Tafuta

Vatican News
Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican 

Kard. Parolin:Mkataba wa Vatican na China ni muhimu!

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ,amethibitisha mara baada ya saini rasmi ya makubaliano ya uteuzi wa Maaskofu, kuwa Mkataba ni muhimu sana hasa katika maisha ya Kanisa Katoliki nchini China na kwa ajili ya mazungumzo kati ya Vatican na Viongozi wakuu wa raia

Sr Angela Rwezaula- Vatican

 “Mkataba ni muhimu sana hasa katika maisha ya Kanisa Katoliki nchini China na kwa ajili ya mazungumzo kati ya Vatican na Viongozi wakuu wa raia”.  Ndiyo usemi wa Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, alio uthibitisha mara baada ya saini rasmi ya makubaliano ya uteuzi wa Maaskofu, saini iliyowekwa tarehe 22 Septemba 2018. Kardinali anasema kuwa, mchakato wa muda mefu uliofanyika kati ya makubaliano  hayo yanasisitiza msimamo wa upeo wa kimataifa wa amani.

Kardinali Pietro Parolin ameendelea kuthibitisha kuwa, “Kusainiwa kwa mkataba wa muda kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa China juu ya uteuzi wa Maaskofu, unapata umuhimu zaidi, si tu hasa katika maisha ya Kanisa la China na nchi kwa ajili ya mazungumzo kati ya Vatican na Viongozi wa rai wa nchi, lakini pia ni msimamo katika upeo wa kimataifa kwa ajili ya  amani katika kipindi hiki ambacho tumo tunafanya uzoefu wa mivutano mikubwa kwa ngazi ya dunia”

Lengo la kiuchungaji

Hata hivyo akisisitizia zaidi amesema, “lengo la Vatican ni lengo la kiuchungaji, kwa maana ya kusaidia Kanisa mahalia ili hatimaye wafikie kufurahia hali nzuri ya uhuru kamili wa kujitegemea na kupanga kwa namna ya kwamba, wanaweza kweli kujikita katika shughuli za kiutume na kutangaza Injili kwa kuchangia maendeleo ya binadamu na katika jamii”.

Kuhangaikia waamini wa watu wa China

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, leo hii Maaskofu wa China wanaungana na Maaskofu wa Roma. Papa Francisko, kwa njia ya watangulizi wake, anatazama kwa namna ya pekee umakini wa kuwasaidia waamini wa China. Kuna haja ya umoja, kuna haja ya imani, kuna haja ya ari mpya; kuna haja ya kuwa na Wachungaji wema,ambao wanapaswa kutambuliwa na Kharifa wa Mtume Petro na Viongozi wa raia katika nchi yao. Makubalino hayo ni upeo; ni chombo ambacho kwa matumaini kinaweza kusaidia mchakato huo na ushirikiano wa wote.

Kushinda vikwazo vya kutoelewana

Katika Jumuiya ya wakatoliki wa China, ikiwa ni maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na waamini, Papa Francisko anawakabidhi kwa namna ya pekee waishi kwa roho ya dhati ya mapatano kati ya ndugu kwa kufanya ishara za dhati ambazo zinashinda vikwazo vya wakati uliopita  vya kutoelewana, hata vya nyakati zilizopo. Kwa maana hiyo waamini wakatoliki wanaweza kuwa mashuhuda wa imani yao, ya upendo na kujifungulia katika mazungumzo kati ya watu wote na kuhamasisha amani ya kweli.

25 September 2018, 10:27