Kardinali Pietro Parolin  huko Chisinau nchini Moldovia Kardinali Pietro Parolin huko Chisinau nchini Moldovia 

Kard Parolin: Familia ya kikristo kupambana na ubinafsi!

Katika hotuba yake Kardinali Parolin Jamamosi 15 Septemba 2018, huko Chisinau, nchini Moldavia alianza na maneno ya jambo moja alilifanya Mungu lilikuwa familia. Hayo aliyochota kutoka katika maneno ya Papa Francisko wakati wa mkesha wa maombi kwa ajili ya familia huko Philadelfia 2015

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

“Jambo zuri alilofanya Mungu, Biblia inasema kuwa, ilikuwa ni familia. Kwa maana hiyo aliumba mme na mke na kuwapatia kila kitu. Aliwakabidhi dunia na kusema, zaeni mkaongezeka na kuijaza dunia kulima ardhi na mfanuye izae matunda”. Ndiyo maneno aliyoanza nayo Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika Kongamano la Familia la duniani huko Chisinau, nchini Moldavia ambalo lilianza tarehe 13-16 Septemba.

Katika hotuba yake Kardinali Parolin Jamamosi 15 Septemba 2018, huko Chisinau, nchini Moldavia alianza na maneno hayo aliyochota kutoka katika maneno ya Papa Francisko wakati wa mkesha wa maombi kwa ajili ya familia huko Philadelfia 2015. Na ndiyo ilikuwa mapendekezo ya tafakari yake kuhusu uzuri wa familia na ujazo mkubwa wa kazi ya uumbaji.

Familia ni taa ya matumaini

Akiendelea na hotuba yake ameonesha uzoefu wa mwisho wa Mkutano wa mwisho wa Familia duniani ambao umefanyika hivi karibuni mjini Dublin Ireland na kusema: “kwa mtazamo wa ushuhuda ambao kwa wengi waliwakilisha na kwa namna ya pekee wenye msingi umeweza kuelekeza kwa namna ya dhati ule uzuri wa maalum wa upendo wa familia ya wanandoa na kwamba, familia ni mapango mzima wa wokovu wa Mungu”.

Nafasi ya famimilia

Na nafasi ya familia ambayo inapaswa kujikita hasa katika kipindi hiki cha udhaifu katika mahusiano ya kibadamu; familia hawali ya yote, asili yake ni Mungu na ambayo utume wake wa kwanza ni upendo ambao unaweza kuendelea kuitwa taa ya matumaini inayochomoza katika dunia. Ukweli wa ndoa na familia ni wa kudumu. Na ni hai kwa umuhimu wake ambao unaendelea kutangazwa kwa ukamilifu wake na ushirikishwaji wake.

Familia ni shule ya kwanza ya ubiandamu

Kwa mujibu wa Kardinali Parolin pia anasema, familia kwa dhati ni shule mahali ambamo tunajifunza maana ya kuishi ubinandamu. Upo utambuzi wa kujua familia nyingi zenye watoto wangi na thamani ya kikristo ambayo ni hekima na nguvu kwa ajili ya jamii na ugumu wake.

17 September 2018, 15:26