2018.08.22 Dublino, Incontro famiglie 2018.08.22 Dublino, Incontro famiglie 

Kardinali Turkson:Biashara inapaswa kulenga talanta ya binadamu!

Kardinali Turkson anasema familia ni taasisi ya kibinadamu iliyopendwa na kuumbwa na Mungu kwa ajili ya kulea na kuendeleza maisha binafsi ya binadamu, kwa maana hiyo, mtu ameumbwa si tu kwa hadhi yake na kama sura na mfano wa Mungu, lakini hata kama mwanaume na mwanamke mwenye uwezo, kwa njia ya ushirikiano wa pamoja wanazaa watoto na kuwalea.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Biashara inapaswa kulenga talanta binafsi na kutosheleza mahitaji ya binadamu kwa zana halisi na endelevu na katika roho ya huduma na mshikamano mbele ya familia ya kibinadamu. Hayo yametolewa na Kardinali Peter Turkson Rais wa  Baraza la Kipapa la Mandeleo fungamani ya binadamu wakati wa kutoa hotuba yake katika siku ya kwanza ya Kongamo la kichungaji ndani ya Mkutano wa Familia duniani unaoendelea hadi tarehe 26 Agosti mjini Dublin nchini Ireland.

Familia ni taasisi iliyopendwa na kuumbwa na Mungu

Katika kuwasilisha  mada hiyo tarehe 22 Agosti jioni, katika  mada iliyokuwa inahusu  wito wa viongozi katika kazi: matarajio ya kazi kifamilia, Kardinali amekumbusha kwamba, kwa mujibu wa Wosia wa Kitume wa Amoris laetitia; familia ni taasisi ya kibinadamu iliyopendwa na kuumbwa na Mungu kwa ajili ya kulea  na kuendeleza maisha  binafsi ya binadamu, kwa maana hiyo, mtu ameumbwa si tu kwa hadhi yake na kama sura na mfano wa Mungu, lakini pia kama mwanaume na mwanamke mwenye uwezo na  kwa njia ya ushirikiano wa pamoja wanazaa  watoto na kuwalea.

Kazi ya mtu.

Iwapo kuna utambuzi wa shughuli ya binadamu ya kulima na kutunza ardhi kwa maana ya kazi, Kardinalia anathibitisha,kwamba hicho  ni kielelezo cha hadhi yake katika sura ya Mungu na hivyo ni kwa namna ya kazi kama utume wa mtu, na  kama binadamu na ambaye anahitaji ili utume wake uweze kuendelea moja kwa moja katika mantiki ya zawadi ambayo kwayo ndiyo hatua ya wema wa  ardhi hiyo iliyopo duniani.

Kazi ni wito mkuu

Katika mtazamo huo anaongeza Kardinali Turkson: kazi ni wito mkuu ambao unaandaliwa na kujikta katika lengo kuu la kupendekeza uumbaji na tunu zake kwa ajili  ya huduma ya familia ambayo inazalisha. Na kwa mtazamo huo familia ni rasilimali ya kudumisha na huduma ya upendo kwa watoto wetu na wale watakao fuata baada yetu.

Wakati huo huo:Kurudia wito katika akili ya maisha na mafundisho ya Yesu kwa kutazama ndani mwake kujifananisha kwa wale wanaoomba ifadhi na wahamiaji waathirika ndiyo mwaliko wa Michael Czerny, Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la meandeleo fungamani ya binadamu katika kitengo ha wahamiaji na wakimbizi , aliotoa wakati wa hotuba yake tarehe 22 Agosti, asubuhi kwenye Kongamo la kichungaji kwenye mkutano wa familia duniani Mjini Dublin mahali ambapo yeye anatazama kwa karibu changamoto ambazo wakimbizi wanakabiliana  nazo na ambapo anasisitiza kuwa ndilo linapaswa kuwa jibu la wakristo katika kipeo hiki.

Kukaribisha mgeni

Kuwa na nafasi, kama sehemu ya mada ya ya mkutano, iliyokuwa inasema hakuna nafasi ya kuweka kicha chake, Padre Czerny ameeleza kuwa, ni kawaida hata ndege na mbwea. Kutokuwa na nafasi ni kawaida. Lakini huo ukawaida kwa upande wa wakristo, haiwezekani ikawa sababu au kidogo kwa bahati mbaya kwa yoyote yule.

Badala yake amekazia kuwa, sisi tunaalikwa kupokea mgeni yoyote yule kwa maana  sisi sote ni kama familia; sisi kama jumuiya katika ukaribu wetu  katika parokia zetu, katika majimbo yetu , mashirika na vyama mbalimbali katolikivya kitume, kwani  maana familia za wahamiaji ni waathirika na siyo tu wahitaji ambao hawana budi kupokea huruma. Wao ni sehemu yetu! amekazia.

Kulinda waathirika:

Kadhalika amesisitiza: familia hizi zinaweza kwa namna moja kusaidia kulinda waathirika katika kuhamsiaha maendeleo fungamani ya kibinadamu na kuweza kuwafanya washirikishwe vema wale ambao wameruhisiwa kuingia. Ni matarajio yake kwamba  Makanisa yetu yote yanaweza kujifunza zaidi kuwasindikiza wahamiaji na hatimaye kuwa Kanisa ambalo linazidi kwa ukuu wake kuwasindikiza familia zote katika mchakato wa haraka wa wenye mabadiliko ya kweli

 

23 August 2018, 16:56