Cerca

Vatican News
Baraza wa Makardinali washauri wa Papa Baraza wa Makardinali washauri wa Papa 

Mkutano wa Baraza la Washauri wa Papa Mjini Vatican

Mkutano wa XXVI wa Baraza la Ushauri la Makardinali wa Papa ulioanza Septemba 10 utamalizika 12 Septamba 2018 ambapo shughuli yao inaongozwa na Papa mwenyewe. Washauri Makardinali wanamsiadia Papa Francisko katika shughuli yake ya uongozi na hata katika mchakato wa mageuzi Vatican

Tarehe 10 Septemba mjini Vatican, unafanyika Mkutano wa Baraza la washauri wa Papa akiwemo hata Baba Mtakatifu Francisko. Huo ni mkutano wa XXVI wa Baraza la Ushauri la Makardinali ambapo Baraza hili litiendelea na shughuli yake hadi Jumatano 12 Septamba 2018. Baraza la Ushauri la Makardinali ambalo linaitwa C9 liliundwa kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko ili kushirikiana katika majukumu ya huduma ya Kanisa na ushirikiano kwa ajili ya  mageuzi ya Vatican. Shughuli yao inaongozwa na Papa mwenyewe. Ni Kikako cha XXVI tangu kuanza kwake kunako tarehe 1-3 Oktoba 2013 wakati huo Baraza la kikao cha mwisho kukaa kilikuwa ni  tarehe za 11-13 Juni 2018.

Tamko la Baraza la Makardinali.

Katika Kikao cha Baraza la Makardianali (C9) sehemu ya kwanza  , wamekijita kukabidhi Baba Mtakatifu mapendekezo karibia ya mageuzi ya Vatican ambayo yamefanyiwa kazi kwa miaka mitano ya kwanza ya shughuli, kwa mtazamo huo, wamemkabidhi Papa tafakari ya kina juu ya kazi, muundo na mpangilio wa Baraza hilo kwa kuzingatia pia umri wa baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho.

Naye Baba Mtakatifu ameelezea juu ya kupendezwa na ufanisi mzuri wa Mkutano wa IX wa Familia Duniani uliofanyika mjini Dublin na kumpongeza pia Kardinali Kevin Joseph Farrell na Baraza lote la Kipapa kwa ajili ya Walei,Familia na maisha ,ambao pamoja na Askofu Mkuu Diarmuid Martin, wa Jimbo Kuu la Dublin waliandaa tukio hilo.

Aidha Makardinali hao, wameonesha mshikamano wa dhati kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa kile kilichotukia katika wiki za mwisho kwa utambuzi ya kwamba majadiliano ya sasa ya Vatican yanatafuta namna ya kupata mwafaka na ulazima wa kuweka masuala yote bayana.

 

 

11 September 2018, 13:37