Tafuta

Ushirikiano wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya utetezi na ulinzi wa watoto Ushirikiano wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya utetezi na ulinzi wa watoto 

Tamko la Tume ya Kipapa kwa ajili ya utetezi wa watoto !

Utme ya Kiapapa imetoa ujumbe wake wa kumshukuru Baba Mtakatifu kwa ajili ya maneno yake yenye nguvu ambapo anatambua uchungu na mateso ya watu waathirika wa manyanyaso ya kingono, ya nguvu na pia nyanyaso za dhamiri kwa baadhi ya watu wa Kanisa. Wanahisi kuwa wadhambi daima, dhidi ya ujasiri wa kinabii na uvumilivu wa watu waathirika

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tume ya Kipapa kwa ajili ya utetezi wa watoto wamendika ujumbe mara baada ya kutangazwa kwa Barua ya Papa kwa Watu wa Mungu juu ya masuala ya manyanyaso ya kingono katika Kanisa. Katika ujumbe huo Tume inamshukuru Baba Mtakatifu kwa ajili ya maneno yake yenye nguvu ambapo anatambua uchungu na mateso ya watu waathirika wa manyanyaso ya kingono, ya nguvu na pia nyanyaso za dhamiri kwa baadhi ya watu wa Kanisa. Wanahisi kuwa wenye dhambi daima, dhidi ya ujasiri wa kinabii na uvumilivu wa watu wengi na wanawake ambao kilio chao kimekuwa chenye nguvu zaidi ya zana ambazo zilitaka kuwanyamazisha.

Wajumbe wa Tume ya Kipapa ya utetezi wa watoto, wanahisi kabisa kuguswa na wito wa Papa kwa wahusika wote wa Kanisa ili kuendelea katika mapambano dhidi ya manyanyaso ya kingono, hata  kwa namna ya kuongeza zaidi juhudi ya  kuwaajibisha wale ambao wametenda au wamefunika uhalifu huo. Katika Barua ya Papa Francisko, ujumbe unaendelea, jukumu na uwajibikaji wa manyanyaso hayo sasa na daima ndiyo shughuli muhimu.

Ujumbe huo umehaririwa na Profesa Myriam Wijlens, mjumbe wa chombo hicho cha tume ikiongozwa na Kardinale Sean O’Malley.  Kwa upande wa profesa wa sheria , anasema katika barua ya Papa  hiyo zipo mantiki tatu:  Nafasi ya kwanza Papa anaeleza bayana muungano kati ya manyanyaso ya kingono, manyanyaso ya nguvu na manyanyaso ya dhamiri na kusisitiza jinsi gani wengi hawataki kulitambua.

Pili Profesa Wijlens, anaandikia, Papa anataja ngazi mbili za manyanyaso, yaani kwa yule aliyetumia nafasi aliyo nayo kujiingiza katika manyanyaso kwa watoto na  watu wazima waathirika , wakati  mwingine anayetumia nafasi yake kama kiongozi kutumia uwezo wake n anafasi aliyo nayo  kufunika manyanyaso hayo.

Sehemu ya tatu anaelezea Profesa, ni kwamba Papa anaomba masamaha  na kutafuta namna gani ya kuweza  kutubu kwa dhati kulingana na janga hili kuwa kubwa, jambo ambalo anasema halitawezakana  kupona, na kwa njia hiyo katika barua yake anaomba yawepo mabadiliko yenye mzizi wa kina wa utamaduni katika ulinzi na usalama kwa watoto na ndiyo liwe suala la kupewa kipaumbele!

22 August 2018, 16:25