Vatican News
2018.08.01 Incontro Mondiale della Famiglia. 2018.08.01 Incontro Mondiale della Famiglia. 

Mitindo ya zamani ya kichungaji ya familia haifanyi kazi tena

Rais wa Baraza la Kipapa la Walei ndoa na familia na Maisha, Kardinali Kevin Farrel akihojiana na Vatican News amesema, Familia inapaswa ijisimulie yenyewe. Je ni nani anaweza kuwa shuhuda mzuri zaidi ya wale ambao wanafanya uzoefu wa kila siku katika uzuri wa familia?

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Wakati wa kusubiri familia nyingi kutoka nchi 116 duniani, vijana elfu 6, wanye umri chini ya miaka 18 ambapo taarifa inathibitisha kuwa, ni namba kubwa ya kihistoria ambayo haijawahi kutokea katika mikutano ya familia duniani hadi sasa, watu wa kujitolea elfu 7 lakini bado pia  tiketi za watu 85,000 watakaofika  kwenye Tamasha na Baba Mtakatifu Francisko katika Uwanja wa   Croke mjini Dublin , watu laki 5 waliojiandikisha kuudhuria Misa ya  Baba Mtakatifu katika hitimisho la Siku ya 9 ya Familia duniani katika uwanja wa Phoenix. Vilevile watu 37 elfu waliojiandikisha kuudhuria Kongamano la siku tatu kuanzia tarehe 22-24 Agosti  na kufanya jumla ya shughuli ya pamoja yenye makundi 65, itakayokuwa na watoa mada 200  na sehemu kubwa ni wanawake walei na familia nyingi.

Katika maandalizi haya ambayo yamebakia siku chache ya Mkutano wa 9 wa  Familia duniani, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei ndoa na  familia na maisha, Kardinali  Kevin Farrel akiojiana na Vatican News amesem: Familia inapaswa ijisimulie  yenyewe. Je ni nani anaweza kuwa shuhuda mzuri zaidi ya wale ambao wanafanya uzoefu wa kila siku katika uzuri wa familia?

Maadhimisho ya Mkutano wa 9 wa Familia Duniani unaongwa na mada ya Injili ya Familia: furaha ya ulimwengu ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 21-26 Agosti 2018 mjini Dublin nchini Ireland (www.worldmeeting.ie). Hata hivyo katika kongamano wataudhuria wawakilishi zaidi ya 100 kati yao 50 watatokea katika nchi za pembezoni mwa dunia, yote hiyo ni shukrani kwa Baraza la Kipapa la Walei,ndoa na  familia na kwa ushirikisnao na Jimbo Kuu la Dublin na majimbo mengine ya Ireland!

Kardinali Farrel anasema, matarajio ni mengi lakini lengo msingi ni maendeleo ya kichungaji kwa familia ambayo kwa mapana na marefu yanajieleza zaidi katika Wosia wa kitume wa Amoris Laetitia, yaani Furaha ya upendo ndani ya familia. Tunaishi kwa mantiki ya ubinafsi na mahangaiko ambayo yanahatarisha kupumbaza uzuri wa ndoa na familia; mikakati na mitindo ya kichungaji ya wakati uliopita utafikiri haifanyi kazi tena mbele ya  mabadiliko makubwa ya kijamii; katika hali hii, yenye mizizi mipya na daima nyeti, wote tunaihisi, lakini tunatakiwa kuwajibika katika kuandaa na kusindikiza wachumba ili kufikia katika ndoa kwa namna ya uwajibikaji hasa na wenye msimam wa kweli kama wakatekumeni, kwa mujibu wa maelezo mazuri ya Papa Francisko!

Rais wa  Baraza laKipapa la  Walei Ndoa na Familia  Kardinali Farrel anaongeza kusema,  hii siyo shughuli ya kuandaa kwa urahisi mafunzo ya ndoa kwanza, bali suala ni kutilia mkazo zaidi na kuwasindikiza hata kwa miaka ya kwanza mara baada ya kufunga ndoa yao wanaume na wanawake ambao wanachagua kufanya kuwa sehemu ya mpango wa Mung! Wakati uliopita katika shughuli nyeti hiyo  na nzuri, ilikuwa ikionesha familia kuwa kiungo kubwa  na kuundwa na mtandao ambao kwasasa umepoteza radha yake kwa sababu ya kulegeza mahusiano au kwa urahisi kwasababu ya matatizo yanayojitokeza, kwa mfano kutokana na dharura ya kazi, watu wangi wanalazima kuishi mbali na maneo yao ya asili.

Katika mtazamo wa mantiki ya nchi ya Ireland kwa namna ya pekee historia yake na urithi mkubwa na ambao kwa kiasi kikubwa kuna makovu,  hasa hali halisi ya moto uliotokana na maoni ya kura za sheria ya utoaji mimba, Kardinali Farrel  anathibitisha  kuwa daima  ni kipindi cha namna ya  pekee cha kukumbuka na kuongezea maisha na utume wa familia. Hali halisi ya sasa ndiyo anasema ni ngumu na ambayo haiwezi kukanushwa, lakini pia imejaa kiini cha maisha na kuchocheo cha kuzaliwa.  Shughuli ya kichungaji inajikita katika maisha ya familia nyinyi na nguvu ya kutangaza furaha katika ulimwenguhasa kwa wakati wa siku hizi na kurudia kutangaza bila kuchoka ya kuwa familia daima ni chemichemi na asili; ni msingi ambao hauwezi kutengeuliwa kamwe kwa ajili ya wema wa pamoja na maisha ya Kanisa.

Mkutano wa Familia mjini Dublin ni fursa kubwa kwa wanafamilia katoliki ambao wanajikita ndani yake, wamehamasika na kuonesha  imani yaona kushuhudia katika ulimwengu kwa familia zote na watu wote wenye mapenzi mema, kwamba furaha ya Injili lazima kuishi , pamoja na vikwazo vilivyopo vya hali halisi ya sasa! Mkutano wa familia duniani hauna lengo lolote la kubadili mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya ndoa, badala yake ni kuonesha ukuu wake na uzuri  na zaidi kwa ishala ya furaha. Ndiyo maana ya kauli mbiu inayoongoza mkutano huo “Injili ya familia: furaha ya ulimwengu”.

14 August 2018, 16:01