Tafuta

Vatican News
Ziara ya Kitume ya Papa nchini Estonia,Lethuania e Latvia 2018 Ziara ya Kitume ya Papa nchini Estonia,Lethuania e Latvia 2018 

Ziara ya Papa nchi za kibaltiki ni kuwa karibu na Kanisa hilo!

Msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Grek Burke ameonesha kwa ufupi wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya kitume ya Papa Francisko katika nchi tatu za Kaskazini ya Ulaya.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ziara ya Papa Francisko kuelekea nchi ya Lithuania, Letvia na Estonia, inarajiwa kufanyika tarehe 22 -25 Septemba 2018, ikiwa pia ni  fursa ya kutoa heshima  kwa wangahanga wote walioteseka kwa ajili kutetea imani.  Ndivyo msemaji Mkuu wa Vatican alivyokumbusha kwa waandishi wa habari  kuhusu ziara ya Papa Francisko ambayo anethubitisha kuwa inaangukia  katika mwaka wa 25 tangu kufanyika ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II  katika nchi za Kibaltiki.

Nchi tofauti sana

Bwana Burke katika kuelezea nchi hizi ambazo Baba Mtakatifu Francisko anatembelea, pia amesisitiza kuwakatika umbali uliopo hapa na wa nchi hizo , unaweza kutufanya tufikirie nchi hizo zinafanana, na kwa hakika ni mataifa matatu kama dada wa kuzaliwa pamoha , japokuwa kama ambavyo dada wa kuzaliwa wakati mwingine hafanani , kwa maana kila mmoja ana utofauti na mwingine. Akifafanua utofauti huo ametoa mfano kuwa nchi ya Lithuania, sehemu kubwa ya watu karibu asilimia 80% wanakiri imani katoliki. Waakati huo huo nchini Latvia, sehemu kubwa ni waluteri, na ambao wamechanganyokana na  kati ya nchi ya  Lativia na Urusi. Nchi ya Estonia, Bwana Burke amekumbusha kuwa,  asilimia 75 % ya watu wanajidhihirisha hawana dini. Pamoja na hayo , anafikiri kwamba hiyo ndiyo changamoto ambayo kwa upande wa Baba Mtakatifu anapenda. Hiyo ni kwasababu ya kufikiria  kwamba katika nchi ya Estonia, Papa Francisco atatembelea jumuiya ya wakatoliki elfu tano, ambao ni kama parrokia moja katoliki katika nchi za Ulaya mashariki. Kutokana na hiyo, ni wazi  kutambua kwa mara nyingine tena kwamba ni ishala ya uwepo wa Baba Mtakatifu  katika maeneo ya pembezoni.

 Safari ya historia

Kati ya kipindi muhimu cha ziara yake hasa Jumapili tarehe 23 Septemba, itakuwa ni kutembelea katika Jumba la Makumbusho ya mateso na mapambano ya kuwania uhuru huko Vilnius, nchini Lithuania , ambapo Papa Francisko atakaa kitambo  kwa sala fupi  katika jukwaa la makumbusho kwa ajili ya waathirika ubaguzi. Bwana Burke amethibitisha kwamba ziara hiyo pia   inafanyika siku ambayo ni kumbukumbu ya  maadhimisho ya miaka 75 tangu waharibu kambi la mateso. Kwa maana hiyo ameongeza kusema: Katika Jengo la makubusho hayo anaamini  ni ishala kwa wale walioteseka. Na katika jengo hilo Papa atatembelea vyumba vilivyo kuwa vya wafungwa, ukumbi wa mateso, na mahali ambamo watu wengi waliteswa vibaya, wakiwemo mapadre na maaskofu ambao walipigwa mijeredi na kuteswa vibaya.

20 September 2018, 11:20