Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na  Paul David Hewson mjini Vatican Baba Mtakatifu amekutana na Paul David Hewson mjini Vatican  (Vatican Media)

Papa Francisko ni mtu wa ajabu kwa nyakati hizi za kiajabu!

Tarehe 19 Septemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta amekutana na msanii Paul David Hewson katika usanii wa Bono Vox: Kikundi cha wanamuziki frontman kutoka Ireland na ameeleza juu ya msaada wa utume wa elimu ya Chama cha Kipapa cha Scholas Occurrentes,katika kusaidia mafunzo na maendeleo ya watoto na vijana duniani kote

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 19 Septemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta amekutana na wasanii Paul David Hewson  katika usanii wa Bono Vox: Kikundi cha wanamuziki frontman kutoka Ireland na  ameeleza juu ya msaada wa utume wa elimu ya Chama cha Kipapa cha Scholas Occurrentes, kinacho jihusisha na mafunzo na maendeleo ya watoto na vijana duniani kote.

Mkutano huo ni kama kupigwa na radi

Mwanamuziki Paul David Hewson  amefafanua kuwa, mkutano na Papa Francisko ni kama vile amepigwa radi, kwa maana ya mazungumzo yao yalikuwa ya asikivu na mwendelezo uliowagusa kwa mada kubwa za nyakati hizi, kama vile elimu kwa vijana, hasa wasichana ambao katika nchi nyingi za dunia wanateseka kwa kubaguliwa na kuwekwa pembezoni.

Uchungu wa Papa

Mara baada ya mkutano wa Papa waandishi wa habari katika ofisi za habari Vatican wamekutana na wasanii hao ambao pia wanathibitisha juu ya mkutano wao uliojikita katika masuala mbalimbali  yakiwemo hata masuala ya manyanyaso ya watoto  kwa njia ya wahusika kwa Kanisa, ambapo  Mkurugenzi wa Kimataifa  wa Chama cha Scholas, José María del Corral, ametoa utangulizi mfupi na kuonesha baadhi ya mantiki ya Baba Mtakatifu Francisko na mwanamuziki hao, lakini hata hivyo amesema kuwa ameona uchungu katika uso Papa wakati wa kugusia masuala ya manyanyaso. Pamoja na hayo msanii Bono Vox ameshirikisha historia yake kama mwanamuziki wa dunia na marufu, ambaye anathibitisha kwamba, yeye hakukosa kukumbana na matatizo na vizingiti katika shughuli yake ya kisanii.

Ni papa wa maajabu

Katika kuendeleza na Mazungumzo hayo, mwanamzuki Paul David Hewson  amethibitisha juu ya msaada wao kwa Chama cha Scholas, na mipango yake ya kiubunifu, katika utume wake mkubwa wa kuanzisha mapinduzi ya elimu, na ili vijana wagundue maana ya maisha.

Kwa pamoja pia katika Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko wamezungumzia hata juu ya utunzaji bora wa Nyumba yetu ya pamoja katika Waraka wake wa “Laudato Si “yaani Sifa kwa Bwana. Na kwa maana hiyo  kabla ya kuacha ofisi ya habari Vatican Bono Vox amethibitisha kuwa Papa ni mtu wa ajabu katika nyakati hizi za kiajabu!, na baadaye katika vichekesho ameongeza kusema , wakati huu sitoweza kufanya tamasha!

20 September 2018, 13:34