Cerca

Vatican News
Papa akiwa na washiriki wa Mkutano juu ya chuki na ubaguzi wa rangi Papa akiwa na washiriki wa Mkutano juu ya chuki na ubaguzi wa rangi  (ANSA)

Makanisa katika kupambana dhidi ya chuki na ubaguzi wa rangi!

Makanisa yako mstari wa mbele kupambana na ubaguzi wa wageni na wa rangi. Ndiyo ujumbe unaojitokeza katika hitimisho la Mkutano wa Kimatafia kuhusu mada ya “Chuki dhidi ya wageni, ubaguzi, ustaarabu wa kitaifa dhana ya mazingira ya uhamiaji wa kimataifa ”, mkutano uliohitimisha tarehe 20 Septemba 2018

Katika ujumbe wa Mwisho wa mkutano wa Kimataifa kuhusu mada ya Chuki dhidi ya wageni,ubaguzi, ustaarabu wa kitaifa dhana ya  mazingira ya uhamiaji wa kimataifa”, uliohitimisha tarehe 20 Septemba 2018,washiriki wa Mkutano wanathibitisha kuwa msingi wa pamoja katika tafakari yao, ni makubaliano ya pamoja ya kuwa kila kiumbe ni sawa katika hadhi, haki na hata vipimo ambayo vinapaswa kuwa katika kuheshimu na kulindwa.  Kwa hakika uhamiaji ni suala linalowagusa wote, ni tabia ambayo inaygusa kila ahali ya maisha. Hiyo ni kutokana na kuwamba imethibitishwa katika hatua ya kihistoria, hata leo hii kwa bahati mbaya, kwasababu ya vita, umaskini wa kukithiri, ukosefu wa chakula, pia fursa za maisha. Kutokana na hiyo,wawakilishi kutoka Makanisa ya kikristo, wakubaliana kuwepo na  katiba ya kuomba hifadhi kwa ajili ya wale wanaokimbia migogoro ya silaha na mateso au na majanga ya asili.

Chuki dhidi ya wageni: mashaka ya kupotea binafsi

Chuki dhidi ya wageni ni hofu ya kuogopa mgeni, hofu ambayo inajionesha katika masuala ya kutaka kumbagua mti  na hata kufikia hatua ya kumchukia mbele yako. Hata hivyo hofu hiyo daima inajitokeza kwa mtindo wa mashaka , ambayo yanatazama mashaka ya kupotea binafsi, utambulisho binafsi, usalama, kushikilia mali  na kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha za wakati ujao. Mgeni badala yake ni tofauti na hayo kwa maana yeye anaogopa tendo la kuwekwa  katika mjadala binafsi n aule wa pamoja kutokana na wakati wake endelevu.

Ubaguzi wa rangi: dhambi juu ya ujenzi wa jamii

Katika ujumbe wao pia  wanaandika kuwa ubaguzi ni ujenzi kijamii ambao unadai kuelezea na  kutengenisha katika makundi ya kibinadamu kwa msingi ya kimantiki ya kimwili, kijamii, kiutamaduni na dini. Kutoka katika ujenzi huo unaotokana na tabia ya ubaguzi wa rangi ambao unatengenisha watu, mmoja kwa mwingine kwa kuweka jina la uongo, hata kuwapa jina maalum katika jumuiya fulani. Kwa njia ya ubaguzi wa rangi, unaunda na kuhifadhi wale waathirika katika makundi na kuwaondolea haki za msingi katika kuishi  na kutafuta sababu za kuwa ni wasumbufu.  Kwa maana hiyo ubaguzi wa rangi ni dhambi, katika kielelezo binafsi ambacho katika mfumo wa mzizi hauendani kabisa na dhana ya mkristo.

Wito kwa makanisa

Kukaribisha ni wajibu,kwa waamini wote kupokea wageni, ni tendo la upendo linalojikita katika imani. Kwa maana hiyo Makanisa yote yanaalikwa kuwa sehemu ya  kufanya uzoefu na kujifunza kuheshimu utofauti na kufurahia  fursa ya kukutana kwa pamoja ambao ni utajiri mkubwa. Katika hitimisho la ujumbe huo: Makanisa ni wadau muhimu wa jamii ya raia na maisha ya kisaisa, na kwa maana hiyo“ tunawashauri washiriki kuwa na kushirikiano wa nguvu na wadau wengine wa dini, maisha ya kisiasa , kiuchumi na kijamii, katika kulinda sayari ambayo ni nyumba yetu ya pamoja.

21 September 2018, 10:30