Mtakatifu Yohane Paulo II, Waraka wa Kitume "Mng'ao wa ukweli" Kumbu kumbu ya miaka 25 tangu uzinduliwe Mtakatifu Yohane Paulo II, Waraka wa Kitume "Mng'ao wa ukweli" Kumbu kumbu ya miaka 25 tangu uzinduliwe 

Jubilei ya Miaka 25 ya Waraka wa Papa JPII. "Mng'ao wa ukweli"

Waraka wa "Mng'ao wa ukweli unajikita katika mafundisho tanzu ya Kanisa kuhusu maadili na utu wema yanayobubujika kutoka katika: Maandiko Matakatifu na Mapokeo Hai ya Kanisa, kwa mwamini kumwelekea Kristo Yesu ili kupata majibu muafaka, tayari kusoma alama za nyakati na kuzipatia majibu mintarafu mwanga wa Injili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kanisa linakumbuka miaka XXV tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipochapisha Waraka wa kitume “Mng’ao wa Ukweli” “Veritatis Splendor” kunako tarehe 6 Agosti 1993. Ni Waraka unaojikita katika mafundisho tanzu ya Kanisa kuhusu maadili na utu wema yanayobubujika kutoka katika: Maandiko Matakatifu na Mapokeo Hai ya Kanisa, kwa mwamini kumwelekea Kristo Yesu ili kupata majibu muafaka, tayari kusoma alama za nyakati na kuzipatia majibu mintarafu mwanga wa Injili. Utu wema unapaswa kuwa ni jibu makini la kimaadili linalolobubujika kutoka katika Amri za Mungu. Mtakatifu Yohane Paulo II alilitaka Kanisa  kuwa makini katika mitazamo mbali mbali ya kitaalimungu.

Uhuru na sheria viwasaidie waamini kutambua wema na ubaya katika maisha; kwa kukubali kuongozwa na dhamiri nyofu, mahali patakatifu ambapo Mwenyezi Mungui anazungumza na waje wake katika ukweli na uwazi. Maadili mema ni nyenzo msingi ya uinjilishaji na kwamba, Kanisa linathamini huduma ya kitaalimungu, lakini kwa kutambua pia uwepo wa viongozi wa Kanisa.

Utu wema na maadili vinapaswa kupenyeza mizizi yake katika maisha ya kijamii na kisiasa na kwamba, maadili ni sehemu muhimu sana ya mchakato wa uinjilishaji mpya unaogusa  mahitaji msingi ya binadamu. Lengo ni huduma kwa binadamu na jamii katika ujumla wake. Mtakatifu Yohane Paulo II anakaza kusema, utakatifu unapambwa kwa Amri za Mungu na kutembea katika Mwanga wa Kristo Mfufuka!

Sikiliza kwa raha zako mwenyewe!

 

04 August 2018, 15:17