Vatican News
Wanafunzi nchini Angola Wanafunzi nchini Angola 

Papa amepokea utambulisho wa Balozi mpya wa Angola P.Baptista

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 7 Septemba 2018 amepokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Angola Bwana Paulino DOMINGOS BAPTISTA anayewakilisha nchi yake mjini Vatican.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 7 Septemba 2018 amepokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Angola Bwana Paulino DOMINGOS BAPTISTA anayewakilisha nchi yake mjini Vatican.

Bwana Paulino DOMINGOS BAPTISTA alizaliwa kuna tarehe 8 Julai 1951 huko Luanda na ni baba wa familia na watoto wanne.

Katika maisha ya kitaaluma na nafasi ya uongozi: Anayo shahada uzamivu wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Agostino huko Neto mwaka 1988.  Zaidi ameweza kushika hata nafasi mbalimbali kama vile Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya ndani katika Wilaya ya Cunene, Huila na Luanda (1976-1990). Mkurugenzi wa Taifa wa Utalii  mwaka 1990

-Makamu Waziri wa Serikali na  Waziri wa mambo ya ndani na Utalii (1991-2016). Waziri wa Utalii (2016-2017). Ujuzi kuzungumza lugha ya Kireno, kihispania na kingereza.

07 September 2018, 16:58