Tafuta

Vatican News
Mkutano wa Familia duniani Dublin, 21-26 agosti 2018 Mkutano wa Familia duniani Dublin, 21-26 agosti 2018 

Parolin:Nchi ya Ireland daima imekuwa na tabia ya matumaini

Ziara ya Papa nchini Ireland ni ujumbe wa kujifungulia wazi kuelekea wakati endelevu kwenye mwelekeo wa imani ambayo daima imekuwa tabia msingi wa nchi ya Ireland na watu wake na ambao watatambua kuzaliwa upya katika mioyo yao na kuzaa matunda ya amani na furaha.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika matazamio ya ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Ireland katika Mkutano wa Familia duniani ambao umefunguliwa rasmi tarehe 21 Agoati 2018 mjini Dublin, inakumbana na donda kubwa la nyanyaso la kingono katika Kanisa. Hii ni mada nyeti na zenye nguvu katika mahojiano ya Vatican News na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.  Katika mahojiano hayo Kardinali anathibitisha kuwa uwepo wa Papa Francisko nchini Ireland utakuwa ni ishara ya matumaini kwa wote na kutiwa moyo Kanisa mahalia na familia nzima ya dunia.

Katika kuelezea juu ya matarajio ya Mkutano huo, hasa baada ya Sinodi kuhusu Familia na Wosia wa Kitume wa Amoris laetitia , Kardinali Parolin anaamini kwamba ziara ya Papa nchini ya Ireland katika mkutano wa familia duniani itakuwa ni fursa kwa upande wake kuthibitisha utajiri wa mafundisho ya Kanisa juu ya tema ya familia kwa maana ya kusisitiza nafasi msingi ambayo familia inachukua katika Kanisa, katika jamii na kusimamia utume wa familia kama hali halisi ya upendo, uaminifu na kuwa nao katika utume wake wa kuonesha na kuelimisha maisha. Kadhalika anadhani kuwa, uwepo wa Baba Mtakatifu utakuwa ni sababu ya kutiwa moyo kwa dhati katika kusaidia familia kwenye utume wao na zaidi katika jitihada za kushuhudia uwepo wa upendo wa Mungu, hata uwezo wa familia kuonesha ile furaha ambayo leo hii dunia inatafuta kwa nguvu zake zote.

Kardinali Pietro Parolin aidha kwa upande wake mchango wa nguvu na asili ambao familia ya kikristo inaweza kutoa leo hii katika Kanisa na hata aliye mbali sana na uzoefu wa imani, anaamini kuwa familia leo hii inayo nafasi kubwa na muhimu ya kujikita na hasa akirudia kusema maneno ambayo amekwisha tamka , kwamba nafasi kuu ni ile ya kushuhudia furaha ya Injili , kuonesha ushuhuda wa furaha ya upendo wa Mungu ambaye anatambua kubadili maisha ya watu na anatambua kubadili maisha ya jumuiya. “ Leo hii tunaishi nyakati ambazo kuna mateso ya upweke , kubaguliwa; ni upweke wa mmoja na mwingine ambao mwisho wake unageuka kuwa upweke hata  mbele ya Mungu. Kwa maana hiyo Papa anasisitiza sana hata juu ya kazi ya familia ambayo ni kutoa uamsho kwa ngazi binafsi, hata kwa ngazi ya kijumuiya kwa maana kamili ya uwepo wa umoja na kuheshimu. Ni tegemeo la Kardinali Pietro Parolini kwamba Familia leo hii inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kujikita ndani ya jamii ya sasa.

Katika Mkutano huko Dublini, watazungumzia hata mada nyeti kama vile uhamiaji, kipeo cha familia na mapokezi kwa watu mashoga. Kanisa lina jambo la kuzungumza leo hii na hasa kwa wale ambao hawashiriki na kuchangia thamani yake na maono ya dunia hii? Katika kujibu swali hili Kardinali Parolin anasema, Kanisa ki ukweli lina pendekezo lake la kufanya, pendekezo ambalo linatokana na Injili; lakini yeye binafsi anaamini kwamba ni muhimu zaidi ya maneno  hasa ile tabia ya Kanisa ambauo ni kushuhudia, kwa maana ya kutoa mfano, na kwa matendo ya dhati, ya uzuri na ukweli wa Injili katika ulimwengu leo hii.

