Tafuta

Vatican News
Tarehe 1 Septemba 2018 ametangazwa Mwenye heri mpya  Anna Kolesarova nchini Slovakia Tarehe 1 Septemba 2018 ametangazwa Mwenye heri mpya Anna Kolesarova nchini Slovakia  

Card. Becciu:Vijana igeni mfano wa kijana Anna Kolesarova!

Kardinali Becciu anabainisha kuwa ushujaa na utakatifu haushutukizwi, kwa namna ya pekee akitazama maisha ya Anna Kolesarova, ambaye mnamo tarehe 22 Novemba 1944 aliuwawa akiwa na umri wa miaka 16 tu, akiwa anatetea hadhi yake na usafi wa mwili na moyo wake!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican News

Huko Kosice nchini Slovakia ametangazwa Mwenyeheri Anna Kolesarova , tarehe 1 Septemba 2018, katika Misa iliyoongozwa ikiwa ni kwa mara ya kwanza na Kardinali Angelo Becciu, Rais mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wenye heri na watakatifu. Katika mahubiri yake, amewaalika vijana kutazama kijana Anna wa miaka 16 aliye chagua kufa kuliko kuharibu usafi wa mwili wake. Je ni nguvu zipi leo hii zinaendelea bado dhidi ya wanawaka hata kwa Barani Ulaya !

Kardinali Becciu anabainisha kuwa ushujaa na utakatifu haushutukizwi, kwa namna ya pekee akitazama maisha ya Anna Kolesarova, ambaye mnamo tarehe 22 Novemba 1944 aliuwawa akiwa na umri wa miaka 16 tu, akiwa anatetea hadhi yake na usafi wa mwili na moyo wake!

kwa njia ya mikono ya wanajeshi wa kisovietik , wakati anatetea hadhi yake na usafi wa mwili wake .  Yeye aliweza kufikia kifo dini akiwa amejiandaa, hiyo ni kutokana na kwamba alibarikiwa kuwa na neema ya dhati katika maisha yake ya kiroho kutokana na kujimwilisha kwa  sala za kila siku na kupokea sakramenti.

Mtakatifu Maria Goreti mpya

Akendelea kufafanua maisha yake, anasema, yeye ni mfano wa maisha kwa ajili ya vijana ili nao waweze kugundua uzuri wa upendo wa dhati, kama hata thamani kubwa ya usafi”. Mwenye heri mpya Anna, amemfananisha na Mtakatifu Maria Goreth aliyetangazwa Mtakatifu na Papa Pio XII kunako mwaka 1950, na kwamba, wapo vijana wengi sana ambao walifanya uchaguzi kama huo. Kifodini cha ubikira, amesisitiza, unaendelea kushuhudia nguvu ya upendo wa Mungu na kwa ajili ya Mungu, upendo ambao unashinda daima ukatili wa binadamu.

Kubaka na uhalifu dhidi ya wanakeKatika kukumbuka kifo dini cha Anna, katika mantiki ya Vita ya Pili ya dunia, Kardinali Becciu ameangaza juu ya historia nyingi za imani na ishara nyingi za kiajabu ambazo zinaonesha jinsi gani Ulaya imekuwa na watu ambao walitambua kuamini thamani kuu isiyo weza kuachwa kamwe.

Kwa masikitiko makubwa Kardinali Becciu anasema: Ni watoto wangapi na wanawake, ambao wamekuwa chanzo cha vurugu na manyanyaso!  Hadi kufikia kufikiria kubaka kama  silaha ya vita na mbayo inabaki bila kuhukumiwa, bila kutambuliwa kama ni uhalifu dhidi ya binadamu. Ni nguvu ngapi zinaendelea kupenya bado juu ya wanawake kwa wazalendo wetu wa Ulaya mahali ambazo vifo vya wanawake vinaendelea kutapakaa, na mwili wa mwanamke mara nyingi umekuwa kitu cha kibiashara bila kujali utu wa kibinadamu.

Kutunza usafi

Kadhalika akitazama Sinodi ya maaskofu ijayo inayo husu vijana, Kardinali Becciu ametoa ushauri kwa vijana wasisaliti upendo wa kweli , na watambue kuwa ni vema kabisa kujisadaka yote kwa Bwana na kuwaalika watunze kile che thamani. “ Wote tunatambua jinsi gani ilivyo muhimu sana kutunza huduma ya uumbaji, na kwa kujikita kwa dhati kuhamasisha usafi wa hali ya hewa, mazingira , maji na chakula. Lakini na ndiyo hivyo na labda hata zaidi  uwepo wa ulazima wa kulinda usafi wa kile ambacho ni chenye thamani, yaani mioyo yetu na uhusiano wetu binafsi na wengine!

03 September 2018, 10:17