Misa Takatifu  ya Papa Francisko katika Uwanja wa  Phoenix mjini Dublin Misa Takatifu ya Papa Francisko katika Uwanja wa Phoenix mjini Dublin 

Askofu Mkuu Martin: Kuchanua kwa matumaini ya Kanisa la Ireland!

Askofu Mkuu Martin wa Dublin anasema, udhaifu wa imani nchini Ireland unaweza kufukuziwa mbali, kwa maana hiyo, utashi wake ni ule wa kuwasaidia familia zote ili waweza kukabiliana na wakati endelevu wa nchi hiyo ambayo ina haja ya kuangazwa na mwanga wa ujumbe wa Yesu Kristo.

Katika hotuba yake ya salam,  Askofu Mkuu Diamuid Martin wa Jimbo Kuuu Katoliki Dublin, alikuwa ameelezea juu ya hali halisi ya Kanisa la Ireland linalopitia kipindi kigumu. Watu wamejeruhiwa kwa kina kutokana na watu wa Kanisa; imani ya watu hawa imeweka katika majaribu, kadhalika amesema na Kanisa la Yesu Kristo limejeruhiwa. Amezungumza hayo wazi na kukumbusha jinsi gani nchi kwa dhati imeishi kipindi cha kivuli. Lakini pamoja na hayo, Kardinali Martin anaahidi kuwa Ireland itabadilika kwani matumaini ni yale ya kuchanua kwa upya Kanisa la hiyo wakati huu na endelevu.

Kardinali Martin, Askofu Mkuu wa Dublin anasema, udhaifu wa imani nchini Ireland unaweza kufukuziwa mbali, kwa maana hiyo,utashi wake ni ule wa kuwasaidia  familia zote ili waweza kukabiliana na wakati endelevu wa nchi hiyo ambayo ina haja ya kuangazwa na mwanga wa ujumbe wa Yesu Kristo.

Mkutano ujao wa Familia duniani utafanyika mwaka 2021 mjini Roma

Na katika salam zake za mwisho wa kuhitimisha Mkutano huo kwa familia ambao umeona watu wengi watoto, vijana wazee na familia nzima kwa ujumla ya kibinadamu imefika kuwakilisha pande zote za dunia kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2018, naye Kardinali Kevin Farrell, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, anakumbusha furaha kubwa ambayo wameiishi katika uzoefu wa siku hizo, wakiwa wanatafakari jinsi gani ya kujikita katika matendo wa kweli ya Wosia wa Amoris Laetitia yaani furaha ya upendo ndani ya familia, na kuigeuza ili iweze kweli kuwa chachu ya dhati katika mafundisho ya kikristo juu ya familia ya kweli  yenye upendo na ukarimu!

28 August 2018, 09:11