Kardinali Fernando Filoni, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu Kardinali Fernando Filoni, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu 

Mafundisho na uzoefu kwa maaskofu wa maeneo ya kimisionari

Semina kwa ajili ya Maaskofu wa maeneo ya kimisionari ambao wamepata daraja la uaskofu kwa miaka ya hivi karibuni imeandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu kuanzia tarehe 3- 25 Septemba 2018. Semina hii inawaunganisha maaskofu 75 kutoka mabara manne, ambako katika siku hizi wataishi uzoefu wa kujifunza na kushirikishana

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mahojiano na Kardinali Fernando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, amejikita kueleza juu ya mada na lengo la Semina ya mafunzo kwa maaskofu waliotangazwa miaka ya hivi karibuni katika maeneo ya kimisionari. Ni  Semina iliyo andaliwa na Baraza la Uinjilishaji wa watu, ikiwa inataka kutazama kwa kina mada ya kutafakari huduma ya uaskofu, kujifunza katika  uhusiano juu ya mantiki tofauti za Kanisa, kutambua vema  Baraza Kuu la Roma na kubadilishana uzoefu wao binafsi katika maeneo yao ya utume.

Hii ni fursa ya mafunzo na kushirikishana kwa maaskofu wapya 75 walioteuliwa kwa miaka miwili ya hivi karibuni, ili kupta kuongoza maeneo yao mahalia ya Kanisa katika ulimwengu wa kimisionari. Na hiyo ndiyo lengo la Semina hiyo ya mafunzo ambayo yamefunguliwa Mjini Roma tangu tarehe 3 Septemba katika Taasisi ya Kipapa ya Mtakatifu Paulo Mtume. Maaskofu hawa wanatoka katika mabara manne ya Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Australia.

Siku ya mafunzo yao itamalizika Jumamosi tarehe 15 Septemba 2018, ambapo semina hiyo imegawanyika katika vipengele tofauti kama vile sehemu ya sala na mada ambayo baadaye inafuata majadiliano na kazi katika makundi kulingana na lugha zao kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Shirika la habari za kimisionari Fides.

Mafunzo mbalimbali

Tukio hili litajikita juu ya mada mbalimbali zenye uhusiano na Kanisa. Kwa maana hiyo atakayetoa neno ni Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishi wa Watu Askofu Mkuu Protace Rugamba, Katibu msaidizi na Rais wa Baraza la Kipapa la matendo ya Kimisionari, Askofu Giovanni Pietro Dal Toso na makardinali wengine wa Vatican ambao watajikita katika mada zinazohusiana na Mabaraza ya Kipapa  ambayo wanaongoza na kuhudumia. Pia maskofu wakuu na maaskofu kama Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican, na  Askofu Juan Ignacio Arrieta, mmoja kati ya watano wa Tume ya kipapa kwa ajili ya Taasisi za shughuli za dini.

Hata hivyo pia anatarajiwa monsinyo Dario Edoardo Vigano kuzungumza  juu ya matumizi ya vyombo vya mawasiliano katika uinjilishaji,na Padre Hans Zollner, juu ya ulinzi wa watoto na watu wazima waathirika, na hatimaye Askofu Mkuu Guido Marini kuhusu liturujia na utakatifu katika Kanisa. Ni fursa ya kujifunza na kutambua vema Baraza la Kanisa la Roma

Aliyefungua shughuli ya mafunzo hayo tarehe 3 Septemba 2018, ni Karidnli Ferdinando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, ambaye amezungumza na Vatican news kwa kuelezea kwa ufasa juu  ya lengo la Semina hiyo kwamba, kwa kawadia Baraza la Kipapa kila baada ya miaka miwili, wanaandaa semina ya kusasisha  na mafuzno ya maaskofu wapya: Hawa ni maaskofu Makanisa vojana , katika maeneo ya kimisionar , ofisi za kitume na kwa maana hiyo shughuli hii inaingia moja kwa moja katika hdumam ambayo Baraza hili linakita katika maeneo yao.

Maaskofu hawa pia ni fursa yao ya kujua zaidi maeneo ya Baraza kuu Vatican , maeneo ambayo Baba Mtakatifu anafanyia huduma yake ya kichungaji. Kwa  njia ya zana walizo nazo Roma, watu maalum wenye taaluma, ambao watawasaidia ili kutoa uwezekano wa kufanya mijadala , kusikiliza na kuwa na uwezo wa kutambua hali halisi kwa ujumla ya uendeshaji wa jimbo na Kanisa zima. Na zaidi ni fursa yao ya kuwa na  umoja kati yao.

Kadhalika Kardinali anafafanua kwamba semina hiyo ni kutaka kuonesha juu ya mchango mkubwa kwa watu  wa Mabaraza ya Kipapa ambao wanao utoa kaika utaalam, au ni wahusika wa sekta maalum.  Sekta hizi ni zile zinazotazama hata Kanisa mahalia za kimisionari ulimwenguni. Kwa maana hiyo pamoja na sehemu ya kwanza ya utangulizi juu ya mada yenyewe, inatazama pia mazungumzo ambayo maaskofu wanaweza kupata maswali ambayo kidogo ni maalum katika kujitajirisha zaidi na mafunzo hayo.

Pamoja na hayowanazingatia kwamba na maaskofu wanatoka kati maeneo yao na watenda shughuli yao kama maaskofu na siyo wageni wa hali halisi ya Kanisa. Kwa ujumla wote ni wazaliwa au wanafanya kazi huko kwa miaka mingi katika maeneo hayo. Katika miaka miwili ya kwanza tangu kuteuliwa kwao, wakiwa na uzoefu wa maeneo yao, wanaweza kweli kubadilishana kwa pamoja na kuchangia uzoefu ambao wanafanya. Kwa maana hiyo kama upo utofauti, hii inakuwa ni fursa ya kujitajirisha zaidi na kuwa bora katika mazunguzo kwa wote. Kujua uzoefu wa wengine, kwa hakika inasaidia hata maaskofu wa majimbo mengi au kufanana au utofauti lakini wakati huohuo wapo wote.

04 September 2018, 12:23