Mabadilishano ya Zana za Mfumo wa Makubaliano ya Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Benin Mabadilishano ya Zana za Mfumo wa Makubaliano ya Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Benin 

Vatican na Benin wabadilishana zana za hati ya mkataba!

Askofu Mkuu Brian Udaigwe wa Sueli na Balozi wa Vatican nchini Benin, na Mhs. Aurélien A. Agbénonci, waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Jamhuri ya Nchi ya Benin, wamebadilishana zana za Hati ya kuthibitisha Mfumo wa Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Benin kuhusu Sheria ya Kanisa Katoliki nchini Benin.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Tarehe 23 Agosti 2018, saa tano asubuhi, katika Makao ya Waziri wa Mambo ya Biashara ya nchi za nje na ushirikiano kimataifa huko Cotonou, Askofu Mkuu Brian Udaigwe  wa Sueli na Balozi wa Vatican nchini Benin, Mheshimiwa Aurélien A. Agbénonci, waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Jamhuri ya Nchi ya Benin, wameendelea Kubadilishana zana za  Hati ya kuthibitisha  Mfumo wa  Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Benin kuhusu Sheria ya Kanisa Katoliki nchini Benin, iliyokuwa umetiwa saini kunako tarehe 21 Oktoba 2016.

Katika tendo sherehe hizo kwa upande wa Vatican kulikuwapo na Askofu Victor Agbanou, wa Jimbo la  Lokossa  na Rais wa Baraza la Maaskofu wa katoliki wa  Benin; Askofu Eugène Houndékon, wa Jimbo katoliki la Abomey na Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu Benin;

Askofu Mkuu Roger Houngbédji, O.P., wa Jimbo Kuu la  Cotonou; Askofu François Gnonhossou, S.M.A., wa Jimbo katoliki la  Dassa-Zoumé; Askofu  Aristide Gonsallo, wa Jimbo la  Porto-Novo; Monsinyo. Luka Jogy Vadakara, Katibu wa Ubalozi wa Kitume ; Padre Pascal Guezodje, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Benin; Padre  Eric Okpeïtcha, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Baraza la maaskofu Benin; na Padre  Emmanuel Michodjèhoun, mhudumu mahalia katika Ubalozi wa kitume nchini Benin.

Na kwa upande wa Jamhuri ya nchi ya Benin walikuwapo: Bwana. Hervé Djokpé, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri wa biashara ya nchi za nje na ushirikiano (MAEC); Bi Agnès Avognon Adjaho, Balozi wa nchi ya  Benin nchini Vatican ; Bwana Bienvenu A. Houngbédji, Mkurugenzi wa sheria za Biashara  wa Wizara hiyo; Bwana Giono Morel Gnamy, Mkurugenzi wa Kitengo kwa ajili ya Ulaya  (MAEC); Bwana Ghislain Agbozo, Mkurugenzi msaidizi wa sera za biashara wa wizara na Bwana BLuc-Arthur Adjou, Mhudumu Maalum wa Waziri wa Wizara hiyo.

Mfumo wa Mkataba huo umeundwa na utangulizi wenye Ibara 19, ambao unahakikisha utekelezaji wa utume wake wa Kanisa nchini Benin. Kwa namna ya pekee kutambuliwa mfumo wa kisheria wa Kanisa na  taasisi zake. Sehemu zote mbili pamoja na kulinda uhuru wake katika uendeshaji wao ambao ndiyo wajibu wake, wanajibidisha pia kushirikiana kwa ajili ya ustawi wa kimaadili, kiroho na zana ya mwanadamu katika  kukuza manufaa ya kawaida kwa wote. Mfumo wa Mkataba huo kwa mujibu wa Ibara ya 19, ulianza kutumika siku ile ile ya ubadilishanaji wa Hati ya Kudhibitisha.

25 August 2018, 10:26