Pamoja na hayo lakini anathibitisha kwamba  hapo kuna majeraha mengi ya kuponya, kuna upweke mwingi na mipasuko ya kuunganisha. Tunaweza kujiundia ile picha ambayo Papa Francisko aliitumia tangu mwanzo wa Utume wake kama Papa, ya kwamba Kanisa ni kama Hospitali kambini, ambayo kwa dhati ndiyo inaweza kuwa karibu na watu na kuwasindikiza katika hatua yao ya kukua, hasa kwa upande wa majeraha, na hata uponyeshwaji. Kwa jinsi hiyo ndiyo tabia ambayo ina uwezo wa kusindikiza na uwezo wa kusikiliza , uwezo wa mazungumzo na uwezo wa kukua kwa pamoja.

Papa amesisitiza mara nyingi kwamba familia zinapaswa  kusindikizwa na taasisi zenye siasa inayostahili. Je kwa upande wake  ni kitu gani kitanapaswa kunza nacho?

Baba Mtakatifu anasema ni lazima kuanza na sisi wenyewe, kwa maana ni familia yenyewe na Kanisa lenyewe pia  linatakiwa kujikita kwa dhati kwa maana hiyo. Ameyasisitiza hayo sana katika wosia wa Amoris laetitia, mahali ambapo anasema, ilikuwa imekwisha fanya mengi, kwa maana ya kujiandaa, kusaidia kuandaa vijana katika Sakramenti ya Ndoa na kuunda familia, lakini pia lazima kufanya zaidi ya hayo.  Kwa hakika upo upande wa jumuiya ya kikristo, ambapo anaamini kwamba ni kwa mantiki ya kutoa ushuhuda na ubunifu,kadhalika kuna haja ya kutoa chachu ya jumuiya ya kisiasa ili waweze kuwa makini katika hali halisi ya familia,  iwe makini kwa mahitaji yake na kutazama shughuli zote zinazohusu mambo ya sheria inayostahili.

Papa anarudi Ireland mara baada ya miaka 40, wakati huo huo nchi ya  Ireland imefanya uzoefu wa jeraha la manyanyaso ya kingono, na  hata kufuatia ripoti ya hivi karibu ya Pennsylvania ambayo imetoa mshutusho. Binafsi ni nini anahisi kusema kwa Watu wa Mungu na hasa wa Ireland?

Kardinali Pietro parolin anaamini kwamba kwa wote na wanaendelea kwa kina kuwa na mshituko wa tukio hilo na ambao unaathiri hata ushuhuda wa Kanisa. Papa daima amewekuwa akisisita na anaendelea kusititiza juu ya uwajibu wetu wa kwanza. Wajibu wetu wa kwanza ni ule wa kukaa karibu na waathirika,  kuwasidia kwa namna ya kwamba wanaweza kujenga maisha yao. Anaongeza kusema Kardinali kwamba, anaamini Kanisa la Ireland limeweza kutambua makosa yake, dhambi zake  na wakati huo huo hata namna ya kutafuta jinsi gani ya kuingilia kati ili matukio haya yasiyo elezeka yasiweze kurudiwa tena. Kwa njia hiyo anaamini ya kwamba Ziara ya Papa nchini Ireland inajitokeza chini ya ishara ya matumaini na uwezo huo wa matumani hasa kwa njia ya kujikabidhi, ndiyo ufunguo wa kujikomboa , kubadilika na kuokolewa na upendo wa Mungu ambaye anajieleza katika uzoefu wa familia. Vilevile ni ujumbe wa kujifungulia wazikatika mchakato  wakati endelevu kwenye  mwelekeo wa imani ambayo daima imekuwa tabia msingi wa nchi ya Ireland na watu wake ambao watatambua kuzaliwa upya katika mioyo yao na kuzaa matunda ya amani na furaha.

22 August 2018, 12:43