, pia amewaalika  kuwasindikiza familia ambazo ni dhaifu  na wale ambao wanaishi kipeo cha talaka, wasio kuwa na ajira au kwa namna moja wamepoteza na wengine kulazimika kuhama kwa kulazimisha kutokana na majanga , mateso na migogoro mingi au vifo. Lakini pamoja na hayo anaomba wasisahau hatafamilia za wenye ndoa vijana au wazee, wachumba na wajane.

Hija chini ya mtazama wa Mama Maria: Wengi wamejikuta wako Scafati kwa ajili ya kuadhimisha uzuri wa familia kikristo, kwa muziki, nyimbo na ushuhuda wa familia nyingi. Kadhalika hata hotuba mbalimbali zilizotolewa na  baadhi ya waalikwa kama vile, Askofu Giovanni D’Ercole na Askofu Francisko Marino, Marais wa Huisho wa Roho Mtakatifu, Salvatore Martinez na wa Jukwaa la Familia Bwana Gigi De Palo, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kichungaji kwa ajili ya Familia ya Baraza la Maaskofu wa Italia Padre Paolo Gentili.

Sala ya kujikabidhi kwa Mama Maria: Mahujaji wote kwa pamoja wakisali Rosari walitembea hadi Pompei mahali ambapo waliokelewa na Askofu Tommaso Caputo wa Madhabahu kwa mama Maria wa Rosari Pompei. Baada ya kusali sala ya kujiweka wakfu kwa Mama Maria familia, vijana na watoto ikiwa katika fursa pia ya ufunguzi wa Mwaka mpya wa masomo, wameshiriki hitimisho la  Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali  Crescenzio Pepe,  Askofu Mkuu wa Jiji la  Napoli Italia

18 September 2018, 15:23