Tafuta

Vatican News
Ziara ya Papa FRancisko mjini mjini Dublin ni tukio muhimu Ziara ya Papa FRancisko mjini mjini Dublin ni tukio muhimu 

Padre Mello:Mkutano huko Dublin ni tukio muhimu la familia !

Padre Mello, Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ana uhakika kuwa, itakuwa furaha kubwa kuungana katika mkutano wa familia duniani huko Dublin, hata kwa wale wote ambao wanakuwa na fursa kama hiyo. Utakuwa ni muda mwafaka wa kuhamasika kwa familia ili iweze kuishi kwa kile chochote ambacho Kanisa linafundisha.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kila kitu mjini Dublin ni tayari kuanza maadhimisho ya Mkutano wa IX wa Familia duniani, ambapo tarehe 21 Agosti umefunguliwa rasmi na  mahali ambapo Baba Mtakatifu ataungana nao katika maadhimisho hayo, kuanzia tarehe 25-26 Agosti 2018 , ikiwa ni ziara yake ya kitume ya 24!  Familia nyingi na waamini nchini Ireland wanamsubiri Baba Mtakatifu Francisko kwa hamu sana ili wapate kumsikiliza ujumbe wake katika maadhimisho ya mkutano huo wa dunia unaotazama familia ya Mungu.

Padre Alexandre Awi Mello, Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha amehojiana na mwandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa Familia duniani huko Dublin ambapo anakiri kwa dhati kwamba, kwa hakika ni moja ya tukio muhimu kwa upande wa a Baraza lao. Yapo matarajio makubwa ya uwepo wa Papa Francisko na kwa kila kitu ambacho atazungumza.

Utakuwa ni muda mwafaka wa kuhamasika kwa familia ili iweze kuishi kwa kile chochote ambacho Kanisa linafundisha.  Padre Mello ana uhakika kuwa, itakuwa furaha kubwa kuungana katika mkutano huo na hata kwa wale wote ambao wanakuwa na fursa kama hiyo. Zaidi ya watu 35,000 wataudhuria Kongamano la kichungaji, na zaidi watu 500,000 wataudhuria Misa ya hitimisho na Baba Mtakatifu. Kwa dhati ni muda mwafaka na wanausubiri kwa furaha na matumaini. Ni kipindi ambacho kitabaki katika moyo wa wote na tukio moja muhimu la kihistoria la Kanisa.

Kongamano la familia limegawanyika sehemu 60 za mafundisho ya Amoris Laetitia

Kwa upande wa Kongamano wameweza kuligawa katika sehemu 60 na ambazo zinazungumzia na kufundisha juu ya Wosia wa Kitume wa Papa Francisko wa Amoris Laetitia yaani furaha ya upendo ndani ya familia. Wengi wataweza kuchota utajiri wa wosia uliomo ndani yake, pamoja na kwamba wengi wa familia wamesoma na wanaendela kuusoma na kuelewa unataka nini katika maisha yao.

20 August 2018, 18:48