Kardinali P.Turkson ametoa hotuba katika mada ya Chuki dhidi ya wageni , ubaguzi, ustaarabu wa kitaifa dhana ya  mazingira ya uhamiaji wa kimataifa Kardinali P.Turkson ametoa hotuba katika mada ya Chuki dhidi ya wageni , ubaguzi, ustaarabu wa kitaifa dhana ya mazingira ya uhamiaji wa kimataifa 

Hotuba ya Kard Turkson kuhusu chuki dhidi ya wageni na ubaguzi!

Katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano juu ya mada ya chuki dhidi ya wageni na ubaguzi, Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, amesema mkutano huo unataka kutafakari jinsi gani jamii ya sasa ya makaribisho inajikita kukabiliana, hasa kwa wageni wapya

Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Umefungulia Mkutano tarehe 18 Septemba 2018 katika Hotel ya Ergife, Mkutano wa Kimataifa unaoongo zwa na mada ya kuhusu “Chuki dhidi ya wageni , ubaguzi, ustaarabu wa kitaifa dhana ya  mazingira ya uhamiaji wa kimataifa.  Mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu, Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha umoja wa Wakristo.

Maisha ya wahamiaji yanawajibisha dhamiri zetu binafsi: Katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano huo, naye Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, amesema mkutano  huo unataka kutafakari jinsi gani jamii  ya sasa ya makaribisha inajikita kukabilisha, na hasa kwa wageni wapya, na  mtazamo ambao unasababisha wafike hao wageni, ili kutathimini maadili, sheria ya kijamii mbele ya matukio haya kama ya wahamiaji ambao daima wamekuwapo katika historia ya binadamu.

Kardinali Turkson akiendelea anasema “ sisi ni mashuhuda wa “ historia za wanaume na wanawake, watoto na vijana ambao wanahatarisha maisha yao, hata ya wapendwa wao, wakitafuta maisha bora. Maisha ya watu hao, majeraha yao na matumaini, yanatufanya tutafakari ndani ya dhamiri na kufikia hatua ya kutafakari juu ya mtazamo ambao jamii ya makaribisho unajikita katika wageni wapya. Hata hivyo amejiuliza kama kweli ubinadamu huo upo kwa miaka 70 ya kutiwa saini ya makubaliano ya Mkataba wa Kimataifa  kuhusu haki ya binadamu. Je kweli dunia imeweza kutambua kujenga jamii mahali ambao raia, rangi, kabila dini, maoni ya kisiasa , uasili wa utaifa au jamii, utajiri au umaskini, vimekuwa sababu msingi kwa kuthibitisha kuwa lazima kuwepo na utofauti, ubaguzi, chuki au watu kuwekwa pembezoni mwa jamii ya binadamu?

Kukaribisha wahamiaji ni msingi kimaadili  unaochota nguvu yake kutoka katika Injili: Licha ya hayo, Kardinali Turkson amethibitisha juu hisia za wengi na matendo ambayo yanajionesha kwa raia kuwa na hofu hata kufikia chuki kwa watu, kabila utaifa au dini mambo ambayo kwa sasa katika jamii imekuwa ndiyo habari sana.  Kadhalika amesisitiza juu ya kesi hiyo kwamba, katika historia ya ukristo, uzoefu wa wahamiaji na uhamisho katika maeneo asili , umetambuliwa hata kwa Bwana wetu Yesu Kristo , ambaye si kwamba alitambulia kuwa kama mgeni tu, lakini yeye mwenyewe akiwa mtoto aliutambua uhamiaji  na kukimbia nchi yake. Kwa kuwa kukaribisha wageni hasa wanakabiliwa na hatari, ni msingi wa kimaadili ambao unapata msingi na nguvu kutoka katika Injili na Maandiko Matakatifu na  ndiyo sehemu ya maisha ya kikristo hata kuwa sehemu ya Kristo, amethibisha.

Kuogopa kumfungulia mwingine: Akizungumza juu mantiki ya ufunguzi wa mwingine amesema, inahitaji udhati kwa mantiki ya uhamiaji kimataifa ambao mara kwa mara kuna hofu na kutokuwa na matumaini ya kumfungulia mwenzako. Wakati huo huo, tunatumaini katika maonesho mengi ya mshikamano na huruma ambayo pia ni desturi ya nyakati hizi.

Benedikto XVI: Jamii ya utandawazi inatufanya kuwa karibu lakini haitufanyi tuwe ndugu: “ Ni mara ngapi tumesikia katika vyombo vya habari  “ kijiji cha dunia” kwa maana ya kuelezea jamii zetu. Wazo la kijiji linatupeleka katika mahusiano, ukaribu, na ule mshikamano wa pamoja, wazo lakini ambao kila siku anabainisha  ni kunyume  na habari kwa maana matendo yanayotazama juu ya  mapokezi ya wahamiaji,inakuwa ni matatizo. Kardinali Peter Turkson  kwa upande huo akikumbuka ndani ya akili yake maneno ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliyo andika katika Waraka wa Caritas in Veritate yaani Upendo katika Ukweli :“ni  Jamii ambayo daima inazidi kuwa utandawazi zaidi ambao unatufanya kuwa karibu, lakini ni ambao hautusaidii kuwa ndugu”. Kwa maana hiyo kwa kuhitimisha kuwa, katika Mkutano huo, ni lazima kutafakari kwa kina juu ya  nafasi ya Makanisa yote ambayo yameitwa kujikita katika mantiki hiyo nyeti ya wahamiaji.

19 September 2018, 14:50