Tafuta

Kila mtu anayo haki ya kufurajia amani katika maisha. Kila mtu anayo haki ya kufurajia amani katika maisha. 

Kila mtu anayo haki ya kufurahia amani katika maisha!

Akofu mkuu Jurkovic anasema, kwa kuwa kila mmoja anayo haki ya kufurahia amani, basi kila taifa lijikite katika kutimiza wajibu wake wa kutafuta njia madhubuti za kusimika amani inayodumu; amani ni matunda ya haki, katika kujihusisha na ushiriki endelevu wa michakato ambapo majadiliano yanatiwa moyo na kinzani zinatafutiwa ufumbuzi katika roho ya uelewano na mshikamano.

Na Padre Celestine Nyanda. – Vatican.

Haki ya kuwa na amani, sambamba na haki ya uhai, uhuru wa kuabudu na imani, vinaweza kutazamwa kwa namna fulani kama ni kiini cha mfumo mzima wa kulinda na kutetea haki msingi za binadamu. Kwa hakika, haki ya kuwa na amani na kutetea amani ni hitaji msingi katika kufurahia haki zote msingi za binadamu. Huu ni utangulizi wa Askofu mkuu Ivan Jurkovic, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva, Uswisi, alipokuwa akitoa hotuba yake hivi karibuni katika warsha juu ya haki ya amani.

Askofu mkuu Jurkovic anasema, kwa kuwa kila mmoja anayo haki ya kufurahia amani, basi kila taifa lijikite katika kutimiza wajibu wake wa kutafuta njia madhubuti za kusimika amani inayodumu; amani ambayo ni matunda ya haki, katika kujihusisha na ushiriki endelevu wa michakato ambapo mazungumzano yanatiwa moyo na kinzani zinatafutiwa ufumbuzi katika roho ya uelewano na mshikamano. Diplomasia  ya pamoja katika karne iliyopita, imewakilisha moja ya kanuni mahali ambapo mataifa kwa kufuata kanuni ya ‘mataifa yote kiasili ni sawa kihadhi’, yameweza kuchakalika kutengeneza simfonia ya mahusiano kadiri ya misingi ya haki, ukweli, na nia ya ushirikiaano na uhuru. Vatican imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mchakato huu na kushirikishana nia ya pamoja ya kuokoa vizazi vijavyo kutoka katika janga la vita, kama ilivyonuiwa katika Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo amani sio tu kutokuwepo kwa kinzani za vita, bali ni ule mwelekeo mpana zaidi wa juhudi za kila siku katika kusimika ulimwengu ulio na utaratibu kadiri ya mapenzi ya Mungu, kwa kuwa na haki timilifu kati ya watu, anasema Askofu mkuu Jurkovic. Kwa mwono huo, ni sahihi kabisa ile ibala ya pili ya Tamko juu ya haki ya amani inayoweka dira ya Jumuiya ya Kimataifa ya malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 inayosema ‘hakuwezi kuwa na maendeleo endelevu bila amani, na wala hakuna amani bila maendeleo endelevu’.

Kama ambavyo Baba Mtakatifu Paul VI anasema kwamba jina jipya la amani ni maendeleo, Vatican inaendelea kusimamia mwono huo wa kuwa na maendeleo yanayofumbata nyanja zote za binadamu kwa kuheshimu utu wa kila mmoja, kwa kuzingatia hali zote tangu kutungwa mimba mpaka mauti inapomfika, bila kutenganisha tunu zake za imani, tamaduni na uhuru, ambazo zinatambuliwa na sheria maadili iliyoandikwa katika maumbile asili ya mwanadamu mwenyewe.

Sikiliza kwa raha zako mwenyewe!

 

01 August 2018, 16:51