Papa:Kanisa litoe kipaumbele kwa waathirika wa manyanyaso !
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Mbele ya ripoti ilitolea kwa umma huko Pennsylvania mapema wiki hii, yapo maneno mawili ambayo yanaweza kujieleza kulingana na majaribu mbele ya majanga ya kihalifu na kutishia ambayo ni aibu na uchungu. Hayo ni maneno kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari za Vatican Bwana Greg Burke.
Bwana Burke akiendelea na taarifa hiyo kwa vyombo vya habari amesisitiza kwamba “Vatican inafikiria kwa umakini mkubwa wa kazi ambayo imefanyiwa na upelelezi wa chombo cha Investigating Grand Jury huko Pennsylvania na ripoti kamili (Interim Report) iliyoitolewa. Ktuokana na ripoti hiyo, Vatican inahukumu vikali manyanyaso hayo juu ya watoto. Na waliofanya manyanyaso hayo hata wotewalioandikwa katika ripoti hiyo wanahukumiwa na kimaadili kupewa onyo kali. Kwa maana matendo hayo yamesaliti matumaini na kuiwaibia waathirika hadhi yao na imani yao”
“Kanisa lazima lifunze kutokana na mafundisho makali ya wakati uliopita na lazima kuwajibika kwa wale ambao wamesababisha manyanyaso, hata kutenda. Sehemu kubwa katika ripoti inatazama manyanyaso yaliyotokea wakati wa miaka kabla ya 2000. Kutokana na kutopata kesi nyingine baada ya mwaka 2002, hItimIsho la uchunguzi wa Grand Jury, wamekuwa makini katika upelelezi uliotanguliwa na ambao wameonesha jinsi gani kuna mabadiliko ya Kanisa Katoliki Marekani na jinsi gani wameweza kupungza matukio haya ya manyanyaso yaliyosababishwa na makleri. Vatican inawatia moyo bila kuchoka hayo mageuzi na usimamizi kwa ngazi zote za Kanisa Katoliki katika kuhakikisha ulinzi wa watoto na watu wazima waliodhulika. Zaidi ripoti inasisitizia juu ya umuhimu wa kutii sheria za raia wakiwemo ulazima wa kutoa ripoti kesi za nyanyaso dhidi ya watoto”
Bwana Burke anahitimisha akithibitisha kuwa, Baba Mtakatifu Francisko anatambua vema jinsi gani uhalifu huo umeweza kutingisha na kudhoofisha imani na roho ya waamini, anatoa wito wa kufanya kila juhudi ili kuunda mazingira salama kwa ajili ya watoto na watu wazima waliodhulika katika Kanisa na katika jamii nzima. Waathirika lazima watambue kuwa, Baba Mtakatifu yuko katika upande wao. Na wote walioteseka ndiyo wa kupewa kipaumbele, pia Kanisa linataka kuwasikiliza ili kuweza kung’oa janga hili la kutisha na ambalo linaharibu maisha ya wasio kuwa na hatia”