Maadhimisho ya liturujia ya  Papa Francisko kwa mwezi Septemba na Oktoba 2018 Maadhimisho ya liturujia ya Papa Francisko kwa mwezi Septemba na Oktoba 2018 

Kalenda ya maadhimisho ya Papa kwa mwezi Septemba na Oktoba

Tarehe 4 Septemba 2018 imetolewa kalenda ya ratiba ya maadhimisho ya kiliturujia ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi Septemba na Oktoba 2018. Katika miezi hii kuna Sinodi, kutangaza watakatifu na ziara yake ya kitume huko Palermo, Sicilia na nchi za kibaltiki

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Sinodi ya Maaskofu, kutangazwa watakatifu ambapo kati ya saba yupo  Mwenyeheri Papa Paulo VI na Askofu Romero , ikiwa pamoja na ziara ya kimataifa ni mambo matatu msingi yanayotarajiwa kutendeka ya Papa Francisko katika mwezi wa Septemba na Oktoba.

Ziara ya kichungaji huko Palermo:  Kalenda ya maadhimisho ya kiliturujia itakayo ongozwa  Papa ambayo Msalishi Mkuu, Askofu Mkuu Guido Marini ameitoa tarehe 4 Septemba 2018, itafunguliwa na  siku ya Jumamosi 15 Septemba kwa Ziara ya kichungaji huko Palermo nchini Italia, katika fursa ya kukumbuku ya mwaka XXV wa kifodini cha mwenye heri Padre Giuseppe Puglisi. Itakuwa ni siku ya kina, mahali ambapo Baba Mtakatifu Francisko atakutana na waamini, makleri mahalia na vijana. Hiyo ni safari inayotarajia kuanza saa 12.30 alfajiri kutoka Roma na kurudi majira ya saa moja kamili za jioni  katika uwanja wa Ciampino Roma.

Safari ya kuelekea katika  Nchi za Kibaltiki:  Nchi zaBaltiki ni jina linalojumuisha nchi tatu ambazo ni  Estonia, Latvia na Lithuania. Jumamosi tarehe 22 Septemba Baba Mtakatifu atafanya ziara yake katika nchi za Kibaltiki. Hiyo itakuwa ni ziara yake ya 25 ya kitume. Ni sehemu  tatu zinazotarajiwa hadi tarehe 25 Septemba, huko Vilnius, Riga, na Tallin , katika nchi za Lithuania, Latvia na Estonia.

Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Vijana:  Katika mwezi wa Oktoba, utakuwa umejikita juu ya Sinodi ya XV ya Maaskofu kuhusu mada ya Vijana, Imani na mang’amuzi ya miito. Shughuli hiyo itafunguliwa rasmi tarehe 3 Oktoba kwa Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kuanzisa saa nne asubuhi masaa ya Ulaya na kuhitimishwa Sinodi hiyo tarehe 28 Oktoba 2018.

Watakatifu saba watakaotangazwa: Tarehe 14 Oktoba 2018  katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican saa nne na roba, Baba Mtakatifu Francisko ataongoza Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza wenyeheri: Papa Paolo VI, Oscar Arnulfo Romero Galdámez, Francesco Spinelli, Vincenzo Romano, Maria Caterina Kasper, Nazaria Ignazia wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu na Nunzio Sulprizio.

04 September 2018, 16:30